KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, July 17, 2013

KUFUFUA ZAO LA KOROSHO NCHINI TANZANIA

Dr louis Kasuga Mtaalamu wa Utafiti wa Magonjwa ya korosho alisema baada ya juhudi za serikali kufanya utafiti na kubaini chanzo  cha matatizo na sababu zilizopelekeakuzotota kwa zao la Korosho iliweza kuongeza uzalishaji wake kutoka tani 16,000 kwa mwaka hadi kufikia tani 158,000 kwa mwaka, kwa kutambua umuhimu wa zao hili la biashara ambalo ni la  pili Tanzania kwa kuingiza pesa za kigeni kutoka Nje.


Miongoni mwa kazi zinazofanywa na Kituo cha Utafiti wa Zao la Korosho Naliendele kilichopo Mkoani Mtwara ni kufundisha wakulima wa zao hilo mbinu bora za upandaji wa zao la korosho kwa njia ya ubebeshaji wa miche ya mikorosho. Picha unayoiona hapo juu ni Miche ya Mikorosho inaweza kupandwa kwa kubebeshwa kitaalamu

Wakulima wa Zao la korosho kutoka mikoa ya Njombe, Mbeya na Ruvuma wamesema chanzo cha kuzorota kwa zaola korosho ni kuchelewa kwa pembejeo, bei ndogo ya kuuzia na ukosefu wa masoko
 Wahiriki 125 wa Mafunzo ya uendelezaji na ufufuaji wa Zao la Korosho yaliofanyika Manispaa ya Songea ukumbi wa Chuo Kikuu Huria yaliyojumuisha wakulima, Maafisa Ugani, Wapuliziaji na  Maafisa Ushirika wa vyama vya Msingi kutoka wilaya za Songea Vijijini,Namtumbo, Mbinga, Rudewa na Kyela.
 Washirikiwa Mafunzo ya ufufuaji na Uendelezaji wa zao la Korosho wakiwa ndani ya ukumbi wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika Mafunzo hayo yaliyoendesha na wawezeshaji kutoka Kituo cha Utafiti wa zao la Korosho Naliendele chini ya Dr. Louis Kasuga na kugharamiwa na CIDTF (Cashew Industry Development Trust Fund).
 Washiriki wa Semina juu ya ufufuajina uendelezaji wa zao la korosho wakifuatilia elimu Bora ya Kilimo cha zao la Korosho ili kuinua viwango vya ubora na uzalishaji bora wa zao hilo, namna ya kuanzisha zao la korosho, kulihudumia, kulifufua na kuboresha Shamba la zamani.
 Washiriki wa Mafunzo ya uendelezaji wa zao la Korosho kutoka wilaya za mikoa ya Mbeya, Ruvuma na Njombe wakisikiliza mada kwa makini katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Huria Songea Manispaa.
 Wataalamu kutoka Kituo cha Utafiti wa Zao la Korosho Naliendele wakiseti mitambo tayari kwa kuendesha mafunzo juu ya uanzishaji, ufufuaji na uendelezaji wa Kilimo cha zao la korosho.
 Wataalamu kutoka Kituo cha Utafiti wa zao la Korosho cha Naliendele wakiwa Mkoani Ruvuma katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria kuwezesha mafunzo juu ya ufufuaji na uanzishaji wa zai la korosho. mwenye kofia kushoto ni Mtaalamu wa Magonjwa na wadudu wanaoshambulia zao la korosho Mr. Barnaba Maarufu kama BB, na wa pili mwenye laptop mbele ni Bw. Maiko Nkondora mwasibu wa Kituo cha Utafiti cha Naliendele.
Dr. Louis Kasuga aliyeshika Projekta kwenye meza akiendelea kuonyesha changamoto zinazozorotesha zao korosho kwa washiriki wa Mafunzo ya ufufuaji na ufuaji na uanzishaji wa zao la korosho yaliyofanyika manispaa ya songea na kujumuisha washiriki kutoka wilaya 5 za mikoa ya Ruvuma, Njombe na Mbeya. Mwenye Jaketi ya Bluu katikati ni Mwanahabari Mkongwe wa Kituo cha Utafiti wa zao la korosho Naliendele Bw. Fakii Mussa. na kulia kwake ni Mtaalamu wa uanzishaji wa shamba jipya na upandaji wa zao la korosho Bw. Swrtbert Magani.

No comments:

Post a Comment