KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, June 29, 2012

KAMANDA MAIKO KAMHANDA AVUNA ALICHO PANDA KUTOKA MKOANI RUVUMA

Mwenyekiti wa Kamati ya Kumwaga Kamanda Maiko Kamhanda akitoa shilingi milioni mbili kama Zawadi Kwake

wadau mbalimbali wakitoa zawadi mbalimbali kwa kamanda kamhanda wakati wa sherehe ya kumwaga katika ukumbi wa songea kilabu

Wadau mbalimbali akiwemo Cerencesia kapinga Mwandishi wa Habari wakienda kutoa zawadi kwa kamanda Mailo kamhanda

Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe Mwikoki akito vyeti kwa wana kamati walio Fanikisha sherehe

Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe Mwikoki akikabidhi Majina ya wana kamati kwa kamanda Mpya Deusdediti Nsimeki

KATIBA NDIYO MIRATHI HALALI KWA VIZAZI VIJAVYO - JAJI MFAWIDHI PETER CHOCHA

Kamanda wa police Maiko Kamhanda ambaye ana hamia Iringa akiwa na Kamanda Mpya Deusdeti Nsimeki katika Afula fupi iliyo fanyika ukumbi wa Songea Club


Police Wanawake Mkoa wa Ruvuma wakiongozwa na Inspekita Anna Tembo wakienda kutoa Mkono wa Heri wa kumwaga kamanda wao wa Zamani Maiko Kamhanda anaye hamia Iringa na Kumkaribisha kamanda mpya Deudedit Nsimeki


Meneja wa TTCL Mkoa wa Ruvuma Michael Chanachayo akiwa mmoja wawa shiriki katika kumwaga Kamhanda


Rose mary Chale akiwa katika sherehe za kumwaga Kamanda Maiko Kamhanda katika Ukumbi wa Songea Club

RCO Mpya akiwa na RTO Wakipongezana katika sherehe fupi ya kumkaribisha kamanda mpya Deusdediti Nsimeki

Mkuu wa kituo cha Police Mbinga akiwa kwenye ukumbi wa sherehe songea Club

Kamati ya sherehe wakiwa wamejipanga kwa ajili ya kumwaga kamanda wa Police Maiko Kamhanda

Viongozi wa Mkoa wa Ruvuma wakiimba wimbo wa Uzalendo katika kumkaribisha kamanda mpya Deusdediti Nsimeki na Kumwaga Maiko Kamhanda

Mkurugenzi wa kirahama akiwa na furaha katika sherehe za kukaribisha na kuaga makamanda wa Police

Mganga Marufu wa Jadi Frola Ndembo akiwa katika ukumbi wa Songea Club ili awa jue Viongozi wake wanao hama na wanao karibishwa Mkoa wa Ruvuma


Umati wawatu walio furika kuja kumwaga kamanda Kamhanda katika ukumbi wa Songea Club

Mkurugenzi wa Kiwanda cha kukoboa kahawa mzee Komba akiwa na Mkurugenzi wa shamba la kahawa lilioko liganga barabara iendayo Mbinga

kikosi cha Police kikiwa katika sherehe za kumwaga na kumkaribisha kamanda mpya

Mke wa Kamanda Mpya Mkoa wa Ruvuma akimpongeza Mume wake Kuhamia Mkoa wa Ruvuma

Sherehe ni kula bila kula siyo sherehe Hapo kamanda Maiko Kamhanda aki chukua chakula kilicho andaliwa kwa ajili yake katika kumwaga

Meja Chacha kutoka jeshi la wananchi akitoa mawaidha machache kuhusu utendaji wa Jeshi la Police Mkoani Ruvuma kuwa toka amefika hakuna ukorofi wowote ulio tokea kati ya JWTZ na POLICE

Tuesday, June 26, 2012

NYETI ZA WANAUME WENYE UMURI WA MIAKA AROBAINI ZA TAKIWA DAR ES SALAAM

MFANYAKAZI WA TGNP APATWA NA MKASA WA NGUVU

Liliani Liundi - Dar - es - salaam

Wajulisheni watoto, wapenzi, waume, wake, wajomba na marafiki zenu wachukuwe tahadhari, hii ni hatari.

Jamani soma kwa makini na chukua tahadhali, tuwe makini tunapochukua tax/kupanda daladala. nimeona ni vyema ni share na nyie hii msg iliyotumwa kwetu kutoka kwa mmoja wa mfanyakazi aliyepatwa na mkasa huu.

