KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, March 30, 2012

INTERNATIONAL CENTER FOR EYE CARE EDUCATION EAST AFRICA WATOA VIFAA VYA TIBA YA MACHO

Mwakilishi kutoka ICEE Uganda Dr Naomi Nsubuga akitoa tarifa jinsi shirika la ICEE Internatinal Center for Eye Care Education East Africa ili navyo pambana na kutokomeza magonjwa yanayo husu Macho akiwa Mkoani Ruvuma,


Mguzi mkongwe katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma bwana Ndunguru akiwa katika ufunguzi wa kituo cha Macho Mkoani Ruvuma

Kaimu meneja wa mipango ya Taifa wa Huduma za Macho Dkt Bernadetha Shiro akieleza nia ya serekari katika mikakati ya mkukuta katika kupambana na maradhi ikiwemo maradhi ya macho ifikapo mwaka 2016 kutokomeza magonjwa ya Macho

HOSPITALI YA MKOA WA RUVUMA WAPATA MSAADA WA VIFAA TIBA

Kaimu katibu tawala mkoa wa ruvuma Weston Nganiwa akitoa tarifa ya wagonjwa wa macho mkoa wa Ruvuma kabla ya kukabidhiwa vifaa vya macho na Kaimu Meneja wa huduma za macho kutoka Dar -es - salaam

Kaimu Katibu tawala Mkoa wa Ruvuma akieleza hali halisi ya utendaji kikazi katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma

Mtalamu wa upimaji wa vifaa vya Macho akimwelekeza Kaimu katibu tawala Weston Nganiwa jinsi vifaa hivyo vinavyo weza kufanya kazi kiurahisi kumpima mgonjwa

Dkt Idda Ngoi akiwa karibisha wageni kutoka Uganda ambao walikuja kukabidhi vifaa vya tiba ya Macho vyenye samani ya shilingi milioni 35


Dr Chanangula akiwasilia na watalamu wenzake katika kufanikisha ufunguaji wa kituo cha tiba ya macho Ruvuma

Tuesday, March 27, 2012

THE FOUNDATION NA AZAKI KATIKA MAENDELEO

Mkatibu wa Asasi ya SONNGO kutoka mkoani Ruvuma akisikiliza kwa makini namuna ya kumutoa Mwananchi katika umasikini kwa kutumia Rasilimali tulizo nazo

Jamii ya wafugaji wakiwa katika eneo la Ruaha mkoani Iringa wakiangalia shamba la mabondeni ili kuweza kulima mahindi,Mpunga, na Mbogamboga

Mkoa wa Iringa una utaratibu wa kuhifadhi maeneo yaliyo mabondeni kwa kutoa elimu ili wananchi wasilime ovyo ili kulinda vyanzo vya majiWatoto wadogo huwa watafiti kwa mambo mengi wakiangalia kitu mara moja huweza kutengeneza kitu kinacho lingana na kitu walicho kiona, Hapo wapo Darasani lakini mara baada ya kufika wandishi wa Habari hawakuweza kuvumilia ,waliuliza maswali jinsi Kamera zinavyo chukua Picha ,wanafunzi hao ni kutoka shule ya Mtunduwalo kwenye Machimbo ya Makaa ya Mawe Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma

Uwapo jijini Dodoma kwa vifaa mbalimbali vya umeme fika katika duka la Kazi Moto liko nyuma ya Jengo la au numa ya jengo la CCM Makao makuu Dodoma hapo ni viongozi kutoka mkoa wa Ruvuma walio Tembelea Duka la Kazimoto

Thursday, March 22, 2012

MJUMBE KUTOKA TGNP AKITOA MAADA KUHUSU KAZI ZA

Mwakilishi wa Mungano wa Mashirika yanayo Tetea Haki za Akina Mama Badi Darusi ambaye ni mjumbe wa JPE pia ana tokea mtandao wa TGNP Hapo anaonekana akipongeza Juhudi zilizo fanywa na Wajumbe wa Mkoa wa Ruvuma ambao ni wajumbe wa TGNP kwa kuweza kujenga jengo la POLICE Wanawake mjini Songea Mada hiyo aliitoa akiwa katika ukumbi wa Dodoma Hoteli


Mwakilishi wa Azaki kutoka Bukoba ambaye anaasili ya Kijerumani akiwa katika Mfunzo ya Kuandika Tarifa za Miradi The Foundation Mafunzo yaliyo fanyika katika Hoteli ya Dodoma

Wednesday, March 21, 2012

DR SILAHA NA KAMPENI

Ndugu mtazamaji hebu niambie umati huu una ashiria nini naomba maoni yako kwenye mtandao huu ni vizuri ukawa mwazi toa fikira zako bila kushawishiwa kila mtanzania ana haki ya kusema lile lenye faida kwa jamii ijinsi ya kuto maoni bonyeza hapo palipo andikwa comment halafu andika

