KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, August 24, 2016

NAIBU WAZIRI WA ELIMU SAYANSI TEKNOLOJIA NA MAFUNZO YA UFUNDI MHANDISI STELLA MANYANYA ASIKITISHWA NA KIWANGO CHA ELIMU WILAYA YA NYASA. ASEMA NI AIBU NYUMBANI KWA NAIBU WAZIRI KUTOFANYA VIZURI AAGIZA KUONGEZA UFANISI KATIKA KUINUA ELIMU WILAYANI HUMO:

 Naibu Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na mafunzo ya Ufundi akiwa ziarani wilayani Nyasa alihudhuria Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Nyasa ambao ulisimiwa na Viongozi wa CCM Mkoa wa Ruvuma na kujadili changamoto zinazokikabili chama hicho.

 Naibu Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhandisi Stella Manyanya akiwa katika mkutano huo amewashauri viongozi wa CCM Kata kufungua akaunti za chama kwenye maeneo yao ili fedha yoyote itakayoingia ipitie Benki na matumizi yatoke benki hii ni katika kupambana na matuizi mabaya ya fedha za chama.
 Pamoja na kushiriki kikao cha Halashauri kuu ya CCM wilaya Mhandisi Manyanya amewataka wazazi kushirikiana na Serikali katika kuinua kiwango cha Elimu kwa Watoto kwa kuhakikisha watoto wanakwenda shule na kuwaboreshea mahitaji yao ya msingi ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa chakula cha mchana mashuleni, Amesema ni fedhea kubwa kuona Jimbo lake linakuwa na kiwango cha chini cha Elimu.
 Katika Kikao hicho cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Nyasa Makatibu wa Kata wameomba kufikiriwa kuongezwa posho wanazolipwa kwa mwezi ili iwasaidie kutekeleza majukumu kwa wakati pale wanapohitajika kupeleka taarifa CCM Wilaya kwa kuwa Jiografia ya Wilaya ya nyasa baadhi ya kata ziko mbali na makao makuu ya chama zaidi ya km 100 kwa posho ya sh 10,000 kwa mwezi ni kiasi kidogo.
 Wamesema inapotokea kuna taarifa zinatakiwa kuziwasilisha Ofisi za chama wilaya Makatibu wanaanza kufikiria jinsi ya kuzifikisha kwa kuwa wanaitaji nauli zaidi ya sh 20,000 kwa kila safari na  ni lazima watumie siku mbili jambo ambalo huwapelekea wakati mwingine kutuma taarifa hizo kwa njia ya simu.
 Aidha Makatibu na wenyeviti wa Kata Vijiji na Matawi wametakiwa kuisaidia Serikali katika utekelezaji wa Ilani ya chama na siyo viongozi kuanza kulalamika.
 Mhandisi Stella Martini Manyanya anaona fahari kuthamini tamaduni za asili ikiwa ni pamoja na chakula cha asili, Pichani ni Naibu Waziri wa Elimu akichukua chakula cha Ugali wa Muhogo kwa dagaa Nyasa kilichoandaliwa katika Hoteli ya kiasili ya Bio Camp iliyopo wilayani Nyasa, kushoto ni waandishi wa Habari wa Chanel Ten na TBC wakiwa wameambatana na Naibu waziri wa Elimu.
Hiyo ni Ngoma ya Asili ya wakazi wa Mwambao wa Ziwa Nyasa almaarufu Kioda  ambayo huchezwa wakati wa mavuno au katika sherehe za kuoana ama katika kumkaribisha mgeni. Hapo walikuwa wakitumbujiza baada ya kutembelewa na Mbunge wao Naibu Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhandisi Stella Manyanya na kumpa ujumbe wa serikali kupitia uimbaji.
Wananchi wa wilaya ya Nyasa wanakabiliwa na changamoto ya kukosa zana bora za uvuvi jambo ambalo hupelekea usalama mdogo wanapokuwa Ziwani endapo hali ya ziwa inabadilika kuwa na mawimbi makali.
Naibu waziri wa Elimu Mhandisi Stella Manyanya akishiriki na wananchi wake katika kuicheza ngoma ya kioda ambayo ni sehemu ya Utamaduni wa Wakazi wa Mwambao wa Ziwa Nyasa . Waimbaji walikuwa wakiiomba Serikali kusimamia Amani Bungeni .
Mhandisi Stella Martin Manyanya aemesema wazazi wasipoweka bidii katika kuelimisha watoto hatutaweza kupata wahandisi katika Nchi yetu pia itakuwa vigumu kuelekea katika uchumi wa kati wa viwanda pasipokusomesha vijana wetu na kuwahamasisha wapende sayansi ili kuongeza wataalamu nchini.
Akioongea kuhusu usalama wa majini kwa wananchi wa wilaya ya Nyasa Mhandisi Manyanya amesema anatamani kuona ulinzi wa watu wanaotumia ziwa Nyasa kusafiri au shughuli za uvuvi ukiimarishwa kwa kutumia njia wanayoitumia wataalamu wa Umeme katika kukabiliana na hitilafu zinapojitokeza kwa kutega baadhi ya maeneo na wataalamu kufuatilia watu wanaopanda kwenye mitambo kwa kutumia mawasilikano ambayo hutegwa ktk vituo mbalimbali ili kufuatilia usalama wa watumiaji wa umeme na mafundi.
Mhandisi Stella Manyanya anasema ni vema tuwe na tabia ya kuvithamini vya kwetu, ameomba wazawa wa Mwambao wa Ziwa Nyasa kuwekeza katika rasilimali zetu kuliko za kigeni ziko fursa nyingi zilizopo wilaya ya Nyasa ambazo maeneo mengine hazipatikani vikitumika vizuri vitasaidia katika kuinua uchumi wa wananchi wa wilaya ya Nyasa na Tanzania kwa ujumla .
Mtanzania anayeishi Ujerumani mzaliwa wa wilaya ya Nyasa ambaye ameamua kuendeleza nyumbani Mr Chengula amewaasa wananchi wa Tanzania kufanya shughuli za Maendeleo kwa kutumia fursa zilizopo Nchini na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika jitihada za kuhakikisha Tanzania inakuwa Nchi yenye uchumi wa kati kwa kufanya kazi. Pia amesema Watanzania wanaoishi nje ya Tanzania wasisahau kuthamini nyumbani kama ambavyo yeye anafanya ingawa amekuwa Ujerumani kwa miaka 25 lakini anaona fahari kuwekeza nyumbani.hamasisha maendeleo kupitia sera yake ya Hapa Kazi tu amesema wenzetu wanathamini kufanya kazi.
Mhandisi Stella Manyanya akiwa katika ufukwe wa Ziwa Nyasa  na Mwenyeji wake Mr Chengula ambaye anaishi Ujerumani. Mhandisi Manyanya amemuomba anapokuwa Ujerumani kutangaza fursa zinazopatikana mwambao wa Ziwa Nyasa na Tanzania kwa ujumla,  pia kukitangaza Kiswahili ili kiwe no moja kuliko kuenzi lugha za kigeni na kusahau nyumbani.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Odo Mwisho amewataka wanachaa wa Chaa cha mapinduzi kuzingatia Matumizi ya Mali za Chama. Amesema kwa yeyote atakayebainika kuharibu mali za chama ama kuzitumia kwa kujinufaisha chama hakitasita kumchukulia hatua.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na mafunzo ya Ufundi Mhandisi Stella Manyanya akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Odo Mwisho na Mwandishi wa Chanel Ten Marietha Msembele juu ya kuimarisha Jumuia za Chama katika wilaya ya Nyasa  ili ziweze kujitegemea.
Mhandisi Manyanya amesema sasa ni wakati wa kuhakikisha kila kata inakuwa na mradi wa Chama ambao utasimamiwa ipasavyo  na kuwezesha chama kujiendesha badala ya kusubiri wakati wa chaguzi.
Mwandishi wa habari Marietha Msembele akiongea na Naibu waziri wa Elimu kukuhu  Mikakati iliyopo katika kuendeleza Elimu wilaya ya Nyasa.  Naibu Waziri amesema kwa sasa wanaikuza Shule ya Mbamba Bay High School ili iwe shule ya Mfano nyumbani kwa Naibu waziri wa Elimu ambayo inaboreshewa miundo mbinu na vitabu vya kutosha na mazingira bora ya kujisomea wakati jitihada za kuendeleza shule zingine zikiendelea.