Leo nimeona ni vyema nika-share nanyi kisa hiki cha kutekwa mfanyakazi mwenzetu ambaye ni cashier siku ya jumatano jioni wiki iliyopita. Ni kama movie lakini ni ukweli, cashier wetu aliomba ruhusa siku hiyo ya tukio aende kwenye mkutano wa wasabato uliokuwa uliendelea viwanja vya biafra. Yeye pia ni msabato aliyeishika dini ya Sabato haswa, kwa hiyo aliondoka saa kumi kamili badala ya saa kumi na moja Baada ya dakika 40 tulianza kupokea sms zinazosema mwenye namba xxx amepata ajali na kufa papo hapo na kwa taarifa zaidi twende muhimbili hospital. Baada ya kutazama hiyo namba xxx ilikuwa ni ya cashier wetu.

Tulijaribu kuipiga iliita tu bila kupokelewa, na pia tulipiga namba iliyotutumia sms iliita bila majibu. Ilipofika saa kumi na moja tuliamua kuelekea muhimbili, ma baada ya kufika pale emergence tukaambiwa tuelekee chumba cha kuhifadhia maiti. Tulioneshwa mwili wa mtu aliyepata ajali lakini haukuwa wa cashier wetu, tukawatuma wenzetu waende hospitali zote lakini hapakuwa na taarifa zake Baada ya kuzunguka bila mafanikio tulitoa taarifa makao makuu ya usalama barabarani na baada ya dk kumi wakatwambia kuwa hakuna taarifa za ajali mbaya iliyotokea jioni hiyo.

Hatua iliyofuata ilikuwa ni kutoa taarifa polisi juu ya tulio hilo na ndipo waliposema kwa kuwa ni mtu mzima tusubiri hadi siku inayofuata. Wakati huo huo ndugu zake pamoja na wafanyakazi wenzetu walikuwa pamoja wakiendelea na jitihada za kumtafuta hadi saa sita usiku. Kilichokuwa kinatia wasiwasi zaidi ile namba iliendelea kutumia sms namba takribani zote zilizokuwa kwenye phonebook yake na ndugu zake hawakuwahi kuona ndugu yao akichelewa kiasi hicho.

Ilipotimu mida kama ya saa sita na nusu walisikia mtu akigonga mlango, alikuwa kaumizwa na amejaa matope, hakuwa na uwezo wa kuzungumza sana, ilibidi wampeleke kituo cha polisi na baada ya muda hospitali ya mwananyamala. Alipopata nguvu alianza kuwasimulia nduguze kilichotokea. Alipotoka ofisini alikwenda moja kwa moja kwenye kituo cha daladala cha karakana, pale kituoni walikuwa abiria wawili yaani yeye na mama mmoja.

Baada ya dk chache ilikuja coaster iliyoandikwa mbele Kawe na ilikuwa na tinted nyeusi, yule mama hakupanda sababu alikuwa anaelekea posta ila yeye alipanda. Ndani ya gari kulikuwa na watu watatu pamoja na dereva, wawili wakiwa wamekaa nyuma na mmoja akiwa amekaa karibu na driver. Gari hiyo hiyo ilikuwa ni mpya, mmoja wa abiria alimumba simu cashier apige simu moja kwa jamaa yake maana alidai kuwa simu yake illiishiwa charge na walikuwa wametoka mtwara kupeleka maiti, alimuuliza cashier umri wake na kama ameoa na anafanya kazi wapi, cashier akamjibu hajaoa na hana kazi pia ana miaka 32.

Walipofika Tazara hawakutaka kupakia abiria yoyote na walikuwa wote wamevaa miwani myeusi, na ndipo akaanza kuingiwa na mashaka akaomba ashuke, wao wakamwambia watapita biafra na hawana mpango wa kusanya kwa kuwa hata yeye walimpa lifti tu. Gari ilipokaribia taa za buguruni akainuka ili ashuke, jamaa wale wa nyuma wakamkalisha chini kwa nguvu, na sio kwenye viti yaani chini kabisa. Mmoja wao akafunga kitambaa cheusi kwenye macho na mikono ikafungwa kwa nyuma na mipira, baada ya muda akasikia kama wamempulizia perfume. Akihisi fahamu kumtoka polepole na neno lamwisho analokumbuka alisikia kuwa waelekee misitu ya Kibaha wakamalize kazi.

