KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, December 28, 2016

VYOMBO VYA HABARI VYA SAIDIA KUWAKOMBOA WANANCHI KATIKA KUWADHULUMU WAJANE NA WAGANE KATIKA KUPATA HAKI ZAOMkuu wa Wilaya ya Makete Mkoani Njombe Veronica Kessi  amewaomba Wananchi ili kuepukana na dhuluma inayofanywa na Jamii kwa kupora Mali za wajane na wagane suluhu yake ni kushirikiana vitendo vinavyotoa Msaada wa Kisheria kwa Wananachi ambao hawana Elimu hiyo, Pamoja na kutoa habari zao za kudhulumiwa kwenye vyombo vya habari.

Mkuu wa Wilaya ya Makete ameyasema hayo baada ya Wagane na Wajane 80 kupata msaada wa kisheria na kuweza kurudishiwa mali walizoporwa.
Mkuu wa Wilaya ya Makete Veronica Kessi amesema wilaya ya Makete ina Kata 23 na katika Kata hizo kata 22 zina wasaidizi wa kisheria ambao wamekuwa msaada kwa wasiojua sheria wakishirikiana na vyombo vya habari  za kitaifa pamoja na vyombo vya wilaya ikiwemo  Green FM na Kituro FM

Mkuu wa wilaya ya Makete Veronica Kessi amesema anashukuru vyombo vya habari kwa kuwa wameweza kusaidiana na wananchi katika kupunguza migogoro mbalimbali inayowakabili wananchi kwa kutangaza  hatua zinazochukuliwa na Serikali baada ya kuona wajane na Wagane wakitaka kudhulumiwa mali zao.
Mkuu wa wilaya ya Makete amesema kuwa na wasaidizi wa kisheria kwa Kata 22 za wilaya ya Makete kumeleta mwanga kwa wasiojua sheria  kusaidiwa na kupata haki zao ikiwemo kurudishiwa mali zao.

Mkuu wa wilaya ya Makete Veronica Kessi amelipongeza Shirika lisilokuwa la kiserikali la PADI  likishirikiana na shirika la Msaada wa Kisheria SOPSE  kutoa Elimu kwa wasaidizi wa kisheria  na kuweza kufuzu vizuri katika utetezi huo, amesema wilaya itaendelea kusaidia Asasi zinazounga mkono shughuli za Maendeleo ikiwemo PADI

Mkurugenzi wa Shirika la PADI Iskaka Msigwa amesema wafadhili baada ya kuona PADI ilivyofanya vizuri katika mwaka mmoja uliopita wameongezewa ufadhili kwa miaka mi nne na kuongeza wigo wa utoaji huduma kutoka wilaya moja ya Makete hadi kufikia wilaya tano za Mkoa wa Njombe.

Mkurugenzi wa Shirika la PADI Iskaka Msigwa amesema vitendo vya kudhulumu wajane na wagane katika wilaya ya Makete vilikuwa vingi mno kiasi cha kuwaacha watoto waliofiwa na wazazi wote wawili kuishi kwa matatizo jambo lililosababisha ongezeko la watoto wanaoishi katika Mazingira hatarishi.
Shirika la PADI limeweza kufikisha Elimu kupitia vitengo vya kisheria na kuweza kusaidia watu 80 waliopatwa na majanga ya Mirathi, ndoa na masuala ya kumiliki Ardhi.

Mkurugenzi wa PADI ameomba pamoja na washauri wa kisheria wameweza kufanikiwa katika kazi hiyo lakini msaada wa vyombo vya habari kama inavyofanya Radio Free Africa , Green FM na Kitulo Fkujitolea kutangaza matukio yanayowapata Wagane na wajane kwa kutangaza bure, na vyombo vingine viige tabia hiyo.


Mkurugenzi  Mtendaji Halimashauri ya Makete Gregory Emanuel amesema katika kupata kituo hicho sasa suala la Maendeleo liko mbele kwani migogoro ya Ardhi sasa imepungua , kwa kiasi kikubwa sasa  wananchi wanashiriki kazi za Maendeleo. Migogoro inashughulikiwa na wasaidizi wa kisheria kwa njia ya upatanishi.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya ya Makete Felex Mbwiro  amesema kazi ya Afisa Maendeleo ni kuhakikisha hakuna Mwananchi anayekosa Maendeleo kwa ajili ya kunyanyaswa kwa kudhulumiwa mali zake, akiungwa mkono na Afisa Idara ya maji jinsi vitengo vya kisheria vinavyosaidia wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Makete Veronica Kessi amewaomba wananchi na Viongozi wa Serikali kutofumbia macho vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa wananchi kwa kudhulumiwa mali zao na familia za wajane na wagane baada ya mme au mke wa marehemu kufariki. Na kuwataka waache kudhulumu mali za familia ya marehemu aliyefariki badala yake wawe wasimamizi kuhakikisha hakuna anayeingia na kudhulumu mali hizo.