RAIS DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE AWAAPISHA WA KUU WA MIKOA YA NJOMBE,GEITA,KATAVI NA SIMIYU

mkuu wa mkoa wa Simiy kapt Paschal Kulwa Mabiti akiapishwa jijini Dar -es -Salaam na Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Rajabu Mtumwa Rutengwe akiapa mbele ya Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete jijini Dar -es - salaam


Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Geita Mh Magalula Said Magalula akiapa mbele ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Mkuu wa Mkoa wa njombe kapt Asery Msangi akiapa mbele ya Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mh. Dr Jakaya Mrisho Kikwete

KWA NINI KAMPENI ZA UCHAGUZI ZIFANYWE NA WATU WA INJE JEE WALIOPO HAWA WEZI ?

Ndugu Msomaji wa Mtandao huu napenda nirudi Mwaka 1964 wakati tulipo ungana na Serekari Zanzibar tulichagua ngao inayo ashiria serekari ya Tanzania Ngao ina itwa Adamu na Hawa.

Nembo hii inaashiriria Serekari ya Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania na Serekari bila katiba haiwezi kwenda .Ndani ya Katiba kuna ibara ambayo inasema kila mtu ana huru wa kutoa mawazo yake na kwenda kokote anako taka bora kama havunji sheria.

Hebu sasa niende kwenye Mada yangu Mahususi, Utamaduni ulio ibuka sasa Tanzania unamnyima mtu kutoa mawazo yake, Kwa mfano mtu ambaye ni kiongozi aliye chaguliwa awe Diwani au Mbunge akifariki tu nafasi ikiwa wazi watu hujitokeza kugombea .

Sasa cha ajabu ni kuwa Mgombea akisha chaguliwa kugombea kupitia CCM au CHADEMA .Badala ya yeye mwenyewe kupiga kampeni badala yake wapiga kampeni hutoka Dar-es- salaam au sehemu nyingine jambo ambalo lina wachanganya mwananchi wa pale na kupata kiongozi ambaye siyo bora kama waliye kuwa wana mtaka wao.

Nikitoa Mfano katika Kata ya Hanga wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma wananchi walimchagua Diwani aitwaye Kasimu Ntara ,kwa kuwa alikuwa hana sehemu ya kukaa alienda kukaa kwenye nyumba ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Mageuzi Mwenyekiti ajulikikanaye kwa Jina la Saidi Kupata,

Mwenyekiti alimkaribisha Nyumbani kwake cha ajabu badala ya kusimamia kazi za maendeleoDiwani huyo Kasimu Ntara akaingia katika swala la mpenzi akampa mimba mtoto wa Mwenyekiti Said Kupata ambaye alikuwa kidato cha pili .

Viongozi wa Ngazi za Juu baadala ya kumwajibisha Diwani Kasimu Ntara badala yake Baraza la Madiwani wa kamteua Diwani Kasimu Ntara kuwa Makamu Mwenyekiti mbali ya kufanya kitendo kiovu kwa mtoto wa Mwenyekiti Said Kupata

Sasa hii ina vunja mioyo kwa wananchi Diwani huyu Kasimu Ntara ni wanamna gani kwa nini asiajibike badala yake anaongezwa cheo kuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani ,jee ana weza kusimamia maendeleo kwa upande wawatoto wa kike .

Kwa ushauri wangu wagombea wangeachwa wenyewe ili wananchi wapate nafasi ya kuwa tafakari kuliko kuleta majeshi kutoka nje siku ya siku viongozi hao wanaishia kuwapa mimba watoto wa viongozi na masikini

Tuesday, March 20, 2012

THE FOUNDATION CIVIL WANATARAJIA KUTUMIA BILIONI 4 KUTOA UELEWA KWA WANANCHI ILI KUPATA MAENDELEO PALE WALIPO

Omary Jecha kutoka The Foundation akitoa elimu ya uandishi wa Tarifa kwa Azaki kutoka Tanzania bara na Tanzania Kisiwani walio shiriki kataka ukumbi wa Dodoma Hotel.Aidha The Foundation Civil wanategemea kutumia shilingi bilioni 4 ili kutowa uelewa kwa wananchi kupitia Azaki zilizopo ili kuwaondoa katika umasikini na kuweza kujua haki zao kwa upande wa Serekar

Mwandishi wa kimataifa wa ndani na inje katika kuendesha midahalo kupitia televisheni ya Star Tv ambayo hupasua mawimbi kwa kusikika inje ya mipaka ya tanzania . Hapo Mwandishi huyo Rosemary Mwakitwange akiratibu maswala mbalimbali.