Kilichomwamsha ni kofi zito alilopigwa na kusukumwa hadi nje ya gari. Alianza kulia na kuwasihi wasimdhuru, wakaanza kumrusha kichurachura huku wakimkanyaga. Walikuwa wameshamfungua kitambaa machoni na waliacha gari umbali kama wa dk kumi na lilikuwa ni pori zito na giza, wao walivaa vitu usoni na walikuwa wamevaa gloves.

Wakamwekea simu yake mfukoni wakiwa wametoa simcard, walichomwambia wanachohitaji ni sehemu zake za siri na sio kitu kingine. Mmoja wao akaambiwa alete kisu kikali wanachokitumia, na walipompigia boss wao akawasisitiza nyeti zinazotakiwa lazma ziwe za mtu wa miaka 40 na kuendelea.

Mwenzao mmoja akasema cashier alisema alikuwa na miaka 32, baada ya kumkagua wakakuta card yake inaonyesha kazaliwa mwaka 1979. Kulingana na yeye asemavyo ndicho kilichomwokoa ila waliendelea kumkung'uta kwa hasira.

Wakamrudisha kwenye gari na baada ya mwendo wakampakia kwenye gari nyingine ndogo iliyokuwa na watu wawili ambao walimchukua na kumtelekeza maeneo ya sayansi. Hawakuchukua kitu hata kimoja wala kumwambia lolote,siku iliyofuata alipelekwa agakhan kwa uchunguzi zaidi na kwa sasa anaendelea vzr. Kwa ufupi ni hayo, ukweli mwenyezi Mungu atulinde na tumwombe pia abadilishe mioyo ya watu ambayo imekuwa migumu mno kwa ajili ya kupata vyeo na utajiri wa haraka

Monday, June 25, 2012

KAMANDA WA POLICE MKOA WA RUVUMA AAMURU MCHAWI ALIYE ANGUKA NA NDEGE YA KICHAWI ARUDISHWE KWAO MSUMBIJI

Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Kaizilege Nsimeki ametoa amri ya uchunguzi wa Mzee ambaye anasadikika alianguka na ndege ya kichawi iliyo anguka maeneo yaNamabengo wilaya ya Namtumbo ikiwa na abiria 12 ,Baada ya ndege hiyo kuanguka mzee aliye chini alizirai na wenzie walidhani amefariki walimwacha hapohapo.

Mzee aliye anguka katika ndege ya kichawi akingoja kurudishwa nchi jirani ya Msumbiji

Mganga wa Jadi Frolla Ndembo akiwa katika ofisi ya RPC Mkoa wa Ruvuma .Binti Ndembo ambaye amemfadhili mzee aliye anguka na ndege ya kichawi akitokea Maputo Msumbiji akitoa tarifa kwa kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma amsaidie kumrudisha mzee huyo kwao Msumbiji

Sunday, June 24, 2012

BINTI HUYU HAPA CHINI ANA TAFUTWA NA WAZAZI WAKE SONGEA

Binti Glolia Mligo ni Mwanafunzi wa kidato cha pili ana soma shule ya secondary Swila Mkoani Mbeya ,Alikuja likizo kwa wazazi wake ambao wanaishi songea. Binti Huyu ametoweka toka siku ya Ijumaa 15/06/2012 mpaka leo haja onekana yeyote atakaye mwona apige simu kwa mawasiliano kwa nomba zifuatazo 0767 668 400, 0714 668 400, 0755 731 234.au unaweza kutoa tarifa police

Hapo Glolia Mligo anaonekana akiwa amepiga picha ya kukata hiyo yote nikukupa mtazamaji ili umwone vema binti huyo wazazi wake wana hangaika wana shindwa hata kula

Glolia Mligo unavyo onekana kwenye picha unaonekana ni mtu mwenye busara, hebu nikuambie dawa ya maudhi nikuya puuzi ,endapo wazazi wame kuuzi ujue ndio maana wakaitwa wazazi kwalile unaloliona wewe kuwa ni zuri wenzio wamepitia hilo ndiyo maana wanatoa somo.Glolia wewe ni mkristo na bibilia ina sema Hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu mhubiri sura ya 7 Hebu shindana na shetani rudi kwa wazazi wako.yeyote aliye karibu na Glolia afikishe ujumbe huu.

