KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, July 25, 2016

WAANDISHI 33 KATI YA WAANDISHI 600 WALIO OMBA RUZUKU VIJIJINI KATI YAO 33 WAPATA MAFUNZO DSM

 Mkugenzi wa TMF Erenest Sungura akiwaasa waandishi wa habari kuacha  tabia ya kulazimisha kupata Ruzuku kutoka TMF. Ruruku hutolewa kwa kufuata vigezo,Mkurugenzi amesema kwa hivi sasa ana fanya mipango ya kuwaita wale waandishi wanao lazimisha Ruzuku kwa njia ya kujuana  swala hilo halipo
 Waandishi wa habari wanawake walio chaguliwa kupata Ruzuku ya kuandika habari za vijijini wakiwa makini kusikiliza Hotuba ya mkurugenzi Erenest Sungura na kuandika kumbukumbu katika Laptop zao
 Mkurugenzi wa TMF akisalimiana na Adamu Nindi katika ukumbi wa TGNP wakati wa semina ya siku nne
 Waandishi Wahabari kutoka mikoa 16 ya Tanzania wao shiriki mafunzo ya TMF kati ya waandishi 600 walio omba mafunzo ya kupata Ruzuku ya Vijijini ambayo ni shilingi mioni 4 fedha ya kitanzania
 Waandishi wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi wa TMF Ndugu Erenest Sungura akiwaasa waandishi kutumia Ruzuku waliyo pata watumie kwa manufaa ya kutatua kero zinazo wakabili wananchi katika nyanda mbalimbali
 waandishi wakiwa katika jengo la TGNP Mabibo wakipata vidongo vya kuwezesha kuandika habari ambazo zita toa matokea mazuri kwa wananchi
 Mmoja wawaandishi kutoka Mkoa wa RuvumaAdam Mzuza Nindi ambaye ana shiriki mafunzo ya TMF kuhusiana na Ruzuku ya Vijijini akishiriki mafunzo hayo Katika Ukumbi wa TGNP Dae - es Salaam
 Kati ya wandishi Thelathini walio teuliwa wanawake ni kumi na tatu kama unavyo waona katika ukumbi wa TGNP. Mkurugenzi  wa TMF Erenest Sungura amesema Uteuzi waandishi 600 walio omba Ruzuku ya Kuandika Habari za Vijijini umefuata wazo zuri la Mtu na siyo Rushwa

Waongozaji katika Mchakato waaandishi wahabari watakao andika habari za vijijni wakiwa katika Semina ya

Saturday, July 23, 2016

DR. BINILITH SATANO MAHENGE AKIWA KATIKA WILAYA ZA NYASA, MBINGA NA SONGEA VIJIJINI ALIKUTANA NA CHANGAMOTO KADHAA

Mkuu wa Mkoa wa ruvuma Dr Binilith Satano Mahenge akiwasili katika wilaya ya Nyasa na kusalimiana na Viongozi wa wilaya.
Mkuu wa Mkoa akielekea kwenye ghala la hifadhi ya Chakula wilayani Nyasa.
Mkuu wa wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba akitoa maelezo kwa mkuu wa Mkoa wa ruvuma dr Binilith Satano Mahenge.

katika ziara hiyo pia  alibaini kuharibika kwa mahindi tani 90 zenye thamani ya shilingi  45,000.000/=  wilaya ya nyasa Mahindi ambayo yalitakiwa kusambazwa kwa watu waliopata maafa ya mafuriko kutokana na kufurika kwa Mto Ruhuhu Disemba mwaka 2015 na kusomba mazao ya wananchi wa wilaya ya Nyasa.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Satano Mahenge akikagua miradi ya maji wilaya ya Mbinga,
sekita pekee ya ya utafiti wa kahawa iliyoko wilayani Mbinga ime kuwa kiungo kizuri kwa wakulima wa kahawa kwa kuwapa mbegu mpya
Mtalamu wa Vikonyo vya kahawa akimwelekeza Mkuu wa Mkoa Dr Binilith Satano Mahenge jinsi ya kuzalisha miche ya vikonyo
Hapo mtalamu wa vikonyo akimwonyesha kwa vitendo Mkuu wa Mkoa jinsi ya kuzalisha miche ya kahawa
Mkuu wa Mkoa akisikiliza maelezo ya watalamu wa kilimo cha kahawa kutoka kulia ni katibu tawala Bendeeko,kushoto Mkuu wa Wilaya ya Mbinga
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akiwa Tunduru kupokea maelezo ya miradi ya maji Miradi ambayo ili mkera
Wilaya ya Mbinga ime weka kipao mbele Zoezi la Madawati kwa kutengeneza madawati ya chuma ili yadumu muda mrefu

