Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Said Thabit Mwambungu ametekeza Nyavu za kuvulia Samaki katika wilaya ya Nyasa
zinye thamani ya shilingi milioni 87 ili kudhibiti uvuvi Haramu unao sababisha
kutoweka kwa samaki wadogo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
akiteketeza Nyavu hiozo amesema serekari haina ugomvi na wavuvi bali serekari
ina ugomvi na wavuvi haramu wanao tumia zana haramu kuteketeza viumbe visivyo
takiwa kuvuliwa
Pamoja na kutumia uvuvi haramu bado kuna matumizi mabovu ya Msaada unao tolewa na wahisani rangi ya Blue unayo iona ni Chandarua za Kuzuia Mbu lakini zina tumika kwa ajili ya Uvuvi,Mvuvi yuko tayari kuumwa na Mbu lakini bora apate Samaki
Katika Kuleta Uvuvi wenye
Tija Serikali katika Wilaya ya Nyasa imetenga Kiasi cha Shilingi 165,000,000/=
ili kununua Ingine mpya za Boti pamoja na Boti zake.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amesema macho madogo ya
nyavu zinapotumika unasababisha kuvua hata Samaki wadogo ambao wangeweza
kukufaa hapo baadaye, amewaomba Wavuvi kutumia Zana Bora katika Uvuvi ili
kulinda Viumbe ambavyo havistahili kuviangamiza.
Wananchi wa Mwambao wa ziwa Nyasa
wameiomba serekari iweze kuwainua ili waweze kuvua uvuvi wa kisasa waepukane na
uvuvi haramu ambao wao waliuzoea wakijua ni uvuvi halali
No comments:
Post a Comment