Wednesday, June 20, 2012

MUNGU AKIKUPA MSHUKURU NDIVYO ASEMAVYO ADAMU NINDI

Ndugu Angelimo Chale akimtakia kila la heri ndugu Adamu Nindi na kumusia kuwa taifa linawategemea waandishi wa Habari kuwa na Usafiri wa vyombo vya moto una hitaji sana umakini



MUNGU NI MKUBWA. MUNGU NDIYE MWENYE HERI MUNGU HUMPA AMUTAKAYE NA KUMNYIMA AMTAKAYE JINA LA BWANA LITUKUZWE.


Mara zite Mungu amepanga kuwapa pepo wale ambao wamefanya kazi kwa ajiliyake. kwa wasitani mimi ninaye itwa Adamu Mzuza Nindi nimefanya kazi za Mungu kwa Miaka 17 . Chakula nilicho kuwa na kula wakati huo ilikuwa ni Kipange cha Mkate mmoja kiitwacho Sinkonzi pamoja na Robo lita ya Maziwa ya Mgando kwa siku.

Kipindi hicho nilichaguliwa kwenda kuhubili uislaamu katika Nchi ya Malawi na Msumbiji nime fanya kazi hiyo kuanzia mpakani Nkata bay Malawi hadi Mangochi mpaka wa Msumbiji na Malawi, nilibahatika kufungua Misikiti nne pamoja na kuweza kuwa silimisha machifu 3.

Baada ya Kumaliza kuhubili Nchi ya malawi nilingia Msumbiji ambako nilianza mahubili Kobwe Nchini Msumbiji hadi Mwambao wote wa Ziwa Nyasa muda huo wote nikiponea kipande kimoja cha mkate kwa siku . kwa mda wa Miaka 17 nimefanya kazi ya Mungu ni kiwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Mkoa wa Ruvuma lakini hata hivyo sikuacha kazi ya uandishi wa Habari.

Ninalo taka kusema ni kuwa ukimkumbuka mwenyezi Mungu hakutupi mkono katika maisha yako kumbuka sana walemavu,masikini wa Kawaida ,Acha kabisa Majivuno mheshimu kila mmoja unaye Mwona mbele yako.

Sasa kwa mapenzi ya Mungu nina Nyumba na Gari Dogo la Kutembelea hiyo ndiyo dawa ya Mungu kukukumbuka nawe usiwe kama hukuzaliwa.

kitu kingine cha Mhimu ni kuheshimu wanawake wote unao waona mbele yako hawo ndiwo wanao mwakilisha mama yako Mzazi, Ukimdharau Mwanamke ni sawa na kumdharau Mama yako Mzazi.

MWANDISHI MKONGWE ATOA USIA SIKU YA KUFA KWAKE



· Abubakar Karsan
Furaha ya kufa bila makuu ni kuzikwa bila sifa na utukufu uliopindukia ubinadamu.Furaha ya kuzikwa kwenye kaburi lisilokuwa na ufahari kiasi ambacho miaka ikipita utakumbukwa kwenye nyoyo ya watu na sio kwenye miundo mbinu ya kifahari,


kaburi ambalo dahari na dahari litaonekana na jina lako,Mungu nijaalie nisizikwe hivo,nizikwe kwa kufukiwa udongo na wala kaburi langu lisiandikwe chochote.


Mungu nijalie niache sifa kwenye mioyo ya watu,sifa zitakazodumu milele,watu ntakaowaacha hawatanitafuta kwenye makaburi bali katika mapindo ya historia ya matendo makuu ya binadamu
·
Abubakar Karsan
Asante Mungu kwa uhai ulionipa kwa miaka hii 51,nimeitumikia hivi:miaka 8 Mwanza Press Club,

miaka 7 Media Council of Tanzania,miaka

12 Mwanza Non Governmental Organization,miaka

3 Non State Actors Support Programme,UTPC naitumikia kwa mwaka wa 7 sasa.Miaka hiyo yote inaingiliana.Kwa miaka 30 iliyobaki nimeweka malengo yafuatayo:


1.Kuijenga UTPC na klabu yake kuwa asasi bora kabisa Duniani

2.Kuchangia kukuza uwezo wa kitaaluma na kipato kwa waandishi wa habari Tanzania

3.Kuwawezesha watoto wangu na mke wangu kuishi maisha bora yenye uhakika

4.Kufa na kuzikwa bila madoido,isirafu au kutukuzwa.MUNGU wangu nijaalie nitimize hayo

Monday, June 18, 2012

WATALAMU KUTOKA CHUO CHA MAENDELEO MLALE SONGEA VIJIJINI


Watalamu kutoka chuo cha Maendeleo Mlale wakiwakatika Ofisi za Radio Free Africa Wakifanya Utafiti wa Kujua Zaidi matatizo ya jamii Kutoka kulia ni Yusta Nduguru, Penina Pasco, Joice Kandosa

