Nimajonzi yaliyo tawala katika familia ya Mzee Matembo baada ya Kumpoteza Baba yao Mzazi Oddo Makita Matembo aliye fariki dunia Wiki hii katika Wilaya ya Mbinga kwa Ugonjwa wahindikizo la Damu.Marehemu Oddo Makita Matembo alizaliwa mwaka 1941 katika mji wa Mbambabay alibahatika kusoma hadi kumaliza Shule ya msingi alijiunga na masomo ya sekondari katika shule ya kigonsera alipata masomo ya Sheria nje na ndani ya nchi alipata shahada ya sheria ya kazi,amewahi kufanya kazi wilaya ya njombe wakati huo, na baadaye alihamia mkoa wa ruvuma kama Afisa wa Kazi alipo toka Songea alihamia Mkoa wa Lindi ambako alisitahafu na kuja kuishi Mbinga aliko malizia masha yake
Binadamu aliye zaliwa na Mwanamke siku zake za kuishi siyo nyingi Huchanua kama ua na kunyauka , Hapo Marehemu Oddo Makita Matembo akiwekwa Kaburini kwa Mapumuziko ya Milele Mungu alitoa na Mungu amechukua ,Jina la Bwana Lihimidiwe
Padri Kaswelo Makita Matembo akiendesha Maombi ya Kuomwombea Marehemu Oddo Makita Matembo katika Makaburi ya Mbinga Mjini aliye vaa jeketi kushoto ni mtoto mwake wakwanza Masiha Makita Matembo
Mtoto wa Mwisho Deogras Oddo Matembo akiweka Taji la Maua huku akitoa heshima za Mwisho kwa Marehemu baba yake Marehemu Oddo Makita Matembo
Mama Mkwe wa Masiha Matembo Mama Nditi akiweka Taji la Maua kwenye Kaburi la Mkwewe Marehehemu Oddo Makita Matembo
Wajukuu wa Marehemu Oddo Makita Matembo wakiweka Shada la Maua katika kaburi la Babu yao
Maombezi ya Mwisho kwa Marehemu Oddo Makita yakiliyo endeshwa na Padri Kaswelo Makita Matembo
No comments:
Post a Comment