Mwana harakati kutoka Zanzibar akichangia hoja kuhusu ushiriki wa wabunge Tanzania Hapo anatoa uzoefu kuhusu ushiriki wa wabunge katika midahalo imebainika kuwa ushiriki wawa bunge ni chini ya asilimia 35% Tanzania Mzima


Washiriki kutoka Tanzania bara na Kisiwani wakishiriki mafunzo kuhusu uandishi wa kuandika tarifa wakiwa ukumbi wa Dodoma Hoteli

Friday, March 16, 2012

RAIS ATEUA WA KUU WA MIKOA MIPYA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete
Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa mipya minne iliyotangazwa na Serikali hivi karibuni. Katika uteuzi huo uliyotangazwa jana Rais Kikwete amemteua Dk. Rajab Mtumwa Rutengwe kuwa Mkuu wa Mkoa wa KATAVI.Wengine walioteuliwa ni Magalula Saidi Magalula anayekuwa Mkuu wa Mkoa wa GEITA, Paschal Kulwa Mabiti ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa SIMIYU na Kapt. Asery Msangi anayekwenda kuongoza Mkoa wa Njombe, kabla ya hapo Kapt. Msangi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa.Kwa upande wake kabla ya hapo Magalula kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dk. Rutengwe kabla ya uteuzi huo mpya alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda huku Mabiti alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida.Kwa mujibu wa taarifa hiyo kutoka mawasiliano Ikulu viongozi wote hao wanatarajiwa kuapishwa Machi 21, 2012 Ikulu jijini Dar es Salaam, saa 04:00 asubuhi na uteuzi huo umeanza tangu jana Machi 15, 2012.

Thursday, March 15, 2012

MAJINA MATATU YA PELEKWA KWA RAIS DR JAKAYA MRISHO KIKWETE

Mjumbe kutoka Tamwa Flola Nzema akitoa maelezo kwa mjumbe wa bodi ya UTPC Juma nyumayo pia akibalilishana mawazo kujadili mada itakayo wakilishwa katika kongamano la Azaki za Tanzania Bara kuhusu swala la Habari

Mjumbe kutoka TAMWA Flola akiwakilisha mada katika kongamano kubwa lililo huska wajumbe 223 kutoka Tanzania kongamano lililo fanyika jijini Dodoma kuhusu ushirikiano wa vyombo vya habari na Azaki zilizopo katika Tanzania , kushirikiana na vyombo vya habari ni moja ya nija mnzuri ya kufikisha mawasiliano kwa wananchi.


Mwenyekiti kamati ya kuhesabu kura za majina ambayo yata pelekwa kwa mheshimiwa Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete ili aya teue kujiunga na kamati ya kuratibu maoni ili kupata katiba mpya hapo Keny Ngomuo ana onekana akitoa majina yaliyo chaguliwa na wajumbe Dodoma

Wajumbe mbali mbali wakipiga kura ili kuchagua majina matatu ta takayo pelekwa kwa Mheshimiwa Rais majina yaliyo teuliwa ni kama yanavyo onekana hapo chimni

Majina yaliyo teuliwa kupelekwa kwa Rais yalikuwa matatu yaliyo pata kura za juu nayo nihayo yafuatayo 1.John Ulanga aliye pata kura 114, Pr Ruth Mena aliye pata kura 97 na Humprey Polepole aliye pata kura 90

Wajumbe wakiwa makini katika upigaji wa kura kuteua majina matau yatakayo pelekwa ikulu kwa Rais mjumbe wa kamati Tabia Kobe akikusanya kura baada ya wajumbe kupiga






wajumbe wakiwa Dodoma wakihudhuria kongamano la Azaki kutoka Tanzania Kisiwani na Tanzania bara

kwenye mkusanyiko hakukosekani watu wengine kutafakari kwa kina hapo mjumbe akitafakari kwa makini kuhusu kongamano la Dodoma la kuchagua wajumbe 3 wa mchakato wa katiba

Tuesday, March 13, 2012

MCHAKATO WA KUCHAGUA WA JUMBE WA MAJINA YATAKAYO PELEKWA KWA RAISI KWA AJILI YA KATIBA

Juma nyumayo katika kongamano jijini Dodoma la mchakato wa katiba akiwa ameketi katikati


Moja ya Wajumbe walio hudhuria ni pamoja na walemavu kama unavyo waona hapo juu

washiriki wa kongamano la kuhusu kuchagua wajumbe ambao watapelekwa kwa Rais ili majina hayo ya ingie katika kupokea maoni ya kuhusu katiba mpya dada mjerumani anaye onekana ni Lena Turowski kutoka mtandao wa KAPUMU [Kazi pamojs Muleba kushoto kwake ni Denes Kibamba

