KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, August 16, 2014

MTOTO FATINA MSUYA ANAOMBA MSAADA WENU NDUGU MLIO ZALIWA NA MAMA MWENYE UTASHI


Ndugu zangu nimezoea kuwa letea habari za Maendeleo na changamoto zinzo husu upande wa serekari, Leo sipo hivyo naomba kabla hujaendelea  kusoma Tarifa hii kwanza anza kuomba kwa Mwenyezi Mungu kumwombea Mtoto Fatina Msuya mwenye umuri wa mwaka mmoja toka azaliwe
Masikini mtoto Fatina Msuya alizaliwa tarehe 24/2/2013 .Mtoto huyu anatia huruma amezaliwa bila kuwa na sehemu ya kutolea haja kubwa kwa sasa anajisaidia kwa kutumia  tumbo. Hapo awali alikuwa akitolea sehemu ya haja ndogo baada ya kufanyiwa upasuaji ndipo alipo kuwa akitolea haja kumbwa Tumboniaidi ambayo imekuwa na aza kubwa z.

Mama Paulina Nyoni anaomba msaada wa kuweza kutibiwa mtoto wake gharama za matibabu ni shilingi milioni mbili, Yeyote Mwenye msaada basi anaweza kutuma kwa Mpesa no 0767 710 113 au 0755 061 588, kwa tarifa zaidi piga kwa mkurugenzi wa Songea Habari 0755 731 234
Ndugu zangu mtoto anatia huruma fikiri kama wewe ndiye mwenye tatizo hilo unge likabili vipi unaona jinsi mtoto avyo tazama kwa huruma  ,chonde tumwombee mtoto Fatina Msuya afanikiwe kwenda kutibiwa

Masikini mtoto Fatina  Msuya hivi sasa akipata haja kubwa inaongozana na damu, Mama yake mzazi Paula Nyoni anaishi Hanga vijijini katika Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma

Tuesday, August 5, 2014

JAJI MFAWIDHI WA KANDA YA SONGEA APATA AJALI NAKUPATA MATIBABU HOSPITALI YA TUNDURU

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amesema Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Kanda ya Songea alikuwa akisafiri kikazi kutoka Songea kuelekea Tunduru akiwa kwenye Gari lenye Namba za Usajili J23 aina ya Toyota lundcruser lilipinduka baada ya Tayari la Mbele kupasuka.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea Mwanaisha Athumani anaendelea na matibabu katika  Hospitali ya Wilaya ya Tunduru baada ya Kupata Ajali Maeneo ya Matemanga Wilayani Tunduru Mkoa wa Ruvuma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Msikhela Mihayo akiwataja wengine waliokuwa kwenye Gari hiyo amesema ni Frank Frank Mwambali Msajili wa Mahakama Kuu ya Kanda ya Kanda ya Songea ambaye amepata michubuko, Askari Polisi W.P. Coplo 3712 Leocadia Mpambe wa jaji ambaye hakupata Majeraha yoyote na Dereva Kaoneka Martine  ambaye naye ametoka salama.

Saturday, August 2, 2014

MAMILIONI YA FEDHA YA TENGWA KWA AJILI YA WAZEE MKOANI RUVUMA


Wazee walioko mkoa wa Ruvuma wapatao 10,000 wanatarajia kunufaika na huduma za afya baada ya Halimashauri 5 za mkoa wa Ruvuma kutenga kiasi cha shilling milioni 100,501,000/=
Wajumbe Mbalimbali kutoka idara ya Ustawi wa Jamii wakiwakilisha tarifa katika Mkutano ulio andaliwa na PAD Shirika linalo hudumia wazee lilioko Mkoa wa Ruvuma wamekieleza kikao hicho juhudi zinazo fanywa ili kuwahudumia wazee na wategemezi wawazee.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Daniel Malekela akitoa agizo kwa waganga wa wilaya za Mkoa wa Ruvuma juu ya Kutumia Mifuko ya Fedha ili kuwa hudumia Wazee

Mkurugenzi Msingwa amesema swala lililo saidia kupunguza vitendp vya ukatili dhidi ya wazee ni baada ya kuunda Mabaraza ya wazee pamoja na kutoa Elimu kupitia tasisi za serekari na watu binafisi,Hivi sasa wazee wanatibiwa bila kunyanya paliwa

Mkurugenzi wa PAD[ Shirika linalo Hudumia Wazee Tanzani ] Issaca Msigwa amesema shirika la PAD limefanikiwa kupunguza vitendo vya ukatili upande wawazee ambapo hapo awali kila wakati wazee wenye macho mekundu au kuhisiwa kwa imani za ushirikina walikuwa wakiuwawa mfano mmoja wapo ni wazee wa kijiji cha magagula ambao walichomwa moto

 Wajumbe kutoka halimashari 5 za mkoa wa Ruvuma wakijadili kwa kina kuhusu swala la wazee na upataji huduma za Afya

Wajumbe walio hudhuria kikao kilicho jumusha halimashauri 5 za mkoa wa Ruvuma wameadhimia kuwa kila halimashauri nilazima iandae vitambulisho vya matibabu kwa wazee,pia kila Halimashauri iwe na idadi kamili ya wazee pamoja na wanao wategemea il kuepusha wanao timia mika 18 wasiwe tegemezi kwa wazee walkio pata msamaha wa matibabu

 Maratibu wa Wazee kutoka Manispaa ya Songea Ngelangela akisikiliza kwa makini swala la Manspaa ya Songea lilipo kuwa likiwakilshwa na kunukuru kero za wazee

Kikao hicho kili toa Changamoto zinazo wakabili wazee, Mashirika ya dini kukosha huduma kwa wazee kwa kuto tambua vitambulishowalivyo pewa,Wazee kukosa wawakilishi katika ngazi mbalimbali zinazo toa Maamuzi,Wazee kukosa Madisha Malumu kama ilivyo fanya Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza.Kikao kimeagiza kufanyike ziara ya mafunzo kwa kutembelea Magu,Mbalali, Simiyu

 Mfanyakazi waq PAD akiwa katika kikao kujua vipi wilaya zina fanya kazi maeneo mbambali ya Mkoa wa Ruvuma
Dakitari kutoka Halimashauri ya Wilaya akisikiliza kwa makini hoja zinazo tolewa zinazo husu Hosipitali za Mkoa wa Ruvuma
 Madhari ya Kituo cha PAD kilichopo Unangwa Manspaa ya Songea kilivyo jidhatiti katika maswala ya Mazingira
                                                  Wajumbe wa kikao wakiwa ukumbini
 Afisa usitawi wa Jamii kutoka Tunduru Blandina Sekela akijieleza jinsi wanavyo hudumia wazee Tunduru
AQfisa ustawi wa jamii Suzana Mkondaya akieleza jinsi wazee wa halimashauri ya wilaya Songea Vijijini wanavyo faidi huduma