KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, September 12, 2012

MATESO MAUMIVU NA MAJONZI KWA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KIFO CHA DAUDI MWANGOSI

Ndugu Mtazamaji Napenda kuomba Radhi kwa kuonyesha picha ambayo ni simanzi kwa waandishi wote Duniani Hayo ndiyo masalio ya Mwili wa Daudi Mwangosi baada ya kulipukiwa kikatili akiwa kazini Nyololo Mkoani Iringa kinacho julikana ni Jaketi alilo vaa .Mungu aiweke Mahali Pema Roho ya Marehemu Daudi Mwangosi


JEE NINI TUFANYE BAADA YA KIFO CHA DAUDI MWANGOSO ?
Adamu Mzuza Nindi -Songea inayo songa mbele Ruvuma inayo Vuma



Waislamu wanasema sisi ni wmwenyezi Mungu na kwake tuta rejea ,(Ina lilahi waina Rajuni) Wakristo nao husema Bwana ametoa na bwana amechukua jina la bwana lihimidiwe.

Waandishi wa Habari Nchini kote Tanzania wanaendelea kulaani kifo cha Daudi Mwangosi kilicho tokea Mkoani Iringa Katika eneo la Nyororo wakati waharakati za Kampeni za CHADEMA za kufungua matawi pale wanapo fikia.



Waandishi wa Habari jambo ambalo nataka kuwaambia ni kuwa katika kifo kuna kitu kina itwa Kadiri na Kifo cha kawaida. Kadiri ni kifo ambacho Mungu hulazi mishwa kuchukua Roho yako baada ya Binadamu Mwenyewe kukiuka kanuni za Maisha

Kifo cha kawaida nikifo kile ambacho Mungu amepanga Taratibu za Maisha Ukiumwa uende Hosipitali na Madakitari na wauguzi wakishindwa kutoa matibabu basi Mungu hulazimika kurejesha Roho yake kwake.

Ninapo fikia tamko la Kadiri ni kifo ambacho kimelazimishwa ili Roho itoke kadiri ina tokana na kupuuza utashi ulio pewa na Mwenyezi Mungu ,Hakuna Mtu ambaye ahapewa kengere ya Hatari ukiipuuza Kengere hiyo ndipo kadiri inapo chukua nafasi yake.Na ninapo sema kifo cha kawaida ni kifo ambacho kina kuwa hakina masha uta sikia watu wakisema kazi ya Mungu haina Makosa.

Sasa tuangalie Mambo ya kufanya .Mwandishi ana Takuiwa kuwa kama Kunguru ,Kanuni ya Kunguru ni Kuhakikisha kila kilicho mbele yake ni Hatari na Niadui, Kwa mfano mwangalie Kunguru ukiwa mbele yake ukijikuna uka peleka Mkono Kichwani yeye anadai unamlenga muda huo huo huruka, hiyo nikanuni mzuri.

Au angalia Makarani wa Benki wamejiwekea kanununi wewe ukiwa mbele yao akili yao huwamtuma kuwa wewe ni Mwizi karani Huridhika baada ya wewe kuchukua fedha na kuondoka, Jambo Hilo huwa fanya wasiingie hasara pi hata kunguru huishi maisha marefu kuliko ndege yeyoyote yule.

Nivizuri kila Mwandishi akachukua Tahadhali za Kunguru, Mwandishi pia anapo Tembea anatakiwa awe na tahadhali kama Mahakama inavyo tumia mizani kutafuta haki ukiwa Mahakamani dalili ya kushindwa kesi ni mizani kukuelemea ukiona hivyo basi ujue wewe una chukua adhabu ya kifo ,kifungo au kupigwa faini.

Sasa ukiwa Mwandishi Nyosha mikono yako kuelekea Mashariki linako toka Jua ikiwa ni ishara ya kupata mwanga kwa jua linalo toka Mashariki, Mkono Mwingine elekeza Magharibi kunako zama jua ikiwa ni alama ya kuzama jua na kuingia kiza,

Baada ya hapo chukua Story yako weka juu ya mizani ukiona inaelea upande wa mashariki kwenye nuru unayo itegemea achana na Story hiyo ,ujue ni hasara kwako kwa Familia yako na Jamii kwa Ujumula, Ukiona Story yako ina uzito zaidi ya Roho yako basi hata mbio kimbia ili uonekana mjinga laki Familia ina kuwa imesalimika.

Sasa nisiwa choshe ndugu zangu Waandishi Michango ya Fedha Kulaani kitendo kilicho fanyika pamoja na Majuto havita weza kurudisha Upendo alio kuwa Daudi Mwangosi akiutoa kwa mke wake,watoto,Jamii kwa ujumula bali sisi sasa tujiepushe na Habari zinazo Hatarisha Maisha yetu, Waandishi tujue kuwa thamani yako iko mikononi mwa familiyako tu , Wewe kazi unayo ifanya ni kazi ya Mshumaa ukifa basi huo ndio mwisho wa Nuru ya Familia yako nani Kama Hayati Moringe ,au Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Rais Kened wa Marekani.


No comments:

Post a Comment