Mwenyekiti wa Mchakato wa Katiba Tanzania Deusi Kibamba akitoa maelezo katika kongamano ya kuchagua majina yatakayo pelekwa kwa Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa ajili ya kushiriki mchakato wa katiba mpya

wajumbe kutoka maeneno tofaauti nchini Tanzania wakijalili majina yatakayo pelekwa kwa mh.Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania kushiriki mchakato wa Katiba Mpya

Wajumbe kutoka Mkoa wa Ruvuma walio shiriki katika mchakato wa kuchagua wajumbe watakao ingia katika mchakato wa kujadili majina yatakayo pelekwa kwa Rais wakiwa katika ukumbi wa Dodoma Hotel katika ni Mathew Ngalimanayo na wa kwanza ni Adamu Nindi

Sunday, March 11, 2012

BABA WA TAIFA ALISEMA HAPENDI MICHEZO KUTOKANA NA MCHEZO WA AMANI KUGEUKA KUWA UWANJA WA MASUMBWI

Wanaume wakiwa wame mbeba shabiki wa yanga baada ya kuleta fujo uwanjani jee hiyo ni halali kuleta fujo kwenye sitarehe
Mtu mzima kama huyu anaenda uwanjani analeta vurugu akipigwa na wanaume ana anza kulaumu hivi usipo leta fujo huta faidi mchezo watanzania tujifunze kuwa na busara
kupenda ni ugonjwa aliye bebwa ni mpenzi wa yanga hapo akiwa amebebwa baada ya matokeo ya yanga na azamu kuifunga yanga mabao 3-i jambo lililo mfanya shabiki huyo azimie

Saturday, March 10, 2012

NYOKA ULIYE MUA NI RAFIKI WA BINADAMU

Dada oliver Moto huyo nyoka uliye mua hana hatia kwanza kwa tabia yake ni rafiki wa binadamu katika maisha niliyo kuwa na ishi vijijini nyoka huyu wa kijani alikuwa ni nyoka ambaye alikuwa ana cheza na watoto sija tokea kuona anauma akiuma mtu ujue kijijini hapo kuna jambo baya lina weza kutokea

Nikawaida ya nyoka huyo kukaa katika paa la nyumba au kama umepanda miti ubani hao nyoka hupenda kuishi humo pia huyo ni pambo ni ajabu kusikia wanaume wana mkimbia sisi kwetu uta kuta mtoto kamuvaa shingoni ,kama kweli wanaume walimkimbia basi ujasili ume toweka hapo Iringa, Ila hongera kwa kuonyesha Mwanamke ana weza

JEE HII NI HALALI TOA MAONI


Shetani huna mamlaka ndani ya binti huyuna kuamuru toka toka toka , Toa Maoni yako

WANANCHI WA RWANDA WILAYANI MBINGA MKOANI RUVUMA WADAI NYONGEZA YA FIDIA KWA SEREKARI

Jopo la Viongozi waandamizi wa Mkoa wa Ruvuma wakingoja kuendesha mkutano wa suluhu kati ya wanakijiji cha ngaka na wachimbaji madini ya Makaa ya mawe ,Madai ya wananchi ni kuwa fidia waliyo pewa hailingani na bidhaa walizo kuwanazo, pili kwa kipindi cha miaka 61 wameendeleza eneo hilo mpaka serekari inapo baini kuwa kuna madini jee hawawezi kulipwa fidia kutokana na kulinda madini hayo kwaq kipindi kirefu,


Wananchi wa kijiji cha Rwanda wakiwa kwenye uwanja wa shule ya msingi wakingoja mkutano wa suluhisho kuhusu fidia kati yao na campuni ya STAM COM wachimbaji wa Makaa ya mawe Ngaka



Pichani hapo chini ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Saidi Thabit Mwambungu akirejea baada ya kushindikana kutoa usuluhisho ya maadai ya wanakijiji cha lwanda kudai kupewa fidia ndogo na wachimbaji wa Makaa ya Mawe STAM COM kutokana na mvua kubwa iliyo nyesha na hatimaye kuairisha kikao hadi mwishoni mwa mwezi huu

Moja ya Mafanikio ya madai ya wanawake kupata uongozi unaye mwona hapo mbele ni Afisa Tawala wilaya ya mbinga mkoani Ruvuma akitoa Maelezo kuhusu chanzo cha siku ya wanawake Duniani

Kikosi cha jeshi la police kikitasimini mafanikio na changamoto zinazo likabili police wanawake katika siku ya wanawake duniani ikiwemo na utoaji wa elimu kwa upande wananchihasa wanawake