Asikari wa kikosi cha kuzuia ghasia akiwa amekaa katika shamba la bangi huko Magagula Songea Vijijini
Majirani walioko katika mashamba ya bangi songea vijijini wakibadilishana mawazo na Asikari wa kikosi cha kuzuia ghasia
|
kazi ya kufika katika maeneo wanayo lima Bangi siyo Rahisi hapo Asikari wa Kikosi cha kuzuia ghasia akivuka katika madaraja mabovu yalioko Songea vijijini |
Mkongwe wa Habari Adamu Mzuza Nindi akiwa katikati ya shamba la bangi usitawi huo unatokana na pembejeo zinazo tolewa na serekari [VOCHA mkulima huyu akiwa amelima hekari moja na nusu Bangi hiyo ni kama unavyo iona
Kamati ya ulinzi na Usalama ikiwa ina panda na kuteremuka katika Milima ya Ngaokola Songea Vijijini tayari kwa kwenda kuteketeza Bangi, Ukifika huwezi kuitambua sehemu inapo limwa pembeni kuna zunguka Mahindi au Ufuta
Kamati ya Ulinzi ya Wilaya ya Songea ikiteketeza Bangi pamoja na Kung'oa Masalio ya Shina la Mti wa Bangi
Ukisogea Hapo kama usipo jua kanuni za Bangi utajikuta umevuta bangi bila kutarajia baadhi ya watu walio kuwa hawajui kanuni za Bangi walijikuta Wakiwa wamelewa bila Kutarajia ,Unauona Moto huo ?
Maeneo yaliyo pandwa Bangi kuna kuwa na Walinzi wa Jadi Unaye Mwona hapo ni Mbwa ambaye kazi yake ni kunusa harufu ya Mtu anaye karibia katika shamba la Bangi halafu hubweka kwa nguvu kuwa fahamisha walimaji Haramu wa Bangi kuwa kuna adui ana kuja Mbwa hao wako zaidi ya Sita
|
Katibu Tarafa wa Mhukuru Songea Vijijini Salima Mapunda akiwa ame beba Bangi tayari kwa kuteketeza |
Mkuu wa Wilaya ya Songea
Joseph Joseph Mkirikiti amewataka Vijana kuacha kutumika kwa kazi haramu kama Kilimo cha Bangi ambacho kinaleta Madhara kwa watumiaji na hata kuwasababishia kuwa vichaa.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Songea (OCD) Alfred Kasoro
amesema walimaji wote wa Bangi orodha yake anayo pia anajua
Viongozi wa Kisiasa wanaosimamia zoezi la ulimaji wa Bangi. Pichani ni Mkuu wa Polisi wilaya ya Songea Akongoza zoezi la kuing`oa Bangi katika kupambana na madawa ya kulevya.
OCD Alfred Kasoro akionyesha mfabo wa kutofurahishwa na wale wote wanaoendelea na ulimaji au biashara ya Bangi amesema kampeni hii ya kuteketeza na kuwasaka wahusika wa shughuli hizi imezinduliwa na Mkuu wa wilaya ya Songea itakuwa endelevu katika wilaya ya Songea.
Mkuu wa Wilaya ya Songea
Joseph Joseph Mkirikiti akiteketeza shamba la Bangi lenye
Ukubwa wa Ekari moja lililoko katika Kijiji cha Ngaokola Songea Vijijini Mkoani
Ruvuma, amesema dhumuni la Serikali inapotoa vocha za kilimo ni kusaidia kuwainua wakulima wadogo ili waimarike kiuchumi lakini badala yake inashangaza kuona vocha hizo zikitumika katika kuimarisha Kilimo cha Bangi.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Songea Sixbert Valentino amesema amewaagiza watendaji wote katika Tarafa ya Mhukuru kukagua mashamba yanayotiliwa wasiwasi
kwa Kilimo cha Bangi. Picha unayoiona ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri akishangaa jinsi bangi ilivyohudumiwa na kustawi vizuri.
Safari ya kuelekea Kijiji cha Ngaokola Songea Vijijini haikuwa rahisi kutokana na barabara na madaraja kuwa ya hatari kama unavyoona pichani Askari wa FFU wakitengeneza mazingira ya kusaidia gari kuvuka katika Daraja hiyo ya Miti.