Sunday, June 17, 2012

KAMANDA WA POLICE MKOA WA RUVUMA ATIMIZA AZIMA YAKE

Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Desdedit Nsimeki akisalimiana na Mwenyekiti wa Police wanawake Anna Tembo
Kamanda wa Police akitoa mchango kwa ajili ya Jengo la Police Wanawake anaye pokea ni Mwenyekiti wa Police wanawake Anna Tembo


Kamati ya Ujenzi ya Jengo la Police Wanawake wakikagua jengo la Police Wanawake aliye Vaa shati la Miraba ni Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Desdedit Nsemike

Friday, June 15, 2012

MAMA HUYU HAPA CHINI AMETELEKEZA WATOTO 6 NA KUIBA SHILINGI MILIONI 3 WATOTO WANA HANGAIKA

Mama huyo hapo juu ana julikana kwa jina la Mesha joseph ambaye ametelekeza watoto walio hapo chini na kuchukua fedha tasilimu kiasi cha shilingi milioni 3 ambazo walijiwekea kwa ajili kuwa somesha watoto. mama huyo amefunguliwa jalada MAT/RB/59/2012 yeyote atakaye mwona atoe tarifa kituo chochote cha POLICE kilichopo karibuMasikini watoto unao waona hapo juu wametelekezwa na mama yao ambaye alikuwa akiishi matarawe katika Manspaa ya Songea, watoto hao wanasikitika mama yao mzazi hapo juu kutoka na kuchukua shilingi milioni 3 ambazo baba yao aliwawekea kwa ajili ya masomo wamemwomba mama yao arudi kwani maisha wanayo ishi simazuri, mpaka mtoto mdogo aliye katikati ana diriki kusema kwa nini mama yao aliwazaa ?

DAWA HIZI ZIME FIKAJE MIKONONI MWA MTUHUMIWA

AKAMATWA AKIWA NA DAWA ZA BINADAMU MALI YA SEREKARIMPWAPWA

Na Noel Stephen Mpwapwa

Jeshi la Polisi Wilayani Mpwapwa Linamshikilia mfanya biashara mmojawa kijiji cha Ng’hambi Bwana Jeremia mhogo kwa tuhuma za kukamatwana dawa za kutibu binadamu na baadhi ya dawa hizo zikiwa na nemboya MSD kinyume na sheria.

MKUU wa polisi wilayani mpwapwa Bwana JEREMIA SHILA ametibitishakutokea kwa tukio hilo na amesema mtuhumiwa bado anashikiliwa napolisi lakini kwa sasa yuko nje kwa dhamana .

JESHI LA POLICE MKOANI RUVUMA LA KAMATA BUNDUKI 16 ZILIZO KUWA ZIKITUMIKA NA WAHALIFU

As inspekita Jumanne akimwonyesha RPC Mkoa wa Ruvuma Deusdit Kaizilege Nsimeki bunduki zilizo kamatwa wilaya mbalimbali katika mkoa wa Ruvuma

Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Kaizilege Nsimeki akikagua Bunduki Zilizo kamatwa katika msako mkali wa kusaka Bunduki zinazo Fanya uhalifu mkoani Ruvuma

OCD Wa Wilaya ya Namtumbo akitoa maelezo jinsi alivyo weza kufanikiwa kukamata Bunduki katika Wilaya yake ya Namtumbo. Aidha kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma ametangaza zawadi ya shilingi laki tano kwa yeyote atakaye weza kufanikisha upakanaji wa Bunduki aina ya SMG

Wednesday, June 13, 2012

KATA SABA ZA WILAYA YA MPWAPWA ZA KABILIWA NA UHABA WA CHAKULA

NA NOEL STEPHEN MPWAPWA ,

JUMLA YA KATA SABA na VIJIJI VITATU vy a wilaya ya mpwapwa mkoaniDodoma vinakabiliwa na uhaba wa chakula kwa msimu huu wa chakula wamwaka 2011/2012.

Kauli hiyo imetolewa na MOHAMED LONGOI afisa mazo wa wilaya alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jana ofisi kwake kwa lengo lakutoa tadhimini ya chakula kwa mwaka 2011/2012 wilayani Hapo.

alisema kuwa kwa wilaya ya mpwapwa ilikuwa na mahitaji yaMazao ya chakula Tani 73,662 na wameweza kuvuna tani 74,254 ambazoni zaidi ya mahitaji ya chakula wilayani hapo .