Wilaya ya Nyasa yenye vijiji 84 ina fursa nyingi ambazo zinahitaji uwekezaji
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba ameomba ushirikiano kwa wananchi wa Wilaya ya Nyasa katika kujiletea Maendeleo.


Fursa zilizopo wilaya ya Nyasa ni pamoja na ufukwe nzuri kaa inavyoonekana pichani.
Hizo ni nyumba zinazopatikana katika Hoteli ya Bio Camp ambayo ni ya asili iliyopo wilaya ya Nyasa koani Ruvuma. Ni ufukweni mwa Ziwa Nyasa pana upepo mwanana na hali nzuri ya hewa ukihitaji kutembelea mazingira ya ziwani usafiri wa Boti unapatikana pia vinywaji na chakula cha asili vinapatikana BIO CAMP.

Madiwani na Viongozi wa CCM Kata za Wilaya ya Nyasa wakiwa katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Nyasa.

Saturday, August 20, 2016

MATATIZO YA MIZANI WILAYA YA TUNDURU YAWA CHANGAMOTO KWA WAKULIMA


WAKULIMA MKOA WA RUVUMA WAMESHAURIWA NA WAKALA WA  VIPIMO KUTUMIA MIZANI ZILIZO KAGULIWA NA SEREKALI ILI KUEPUKA CHANGA MOTO ZA KUUIBIWA MAZAO YAO


Meneja wa vipimo mkoa wa Ruvuma Hasani  Halletu amewaomba wakulima pale wanapo ona mfanya bishara au mtu yeyote ana tumia mzani usio kaguliwa watoe tarifa mara moja


Watalalamu hao wa vipimo wamesema njia ya kugundua kama mizani ni salama ni kuangalia tarehe ya kukaGuliwa na kuona kama mizani ina cheza vizuri alama za kukaguliwa ni Mhuri wa mwaka ilipo kaguliwa na nembo ya serekari inayo gongwa.

Wakulima wa wilaya ya Tunuru wametakiwa kuwa makini wanapo kwenda kuuza mazao yao kwa kuhakikisha Mizani ziko salama hazina ubovu  Kauli hiyo imetolewa na mawakala wa vipimo kutoka Dar es alaam wa kishirikiaani ni salamana na mawakala wa vipimo kutoka mkoa wa Ruvuma walipo kuwa wakikagua mizani zinazo tumika kupimia mazao ya wakulima na kubaini kati ya mizani 5 zilizo pimwa tatu ni mbovu

Nao wakuliwa wawilaya ya Tunduru wakionyesha elimu ilivyo waingia walieleza jinsi somo la mizani lilivyo waingia  kwa kufafanua kama ifuatavyo

Wakulima wakionyesha jinsi ya kuweza kutumia Mizani na pia kujua kama wanaweza kuuza mazao yao kwenye mizani mbovu