Hapa unapo paona ndiyo sehemu inayo patikana makaa ya mawe eneo la Ngaka, ni eneo ambalo Serikali ili chukua hatua baada ya kuona Makaa yakiungua zaidi ya miaka 4 moto ambao uliigharimu serekali ya Tanzania shilingi milioni 59 kuuzima moto ulio kuwa ukiunguza makaa hayo
Baada ya kufanikiwa kuuzima Moto ulio kuwa ukiunguza Makaa ya Mawe Viongozi mbalimbali walianza kuwasili eneo la Ngaka kuangalia jinsi ya uchimbaji akiwemo Makamu wa Rais Gharib Mohamed Bilali hapo akisalimiana na wamiliki wa machimbo ya TAN COAL
Mh. Makamu wa Rais alipo wasili Mkoani Ruvuma ili kukagua miradi mbalimbali ikiwemo machimbo ya Mawe ambayo yameonyesha kuleta ufanisi Mkoani Ruvuma
Kampuni ya TAN COAL ikiwa kazini kuchimba Makaa ya Mawe na kuweza kuwatia tumaini wakazi wa Ngaka kuona sasa umasikini utawatoka kwa kuajiliwa pia kuweza kuuza bidhaa zao kiurahisi eneo la Machimbo
Kamati ya Bunge inayo husiana na Viwanda ilipotembelea eneo la Machimbo na kuhakikisha kuwa Wananchi wako shwali na Machimbo hayo, pia ilifanya mkutano na wananchi na wao kudai ajira. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Saidi Thabiti Mwambungu akiwa mmojawapo aliye wahi kufika na kuchukua Changamoto za Ajira katika eneo hilo.
Viongozi waandamizi wa NDC nao waliweza kuhudhulia vikao mbalimbali ambavyo vilikuwa havina migogoro mikubwa, zaidi wana kijiji waliomba huduma muhimu kama Maji, Ajira, Pamoja na wao kupewa kipaumbele kwa mambo Muhimu
Mmoja wa Maafisa wa TAN COAL ndugu Didi aliweza kuihakikishia Kamati ya bunge juu ya Ajira kuwa atatoa kipaumbele kwa wazawa lakini alitoa angalizo atatoa ajira kutokana na Elimu waliyo kuwa nayo na si vinginevyo
No comments:
Post a Comment