Familia ya Mama Alice Matembo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Mazishi ya Alice Matembo. Mungu alitwaa na Mungu amechukua apumzike kwa amani amin.Picha kwa hisani ya kakayake Adam Mzuza Nindi
Barabara ya Tunduru - Songea inavyoonekana baada ya barabara hiyo kuwa changamoto kwa watu wanao safiri kutoka Songea vs Tunduru wakati wa mvua za masika pichani ni eneo la Kilimasela lori ikijaribu kushindana na udongo wa mfinyanzi
Pichani ni Mahakama Mpya ya Nakapanya ambayo kibao chake kimeonyeshwa hapo juu ikiwa imejengwa vizuri imeezekwa kwa bati ikiwa imezungukwa na nyasi Jee Kukwaa Nyasi kuzunguka Mahakama hiyo ni jukumu la Serikali au Wananchi? Jee Ikitokea Nyoka kuvamia wakiwa wanaendesha kesi humo Mahakamani jee nyoka kuwa katika eneo hilo watakuwa wanakosea au watakuwa sahihi kwa kuona yanafanana na makazi yao?
Pichani ni Mahakama ya zamani ya Nakapanya wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma ambayo wamehama na kuhamia Mahakama Mpya kutokana na uchakavu swali la kujiuliza jee hali inayoonekana hapo juu ina tofauti gani na ile mpya ambayo wamehamia. Jee Serikali haipati hasara kwa mazingira kama haya.?
No comments:
Post a Comment