MAJIBU YA WAHUSIKA WA TTCL KUJIBU TUHUMA ZA WANCHI WA MKOA WA RUVUMA
KAMPUNI ya mitandao ya simu nchini TTCL imesema tayari imekamilisha matengenezo ya matatizo ya mtandao katika Mkoa wa Ruvuma. Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo, Amini Mbaga, alisema tatizo la kukatika kwa mtandao kwa baadhi ya wateja wa mkoa huo limekwisha kwa kuwa tayari mafundi wameshalirekebisha. Mbaga alisema tatizo hilo lilisababishwa na radi, hivyo baadhi ya mitambo kuharibika na kukosekana kwa mawasiliano katika baadhi ya maeneo ya mkoa huo, lakini kwa sasa wateja wataendelea kupata huduma hiyo muhimu kama kawaida. “Hilo tatizo lilikuwepo awali, lakini kwa sasa mafundi wetu wamesharekebisha, na tunategemea huduma zitarejea kama kawaida. Na tatizo hili lilisababishwa na radi ambayo iliharibu baadhi ya mitambo ambayo hata hivyo imeshatengamaa,” alisema Mbaga. Aliongeza kuwa mtandao wa kampuni hiyo hauhusiki na huduma za kibenki mkoani humo kama ilivyodaiwa na wananchi wa mkoa huo hapo awali na hivyo usumbufu wa kibenki wanastahili kuulizwa wahusika. Baadhi ya wananchi wamekuwa wakisema kwamba mitandao inayohusika na benki imekuwa ikikatikakatika kutokana na huduma hafifu za TTCL.
WAZIRI WAMAWASILIANO KAMAHAWEZI KUWAHUDUMIA WANANCHI BASI AJIUZURU
Kwa Muda mrefu sasa watanzania wamekuwa wakishuhudia Tuhuma mbalimbali zikienda kwa viongozi , Tuhuma hizo zina enda kwa viongozi kwa kuwa dhamana ya kuwaongoza wananchi wame kabiliwa wao.
Tukienda kwe mada yetu tume ona mashirika mengi yalitaifishwa kwa manufaa ya uma ili wananchi wasiendelee kupata hasara na uendeshaji wa mashirika hayo ambayo yalikuwa haya leti faida kwa wananchi.
Katika mashirika mengi yaliyo binafisishwa ili kuwa moja wapo ni Bank , viwanda mbalimbali, pamoja na sekita nyingine nyingi ambazo wana nchi wanazijua,
Sasa hebu tuone shirika lililo baki mikononi mwa Serekari ambalo ni TTCL hivi sasa shirika hili limekuwa mkombozi kwa upande wa mawasiliano kwa njia mbalimbali .Mabank mbali mbali yana tumia mawasiliano kwa kusafirisha fedha, wanchi kupata mawasiliano kwa njia ya Intenet jambo ambalo wanchi wamefurahia;
Kwa hivi sasa yapata mwezi mmoja shirika hili TTCL Mkoa wa Ruvuma lime shindwa kabisa kuwa hudumia wananchi misururu mikubwa mkoani Ruvuma wamekuwa wanajipanga bank lakini kwa masikitiko mabwa Mameneja hutoa tarifa kuwa huduma ya TTCL hakuna, Jee kitu nyeti kama hiki kwa nini kikwame kwa muda wa mwezi mzima bila utatuzi wakati shirika hili liko mkononi mwa serekari .
Mitandandao mingine ambayo ina toa huduma za kibank shuguli zao zina endelea kama kawaida na campuni hizo hutoza garama kubwa lakini bado zinadunda jee wananchi wakisema waziri husika ana husika na kukwama kwa TTCL ata kataa ? tunamba omba kama waziri wamawasiliano ameshindwa kazi basi ajihudhu
Mimi binafisi nimeomba maelezo ya kina kutoka kwa meneja wa TTCL bwana Chanachayo hana majibu ,fundi mkuu wa TTCL Mkoa wa Ruvuma bwana Maburuku naye hana majibu
Mkuu w Mkoa wa Ruvuma Mh. Said Thabit Mwambungu naye hana majibu amesema atafuatilia.
Jee shirika hili TTCL lina uwawa kinyemela hivi wanyonge wata kimbilia wapi
No comments:
Post a Comment