Kilimo cha Tumbaku kime kuwa ni ukombozi kwa wakulima wa wa Mkoa wa Ruvuma,Lakini changamoto zinazo wapata zina rudisha mori wa kuendeleza zao hilo.1.wakulima wa Mkoa wa Ruvuma walikuwa na kiwanda cha kusindika Tumbaku ambacho kilikuwa na uwezo wa kuajiri wafanyakazi 2000lakinihivi sasa kiwanda hichohakifanyi kazi kwa muda wa zaidi ya miaka 10
Katibu wa Kampuni ya LIFADA ya Wilaya ya Namtumbo Mohamed Kakwila akiwa Shambani huku akiwa na masononeko ya kuuza Tumbaku kwa bei ya Chini ambayo ime pangwa na Makampuni, Jambo lingine linalo msonenesha ni liba kubwa inayo tozwa na benk wakati wa kuomba kupata mkopo wa kununua pembejeo,Hapo awali walikuwa wakipewa Pembejeo na ATTT na wakati mwingine umoja huo wa ununuzi wa Tumbaku Mkoa wa Ruvuma walikuwa wakilipa Fidia endapo mkulima ana pata hasara hivi sasa Jambo hilo ni la Mkulima
Mama akiwa shambani akiwa na Furaha jinsi tumbaku yake ilivyo kubali na akiwa na Tegemeo la Kupata Mahitaji Mhimu kama Matibabu,Kusomesha,na kuwa na Fedha za dharura lakini ndoto hizo hutoweka baada ya kukutana na bei isiyo ridhisha,Wafanye nini wana Ruvuma ili wainue uchumi wao
Juhudi za kuongeza Zao la Biashara lime pata Mwitikio katika Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma hilo ni shamba lilioko Lionde Namtumbo Vijijini hapo mama anaonekana akivuna Tumbaku yake anacho sikitika ni wakati wa kupanga madaraja ndipo wanapo angushwa wa kulima wameomba serekari kuwa jicho la wakulima pale wanapopangiwa madaraja
No comments:
Post a Comment