Nikikao kizito kujadili Changamoto za Manspaa na za Mkoa wa Ruvuma ,Wakiwa asikari wa Mwavuli kuhakikisha swala la Maendeleo Mkoa wa Ruvuma Lina pewa kipao mbele, Kulia ni Mbunge wa Songea Mh. Dr. Emanueli John Nchimbi na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Saidi Thabiti Mwambungu
Mbunge wa Jimbo la Songea Dr. Emanuel John Nchimbi akikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi magari matatu yaliyo fadhiliwa na Benki kuu ya Dunia kwa ajili ya kuzoa takataka katika Manspaa ya Songea
Mara baada ya Kuya kabidhi magari hayo Wananchi wakishangilia aliye vaa shati Jekundu ni Meya wa Songea Chares Mhagama
Mbunge wa Jimbo la Songea Dr. Emanuel John Nchimbi Amesema Mafanikio Ya Kupata Magari hayo yametokana na Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mh. Dr.Jakaya Mrisho Kikwete kusimamia maombi ya ufadhili kutoka Benk kuu ya Dunia akishirikiana na uongozi wa Mkoa wa Ruvuma.
Mwonekano wa Magari hayo aina ya Issuzu yakiwa na Utepe kuonyesha kuwa ni mapya na yanauwezo wa kuzoa Taka bila wasiwasi cha Msingi ni wananchi kuunda kamati za kuwezesha kuzoa Taka kwa kujiwekea fedha kwa kila huba kusaidia Mafuta
Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mh. Dr. Emanuel John Nchimbi akiliwasha gari aina ya Issuzu kuoinyesha Magari hayo ni Kamiri na Imara
Mbunge wa Jimbo la Songea Mh.Dr. Emanuel John Nchimbi amewataka
wananchi wa Manspaa ya Songea kuwa na tabia kuchukia Uchafu na kubuni mbinu
mbalimbali za kukabiliana na ongezeko la Taka kwa kusimamia sheria walizo
jiwekea.
Mbunge wa Jimbo la Songea Mh.Dr. Emanuel John Nchimbi ameyasema
hayo wakati akikabidhi magari matatu mawili makubwa kwa ajili ya kuzolea taka
na Moja dogo kwa ajili ya matumizi ya Manspaa ya Songea yakiwa yame gharimu
kiasi cha shilingi 478,986,584.00/=
Gari dogo kwa ajili ya Matumizi ya Manspaa likiwa limepambwa tayari kwa kukabidhiwa kwa Manispaa ya Songea,
Mbunge Mh. Dr.Emanuel John Nchimbi amesema pamoja na mradi wa magari kukamilika swala la kuboresha miundo mbini ya Maji tayari limepatiwa ufumbuzi kwa kutengewa bilini moja katika bajeti ijayo,mbali ya miundo mbinu ya Maji mradi wa kujenga kilometa 15 katika manspaa ya Songea uko tayari.akizungumuza kuhusu Umeme katika kata ya Lilambo amesema serekari imeridhia kujenga Transfomer mbili
Katika ghafula hiyo ya kukabidhi magari wananchi wa manispaa ya Songea wamemwomba Mbunge wao kuwakilisha kilio chao katika bunge la katiba kuwa wao wana unga mkono kwa wale wote wanao taka serekari mbili
No comments:
Post a Comment