
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi Maimuna Tarishi aliyesimama akitoa ahadi ya kuisaidia kujenga uzio kuzunguka Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji Songea wakati wa maadhimisho ya siku ya mashujaa February 27 mwaka huu katika Viwanja vya Mashujaa Mahenge Manispaa ya Songea, katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu na kulia ni Chifu wa Makumbusho ya mashujaa Chifu Emmanuel Zulu Gama.

Msanii wa Vichekesho vya kuigiza Bw. Athuman Keneth akitumbuiza kwa kuonyesha Vimbwanga vya kijadi katika maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa Mjini Songea.

Viongozi wa Serikali wakifuatilia kwa karibu maonyesho mbalimbali katika sherehe za siku ya mashujaa february 27 mwaka huu katika viwanja vya makumbusho ya majimaji kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa Mstaafu Meja Jenerali Said Kalembo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Joseph Simbakalia, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii bi Maimuna Tarishi, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu na mwishoni mwenye suti nyeupe ni Mkuu wa wilaya ya Songea Thomas Sabaya.

Msanii Athumani Keneth akionyesha vitu vyake mbele ya mgeni rasmi katika sherehe za mashujaa wa vita vya majimaji katika viwanja vya Mashujaa Mahenge Mjini Songea.
Kikundi cha ngoma ya asili ya kingoni maarufu kwa jina la Libihu wakiwa na zana za jadi mara baada ya kuonyesha gwaride la kingoni katika maadhimisho ya vita vya Majimaji.
No comments:
Post a Comment