Pia alisema kuwa mbali ya kuwa na zaidi tani 592 lakini alidai kuwakuna kata saba ambazo hukabiliwa na uhaba wa chakula na kata hizoalisema kuwa ni CHIPOGORO,MTERA,IWONDO,MIMA NA GHAMBI.Kata zingine ni RUDI NA GULWE na vijiji vya Idodoma,Kinusi, naKIJIJI Cha kiegea kata ya ghambi.

Alisema kuwa sababu za kata hizo kuwa na upungufu wa mazao ya chakulani kutokana na hali kijografia iliyopo ktika maeneo yao, ya katahizo na kingine alisema kuwa ni wanajamii wengi kung,ang,ania kulima mazo yasiyoweza kusatahimili ukame

Monday, June 11, 2012

WANAWAKE WA KATA YA TANGA SONGEA MANSPAA WADAI KUNYIMWA TENDO LA NDOA NI UNYANYASAJI KIJINSIA

Meya wa Manspaa ya Songea Chares Mhagama akitoa ufafanuzi kuhusu mfuko wa Jimbo ambao wananchi kata ya Tanga walidai hawajui kazi yake.

Wandishi wa Habari wakiwa na Meja Nyumayo ambaye alikuwa akipeana mawazo baada ya kuja Songea kwa Likizo fupi kujua hali ya Nyumbani Kutoka Kulia ni Insp Anna Tembo anaye fuatia ni Dereva Wawaandishi Chichi Chichi, watatu kutoka Kulia ni Meja Nyumayo Wapili kutoka kushoto ni Mwandishi Adamu Nindi wakwanza kushoto ni Juma Nyumayo

Wananchi waliokuwa katika Mdahalo wa Usawa wa kijinsia ulio fadhiliwa na The foundation

Katibu wa Mbunge wa Songea Mjini Andrew Chatwanga akiwa kwenye mdahalo ulio husisha wananchi wa kata ya Tanga kujadili maswala ya kuweze kuleta maendeleo kwa wanawake

Wanawake walio Hudhulia katika Mdahalo wa usawa wa kijinsia mdahalo ulio fanyika kata ya Tanga Mansipaa ya Songea, Wanawake wamedai kunyanyaswa kijinsia kwa kunyimwa tendo la ndoa ,Pia wamedai kuwa wanawake walio zaidi ya miaka 50 kulazimishwa tendo la Ndoa wakati wao hawako tayari kufanya tendo hilo kutokana na kutokwa na fikira za kufanya tendo hilo wameomba msaada wa kisheria.


Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika mdahalo wawazi kuhusu usawa wa kijinsia ulioendeshwa na Asasi ya SONNGO


Washiriki wa Mdahalo wawazi katika kata ya Tanga manspaa ya Songea wakiwa makini kumsikiliza Insp Anna Tembo alipo kuwa akitoa Mada kuhusu sheria zinavyo walinda wanawake na wanaume .

Saturday, June 9, 2012

UFUGAJI WAKUKU WAWAKOMBOA WANAWAKE SONGEA

Manspaa ya Songea ina wafugaji 150 ambao wana kuku wa mayai na kuku wa nyama wapatao 100,000

Makamu meya wa Manspaa ya Songea Mariamu Didhumba akifungua semina ya Ufugaji wa kuku Manspaa ya Songea wapatao 100 ili kupata mafundisho sahihi ya ufugaji wa kuku


Wasiriki wa semina ya ufugaji wa kuku wakisikiliza kwa makini kuhusu ufugaji bora

Watalamu wa Kilimo na Mifugo wakipeana mawazo wakiwa inje ya ukumbi wa manspaa ya songea

Dr.Nkoma akimkaribisha mgeni Rasimi katika semina ya ufugaji wa kuku wa nyama na Mayai

Washiriki kutoka kata 24 za Manspaa ya Songea wakisikiliza jinsi ya ufugaji bora na jinsi ya kuepukana na Magonjwa yanayo kabili kuku

Wanawake wakiwezeshwa wanaweza ndiyo kauli iliyo kisiri katika semina ya ufugaji wa kuku

Mwanamke ni kujiamini akijiamini anaweza kufanya kila kitu walidai wanawake hawa

Watalamu wanao leta dawa za kuku wametakiwa kuleta dawa bora badala ya kuleta dawa ambazo zina wapa hasara wafugaji.