KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, April 3, 2014

UZUNDUZI WA MRADI WA UZAZI WA MPANGO NAMTUMBO MKOANI RUVUMA

 Shirika lisilo la Kiserikali la MARIE STOPES Tanzania limezindua Mradi wa Huduma za Uzazi wa Mpango na upimaji wa VVU Mkoa wa Ruvuma ikiwa ni mwendelezo wa utoaji wa huduma hizo katika Mikoa 26 ya Tanzania. Uzinduzi huo umefanywa katika Wilaya ya Namtumbo na Katibu tawala wa Mkoa wa Ruvuma Hasani Bendeyeko  Mrahu umefadhiliwa na Serekari ya Uingereza (DFID) chini ya usimamizi wa shirika la maendeleo la kimataifa la Marekani  [USAID]
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko anayeonekana katikati akizinduaMradi wa Huduma ya Uzazi wa Mpango kwa kukata utepe na kuzindua Gari aina ya Land cruser itakayotumika katika huduma hizo yenye thamani ya shilingi milioni 150 kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la MARIE STOPES Tanzania Zawadi Athanase na aliyeshika maiki kushoto ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Dr. Daniel Malekela.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko akikagua machapisho na shughuli zinazofanywa na shirika la MARIE STOPES Tanzania.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko hapo akipokea maelekezo kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika la MARIE STOPES Tanzania Zawadi Athanase juu ya utoaji huduma ya Uzazi wa Mpango.
 Hapo ni katika Mabanda ya Maonyesho Katibu Tawala akipokea maelezo kutoka kwa watoa huduma .
 Hapo watoa huduma wakifafanua kwa Katibu Tawala Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu Faida za kutumia vikinga mimba kama vipandikizi na vitanzi vinavyomsaidia mama kuweza kumudu kuhudumia familia kwa uhakika na kutimiza mahitaji, pia wameeleza hakuna madhara yanayotokana na matumizi ya kinga hizo isipokuwa ni maudhi madogo madogo ambayo hayaendelei kwa muda mrefu.
 Hapo Wahudumu wa Afya wa Wilaya ya Namtumbo wakifurahia kupokea huduma hiyo na kusema kupeleka Mpango huo wa huduma ya uzazi wa Mpango  wilaya ya Namtumbo ni ukombozi kwa wanawake wa wilaya hiyo kwa kuwa katika Mkoa wa Ruvuma wilaya zinazoongoza kwakuto fuata uzazi wa mpango
 katibu tawala Mkoa wa Ruvuma akifurahia kuhusu uzazi wa mpango, serekari hupata Changamoto watu wanapo zaa bila kufuata Uzazi wa Mpango
 Akina mama wawila ya Namtumbo ambao wamekumbwa na Mfumo dume kuzaa bila ridhaa yao sasa wanafurahia kupata elimu ya Uzazi wa Mpango
 Siyo rahisi kuwaona wanaume wa wilaya ya Namtumbo kupokea Elimu ya uzazi wa Mpango lakini kutokana na watu walio enda darasani wame weza kuwa shawishi wanaume wa Namtumbo hadi kupokea Elimu ya Uzazi wa Mpango
 Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Hassani Bendeyeko akiwahamasisha Wananchi wa Wilaya ya Namtumbo kushirikiana na Serekari kufuata Mpango wa Uzazi
 Ilikuweza kufikisha ujumbe wa matumizi Bora wa Vipandikizi vya Uzazi wa Mpango ina bidi elimu hiyo isambazwe na Vyombo vya Habari ,Kutoka kushoto ni Mwandishi wa Chaneli Ten Emanuel Msigwa na aliye Katikati ni Judith Lugoye kutoka Star Tv na aliye kulia ni Hamza Hamza kutoka TBC 1
 Mhamasishaji aliye bobea katika Elimu ya Uzazi wa Mpango kutoka Marie Stopes  James Mhina akisambaza vipeperushi vinavyo mpa nafasi mwanchi kujua zaidi kuhusu uzazi wa mpango
 Nirahisi kuhamasisha uzazi wa Mpango lakini kimila na Desturi ya Wandendeule kuwa na Watoto wengi na wake wengi kuna kupa na fasi ya kuteuliwa kuwa balozi, Kazi aliyo ifanya katibu Tawala Hassani Bendeyeko ni Kueeleza Madhara yanayo tokana na kuwa na watoto wengi kuna didimiza uchumi wa Familia, Wananchi wa Wilaya ya Namtumbo wamekubaliana na Uzazi wa Mpango


 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la Marie stopes Tanzania  Zawadi Athanase ambaye ni Mama aliye bobea katika utoaji wa Elimu ya Vipandikizi, Vitanzi ,Kondomu za Kike, Vijiti na Ushauri Nasaha  na Kutoa Neno la Mbele kuhusu Faida ya Uzazi wa Mpango kwa wanawake
 Mwonekano wa Banda la Marie Stopes lilivyo pendei wa Mpangoza ikiwa ni Dalili ya Wanchi wa Namtumbo kupokea kwa dhati Elimu ya Uzazi
Katibu Tawala Hasani Bendeyeko akiliwasha gari lililo tolewa katika Wilaya ya Namtumbo kwa ajili ya Matumizi ya Kuelimisha na Kutoa Huduma za Uzazi wa Mpango

No comments:

Post a Comment