KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, April 10, 2014

WAHAMIAJI HARAMU KWA NINI WANA PENDA NJIA KUPITIA MKOA WA RUVUMA ?

Afisa uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Kokwi Lweba ndiza akieleza uingiaji wa wahamiaji haramu katika Mkoa wa Ruvuma ,Amesema adha inayo wapata wahamiaji haramu kwa kupita njia zisizo halali ni kubwa mno wengi hunyang'anywa vitu vyao pamoja na kufanyiwa vitendo vya kinyama ni bora kufuata njia zilizo halali majuto ni mjukuu
Wahamikaji hao wan ne kutoka Pakistan wakiongozwa na Muhamad Ally wamesema mbali ya kuporwa fedha, simu na nyaraka za kusafiria wao wanaomba Serikali ya Tanzania na Ubalozi wa Pakistan uweze kuwarudisha kwao Karachi Nchini Pakistan wakaanze Maisha mapya

Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma imewakamata Wahamiaji Haramu 4 kutoka Pakistan ambao walitaka kuvuka Mpka kwa kupitia Boda ya Magazini kuelekea Msumbiji. Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza amesema Wahamiaji hnao Haramu kutoka Pakistani  Muhamad Sadick Maliki,Tewir Shari Ahamad,Sohuir Mohamed Bath,na  Muhamed Shahid Aly walivuka katika Boda ya Magazini Wilaya ya Namtumbo Kuelekea Msumbiji  ambako walikamatwa na Askari wa Doria WA Msumbiji ambao waliwapiga na kuwanyang`anyang`anya vitu walivokuwa navyo ikiwemo Dola 130 za Kimarekani


Mkoa wa Ruvuma kutokana na kuwa na Pori kubwa umbali wa kilometa 178 njia zote zikiwa na Msitu mkubwa ndiyo chanzo cha Wahamiaji Haramu kutumia njia hizo za Mhukuru – Mkenda na Magazini Namtumbo Vijijini kwa ajili ya kusafiri kwenda nchi jirani  Afrika ya Kusini.
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Kokwi Lweba ndiza amesema Wahamiaji hao haramu wanadai waliingia Nchini Tanzania tar 6/3 wakiwa na Hati za kusafiria (Paspoti)jijini Dar –es – salaam , lakini hilo halijathibitishwa ila kutokana na Majeraha waliyokuwa nayo kwa madai ya  ya kupigwa na Asikari wa Msumbiji pamoja na kufungwa kamba zilizo leta majeraha mikononi na miguuni  , kwanza wanapelekwa Hospitali kutibiwa ndipo uchunguzi utakapofanyika

No comments:

Post a Comment