KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, July 11, 2013

ORYX YA TINGA SONGEA


Habari njema kwa Wanasongea,

"Katika muendelezo wa kusogeza huduma na bidhaa za Oryx Gas kwa wateja
wetu, ORYX Gas imefungua rasmi duka na depot ndogo mtaa wa SIDO kituo cha
mafuta kwa Komba- Mjini Songea. Tunasema sasa adha ya kukatika kwa nishati
muhimu ya gesi katika mkoa wa Ruvuma sasa baaasi" alisema Bwana Mahfoudh
Maulid- Meneja Mauzo wa Oryx Gas.

Tunataraji duka letu litasaidia kuhakikisha upatikanaji wa gesi katika mkoa
wa Ruvuma kwa bei elekezi ili kumlinda mteja wa ORYX Gas. Tunawaarifu
wasambazaji wetu wa Oryx, kuchukua bidhaa za Oryx kutokea duka letu na
kukemea kupandisha bei kiholela. Oryx ilianzisha utaratibu wa bei moja nchi
nzima kuanzia Decemba mwaka jana na bei kwa mtumiaji wa mwisho imekuwa shs
22,000 shs 54,000 na shs 133,000 kwa mitungi ya kilo 6, kilo 15 na kilo 38.


Aidha, Bwana Mahfoudh alihimiza watumiaji kuhakiki mitungi ya gesi
wanayonunua ina vizibo maalum au "seal", na wadai kupimiwa katika mizani
wanunuapo gesi. Uzito wa mtungi pamoja na gesi iliyomo ndani ya mtungi
vimeandikwa juu ya mtungi.

Hali kadhalika, Mahfoudh alinadi utaratibu mpya wa "Piga Uletewe" kwa maana
ya kuwa huhitaji tena kuhadaika na mtungi wa gesi ila tu piga simu uletewe
gesi nyumbani, mgahawani na hotilini kwako. Namba ya simu ya mhudumu wa
duka la Oryx ni 0758 002 090.

Kwa msisitizo mkubwa, Mahfoudh amewaomba wananchi kuwa makini na kutokubali
kubadilishiwa mitungi isiyokuwa rangi nyekundu ya Oryx. Wateja wetu
wanadanganywa na kufanyiwa uhuni usiokubalika kwa mujibu wa Sheria za Gesi
ya LPG. Mteja atapopeleka mtungi wa Oryx kwa muuza duka, amtake kumpatia
mtungi wa Oryx wa rangi nyekundu na si vinginevyo. Usisite kutoa taarifa
kwa namba +255767062896 endapo utafanyiwa uhuni huu.  Hili ni kosa kisheria
na Oryx inao wajibu wa kuchukua hatua kali za sheria kwa watuhumiwa.Kwa hali ya kipekee kabisa, nitoe tena shukrani za dhati kwa wateja wetu
wapendwa wa ORYX GAS, Taasisi mbalimbali za serikali na binafsi, wadau
mbalimbali ambao kwa pamoja tumekuwa tukishirikiana kunadi na kuelemishana
kutumia nishati mbadala kama ORYX GAS ili kutunza mazingira yetu.
Oryx Gas
ni nishati mbadala ambayo ni Safi, Salama, Garama nafuu, Chapchap na rafiki
wa afya na Mazingira.

Endelea kufurahia nishati yako ya Oryx Gas, na kwa wasambazaji wapya,
tafadhali tuma sms au piga simu namba kwa Sales Person wetu wa kanda
+255759588115 au moja kwa moja kwa Meneja Mauzo 0755 017 073.
Oryx Gas,
Mtindo wa Kisasa!

No comments:

Post a Comment