Wananchi wa kigonsera waki mlalamikia Mkuu wa Mkoa kuhusu fedha yao milioni 11 iliyo chukuliwa na Halimashauri ya Mbinga ambayo mkuu wa Mkoa ameamuru irudi mara moja
Katibu tawala wa Mkoa akimtambulisha mkuu wa wilaya ya Mbinga katika uteuzi wa hivi karibuni
Huo ni umati wawananchi wa Kigonsera waki lala mimika kuhusu zahanati ambayo ujenzi wake bado uko kwenye msingi .Mkuu wa Mkoa Dr Binilith Satano Mahenge ameahidi kusimamia ujenzi huo na kuhakikisha wananchi wana pata Zahanati
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Satano Mahenge akiongea na wananchi wa kigonsera kuwa taka kushiriki maswala ya maendeleo
Afisa mipango wilaya ya Tunduru Mapunda akijibu swala la ujenzi wa Zahanati na kuahidi kuwa kila kitu kinacho husu kupaua zahanati vyote vimesha andaliwae
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Satano Mahenge akiwa katika eneo la uzalishaji umeme chipole Mashine ambazo zina toa Megawati 7 za umeme .umeme ambao ume kuwa ukombozi kwa wana nchi wa Moka wa Ruvuma
Daraja hili ndilo linalo linalo tumika kuvukia wananchi wa chipole, Mkuu wa Mkoa ameagiza wilaya ya Mbinga na wilaya ya Songea kushirikiana kuweza kujenga daraja imara
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Satano Mahenge amewaomba wananchi wanao ishi maeneo ya Mradi wa Umeme kuacha kuiba nondo za Daraja yoyote atakaye kamatwa hatua kali zichukuliwe dhidi yake
Ramani ya Mtambo wa Umeme wa Chipole ulio chukua garama zaidi ya fedha za kimarekani Dola 25 elfu
Mkuu wa wilaya ya Songea akivuka daraja katika eneo la Mradi wa Chipole
Nyuma ya Mkuu wa Wilaya ya Songea ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma  Dr Binilith Satano Mahengeakivuka daraja lililo jengwa kwa mtindo wa Nondo
Mara baaMradi kulinda vyanzo da ya kuvuka katika daraja la Chipole ametoa agizo kwa wananchi walio kuwa karibu na Mradi kulinda vyanzo hivyo

ZIARA YA MKUU WA MKOA WA RUVUMA DR. BINILITH SATANO MAHENGE WILAYANI TUNDURU KATIKA KUTEMBELEA MAENEO YA UTAWALA KUJITAMBULISHA NA KUPATA CHANGAMOTO ZA WANANCHI


Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Satano Mahenge alipotembelea Taasisi ya Kihuma kuona shughuli za Maendeleo akiwa na Dr Matomola katikati Mkuu wa Taasisi ya KIUMA na kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko. Dr Matomola ameomba Rais kutembelea kwenye Taasisi yake katika sherehe za jubilei ya miaka 25 ya kuanzishwa kwa Taasisi hiyo.
Dr matomola akielezea namna wanavytoa mchango wa maendeleo kupitia Taasisi yake ya KIUMA wilayanik Tunduru ambayo inatoa Elimu kuanzia ngazi ya Sekondari Chuo cha Ufundi Stadi Veta na Chuo cha Wauguzi  ambapo inahusisha na utoaji huduma za Afya kwa wananchi wa Wilaya ya Tunduru.
 Aidha amemuomba Mkuu wa Mkoa kufikisha ujumbe Serikali wa kuomba kupatiwa mkoas wa SELUU ili kusogeza huduma karibu kwa Wananchi kuliko sasa ambapo kutoka tunduru hadi Makao makuu ya Mkoa ni umbali wa KM 280.
Jamii ya Wafugaji waliopo eneo la Mtina wilayani Tunduru walipotembelewa katika Ziara ya Mkuu wa Mkoa wametakiwa kuhama eneo hilo kwa kuwa ni eneo la Hifadhik ya Seluu Serikali inawatafutia Eneo la kuhamia.
Jamii ya Wafugaji walioko Kijiji cha Mtina wanafuga Ng`ombe zaidi ya 1500 ambapo pana familia zaidi ya 500 kutoka kwenye jamii hiyo ya wafugaji. Wafugaji hao wameomba ma Afisa Mifugo kuwatembelea na kuwapa Elimu ya ufugaji wa Kisasa na ushauri mbalimbali katika ufugaji.
Mkuu Mkoa wa Ruvuma akihutubia Wananchi wa Kijiji cha Matemanga  aliweza kubaini kero ya Maji na kusua sua kwa Miradi ya maji inayoendelea wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma DR Binilith Satano Mahenge katika Ziara hiyo wilayani Tunduru aliweza kubaini Jumla ya Miradi kumi ya Maji  iliyogharimu kiasi cha Shilingi 4,462,364,220.00 ambayo haikumridhisha utekelezaji wake.
Katika Ziara hiyo pia aliweza kukagua ujenzi wa Barabara ya Tunduru - Songea kwa kiwango cha lami ambayo ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wake inayotarajia kukamilika ifikapo Oktoba mwaka huu.
Hiyo ni sehemu ya ujenzi wa Barabara hiyo katika daraja la Mto Nampungu yenye urefu wa mita 100 kama inavyoonekana wakati mkuu wa mkoa Dr Mahenge na Msafara wake wakikagua ujenzi wa Barabara.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Satano Mahenge akiwa katika Mto Nampungu ambako ujenzi wa Daraja kubwa unaendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr. Mahenge akiwa katika Kijiji cha Lukumbule ambako kuna Mradi wa Maji unaendelea akielekea kwenye Matanki ya maji kukagua hali ya maendeleo ya ujenzi huo.
Mkuu wa Mkoa akimba maelekezo ya namna ulivyotekelezwa mradi huo wa maji katika Kijiji cha Lukumbure.
Tanki la Maji katika Mradi wa Lukumbule uliogharimu kiasi cha Shilingi 475,472,151 ambao umefikia Asilimia 95%    .
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Mahenge akikagua Mradi huo alilazimika kupanda juu ya Tank la Maji kujua uimara wa Tank hilo kama anavyoonekana hapo juu.

Mkuu wa Mkoa katika ziara hiyo amebaini uzembe ulio fanywa na wahandisi wa Maji wilaya ya Tunduru kulipa fedha bila kufutilia miradi hiyo na kupelekea miradi 9 kutokamilika wakati fedha zake zimetoka, kutokana na hilo amelazimika kuunda tume ili kujua jinsi zilivyotumika fedha za miradi hiyo.
Wananchi wa Wilaya ya Tunduru wamemuomba Mkuu wa mkoa wa ruvuma kuwafuatilia watendaji wake kujua namna wanavyowatumikia wananchi ambapo amewataka wananchi kuwa watulivu yeye atahakikisha maji yanapatikana Tunduru na hatua zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kuhujumu miradi ya maji.
Wananchi wajasilikamali wa wsilaya ya Tunduru wakifurahia kutembelewa na Mkuu wa Mkoa kubaini kero zao huku wakiwa na imani ya kusimamiwa na kuhakikisha wanasonga mbele kwa kuinua uchumi wilayani humo.
Mjasiliamali tina wilayani Tunduru

Mkuu wa Mkoa wa ruvuma Dr. Mahenge pia alitembelea Kiwanda cha kubangua Korosho kilichopo wilaya ya tunduru kuona hali ya uendeshaji wa kiwanda hicho na changamoto zinazojitokeza.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma DKT Binilith Satano Mahenge alipopewa Taarifa ya Miradi  ya maji na Kaimu Mhandisi wa Maji wilaya ya Tunduru Michael Kasangano  aligunduwa kutolewa kwa Kiasi cha Shilingi 1, 983,584,119.90 fedha ambazo zimechukuliwa pasipo kufanyika kazi katika baadhi ya Maeneo ya Miradi ya maji.


Katika ziara hiyo imebaini miradi mbalimbali ya maendeleo ime kuwa na usimamizi hafifu na kuitia hasara serekari kutokana na uzembe  wa Wakuu wa idara