Saturday, December 24, 2016

MKUU WA WILAYA YA SONGEA POLOLET MGEMA AMEPIGA MARUFUKU WANANCHI KUFANYA SHUGHULI ZA KIBINADAMU KATIKA HIFADHI YA MILIMA YA MATOGORO


Mkuu wa Wilaya ya Songe amepiga marufuku kwa Wananchi kufanya shughuli za kibinadamu katika Eneo lililopimwa kwa ajili ya Hifadhi ya Milima ya Matogoro lenye Ukubwa wa Hekta 6755.


Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema  ameyasema hayo baada ya Wananchi wa Kijiji cha Kikunja kukataa kuweka Mipaka ya hifadhi ya Misitu kwa madai kuwa Hifadhi ikipimwa Wananchi wananyanyaswa na Maliasili kwa kupigwa na kukatazwa kusogea katika Mipaka hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema akikagua Hifadhi ya Milima ya Matogoro Kusini ametoa Agizo kwa Mtu yeyote atakayeonekana akifanya Shughuli za kibinadamu katika Hifadhi hiyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kupelekwa Mahakamani
 kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Songea ikiongozwa na mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Songea Mgema wakiw katika mazungumzo ya pamoja na viongozi wa kijiji cha kikunja na uongozi wa kata ya Matimila  pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu katika Kijiji cha Kikunja Songea Vijijini
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kikunja katikati Teodat Ansgar Kwanji akipokea Agizo toka kwa Mkuu wa Wilaya juu ya kusimamia ulinzi wa vyanzo vya maji katika hifadhi ya misitu kwenye eneo lake ambalo wananchi walizuia wakala wa misitu kuweka mipaka ya hifadhi hiyo kisheria
 Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kikunja Teodat Ansgar Kwanji amemuomba Mkuu wa wilaya

kuitisha mkutano wa hadhara kwa Wananchi ili kutoa Elimu juu ya Mipaka kwa kuwa Wananchi hawana Mihutasari inayoainisha uwepo wa Mipaka.
  Eneo la Hifadhi katika safu ya Milima ya Matogoro Magharibi
 Sehemu ya eneo la Msitu wa Matogoro ambalo ni chanzo kikubwa cha maji kwa wakazi wa Manispaa ya Songea
 Wananchi wa Kijiji cha Chikunja Kata ya Matimila Tarafa ya Muhukulu
 Wananchi wa Kata ya Kilagano waliokuwa wanafanya shughuli za Kilimo katika eneo la Hifadhi ya misitu
 Sehemu ya eneo la hifadhi Kata ya Kilagano lililoingiliwa na wakulima kufanya shughuli za Kilimo
 Afisa Mtendaji kata ya Matimila Emmanuel Njogopa akitoa maelezo mbele ya Mkuu wa Wilaya jitihada walizozichukua katika kusimamia eneo la hifadhi ya misitu.
 Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu wilaya ya Songea Manyisye Mpokigwa akiratibu sheria za uhifadhi na nini wananchi wanruhusiwa kukifanya eneo la Hifadhi amesema ni kosa kufanya shughuli za kilimo na kukata miti mibichi.
 Wananchi wa Vijiji vya Kihagala, Muungano Zomba na Kilagano wamesema eneo wanalolima walirithi kwa mababu toka zamani wameomba Serikali kuwafikiria kwa kuwa hawana maeneo mengine ya kulima wamesema wapo tayari kushirikiana na Serikali kwa kupanda miti na kuilinda.
 Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema katikati akibadilishana mawazo na viongozi wengine juu ya athari zinazoweza kujitokeza kutokana na wananchi kuingilia hifadhi ambazo ni vyanzo vya maji yanayotumiwa na wakaazi wa Wolaya ya Songea. Kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Songea Pendo Daniel
 Viongozi wa Kata ya Kilagano wakiratibu maelekezo toka kwa Mkuu wa wilaya ya Songea namna wanavyopaswa kusimamia sheria katika kuhifadhi misitu na vyanzo vya maji kwenye maeneo yao.

Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Wilaya ya Songea Manyisye Mpokigwa  ameainisha shuguli zinazopaswa kufanyika katika eneo la hifadhi ambazo haziathiri vyanzo vya maji na uharibifu wa Mazingira.


Eneo la Hifadhi ambalo halijapimwa lenye ukubwa wa Hekta 3208 ni miongoni mwa maeneo ya Vyanzo vya Maji ambavyo ni tegemeo kwa wakazi wa Manispaa ya Songea.