KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, July 24, 2013

MAZISHI YA SHUJAA RODNEY NDUNGURU ALIYEFARIKI NCHINI SUDANI AKILINDA AMANI


Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majenshi Nchini Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ameitaka Familia ya Marehehu Rodney Ndunguru na Watanzania wote kuwa na Moyo wa Subira kwa kifo cha Praiveti Rodney Ndunguru kilicho mpata huko Durfer Sudani  13/7/2013 baada ya kuvamiwa na waasi

Mheshimiwa Amiri Jeshi mkuu Jakayaya Mrisho Kikwete ameya sema hayo wakati akitoa salamu za Rambirambi kwa Familia ya Marehemu Rodney Ndunguru salalamu zilizo somwa na mwakilishi wa  Briged ya 401  Tembo  brged  kanaliGeorge Tomasi Msongole

 Jeneza la Rodney Ndunguru muda mfupi kabla ya kuzikwa katika Makaburi ya Mjimwema Songea.
 Afisa Tawala Wilaya ya Songea Joseph John Kapinga katikati akiwa na Maafisa wa Jeshi katika Maombolezo ya Msiba wa Rodney Ndunguru Mjimwema Songea Mkoani Ruvuma.
 Jeshila la Wananchi (JWTZ) lina taratibu zake katika kutoa heshima za mwisho kwa mwenzao anapofariki, hapo ni wanajeshi wakitimiza taratibu za heshima za mwisho katika viwanja vya Makaburi ya Mjimwema Songea ikiwa ni ishara ya kumuenzi Shujaa Rodney Ndunguru aliyefariki tar 13/07/2013 huko Darful Sudani akitekeleza Jukumu la Kimataifa la kulinda Amani.
 Jeneza lililohifadhi Mwili wa Marehemu Rodney Ndunguru likiwa limetolewa Bendera ya Taifa na Mavazi aliyokuwa akiyatumia tayari kwa kuingizwa kwenye Makao ya milele.
 Wanajeshi wakiwa katika viwanja vya Makaburi ya Mjimwema wakiendelea kutoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu Rodney Ndunguru kadiri ya taratibu za ki Jeshi.
Katika mazishi hayo yaliyo fanyika katika makabuli ya Mjimwema manspaa ya Songea ya liweza kuhudhuliwa na viongozi wa serekari wa kiwakilishwa na katibu tawala Joseph John Kapinga ,jeshi la wananchi wa Tnzania ambapo heshima zote za kijeshi zilitolewa
 Wanajeshi walioshiriki msiba wa Mwenzao Rodney Ndunguru wakitafakari changamoto zinazowakabili katika kulinda amani.
 Mamia ya waombolezaji Wanajeshi wakiwa na huzuni katika kumsikitikia mwenzao aliyekufa kishujaa katika kutekeleza Majukumu ya Kitaifa wakiwa nyumbani kwa Marehemu Mjimwema Songea Mkoani Ruvuma kabla ya Mazishi.


Padre Noi Duwe akiendesha misa amesema swala la uvunjifu wa amani una tokana na kuto tii sheria zinazo tolewa serekari badala yake kuendeleza migomo na maandamano amewataka waumini waache kukashifu serekari

Msemaji wa Familia ya Marehemu Rodney Ndunguru amewaomba wa Tanzania kudumisha amani katika nchi yao bila ya amani ya kudumisha amani yata tupata yanayo tokea Sudani hivi sasa hatunge weza kumpoteza ndugu yetu Rodney Ndunguru lakini ni kutokana na kukosekana kwa Amani

Maafisa wa Jeshi wakitoa vifaa vya kazi (kofia, Sare, Mkanda na viatu) alivyokuwa akivitumia Marehemu Rodney Ndunguru wakati wa uhai wake tayari kwa Mazishi

 Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) wakitoa heshima zao za mwisho kwa Shujaa Rodney Ndunguru kwa kupiga Risasi  hewani mara baada ya mazishi yake katika Makaburi ya Mjimwema Manispaa ya Songea

Captaini Patrick Kitosi kutoka kikosi cha 92 akisoma wasifu wa marehemu Rodney Ndunguru amesema Rodney Ndunguru alizaliwa 9/7/1985 Mjimwema mkoani Ruvuma alikuwa kijana shupavu, aliweza kufuzu mafunzo ya ukomandoo dalaja la pili na dalaja la tatu. Alisha wahi kwenda Dur fur mara mbili katika jitihada za kulinda amani Umoja wa Mataifa wa Nchi za Afirika alipata nishani akiwa Durfur Sudani


Mheshimiwa Rais  Jakaya Kikwete amesema Marehemu Rodney Ndunguru alipwatwa na mauti hayo wakati akitekeleza jukumu la umoja wa mataifa wa Africa la ulinziwa amanikatika eneowalilo shambuliwa ghafula ambapo yeye na wenzake 6 waliweza kupoteza maisha.

Kanali Goerge Thomas Msongole akisoma salamu hizo kwa niaba ya Amiri jeshi mkuu wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amesema msiba huu ni wa wa Tanzania wote na Taifa lote hivyo ni wajibu wetu watanzania wote kushiriki katika maombolezo na maombi ya kumwombea ndugu yetu Rodney Ndunguru

 Jeneza lililohifadhi mwili wa Marehemu Rodney Ndunguru likitolewa ndani nyumbani kwake Mjimwema Songea tayari kwa kuelekea Makaburini kwenye Makao ya Milele.

No comments:

Post a Comment