KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, January 10, 2017

TAMASHA LA UTALII NYASA MKOANI RUVUMA

 hiyo ni hali halisi ya uzuri wa Ziwa Nyasa  kama inavyoonekana pichani ni safari ya kuelekea Kisiwa cha lundo kutokea Fisheries Mbamba Bay kufuatilia matukio ya vivutio vinavyopatikana katika kisiwa hicho na kujionea uzuri wa madhari ya mwambao wa Ziwa Nyasa Wanaoonekana kushoto ni Mwandishi wa BBC Maxmiliana Mtenga akiwa na Katibu wa Naibu waziri wa elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Yonafika Mzungu
 Wananchi wa Mwambao wa Ziwa Nyasa waliojitokeza kwa wingi kufuatilia matukio yaliyoambatana na uzinduzi wa Siku ya Utalii wilaya ya nyasa katika viwanja vya fishariz Mbamba Bay kandokando mwa Ziwa nyasa.
 Miongoni mwa vivutio vinavyopatikana katika Mwambao wa Ziwa Nyasa ni pamoja na utamaduni wa kuenzi nyimbo za asili, wakazi wa ziwa nyasa wameomba vijana kutodharau asili kwa kuzienzi ngoma za asili zinazomtambulisha mtu asili yake. Hiyo ni Ngoma ya muhambo ambayo inachezwa katika kusherehesha shughuli mbalimbali ama wakati wa mavuno.  Hapo wakifurahia fursa zilizopo Mwambao wa Ziwa Nyasa na kuomba wawekezaji kuja kuwekeza Nyasa kupitia fursa zinazopatikana wilayani Nyasa.
 Unapozungumza Mwambao wa Ziwa Nyasa na utamaduni wake huwezi kuikwepa ngoma ya Mganda ambayo inachezwa kwa mahesabu maalumu na ni ngoma pekee ambayo huchezwa watu wakiwa watanashati. Hapo wachezaji wa ngoma hiyo wakitumbuiza siku ya uzinduzi wa utalii wakielezea vivutio vinavyopatikana Ziwa Nyasa kuwa ni pamoja na Samaki wa Mapambo na ziwa Lenye fukwe nyingi mzuri.
 Wachezaji wa Ngoma ya \mganda wakitumbuiza kwa kujivunia uzuri wa Ziwa Nyasa na Fursa zilizopo katika ziwa hilo ikiwemo samaki zaidi ya aina 500 na Dagaa.
 Katika Tamasha hilo mashindano mbalimbali yalifanyika ikiwa ni pamoja na mashindano ya kuogelea kwenye maji ya Ziwa Nyasa na Kupalaza Mitumbwi. Pichani ni akina Mama wakipalaza Mitumbwi katika Ziwa hilo.
 Katika Shindano hilo la kupalaza Mitumbwi kwa upande wa wanawake aliyeibuka na ushindi ni bibi mwenye umri wa miaka 63 ambaye alidai amekuwa akifanya kazi ya kuparaza mtumbwi toka akiwa mdogo umri wa miaka 8 na shughuli yake kuu ni uvuvi ambao huufanya kwa kutumia mtumbwi shughuli ambayo inamwezesha kulea familia yake watoto na wajukuu.


Katika Tamasha hilo Naibu Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhandisi Stella Manyanya amewataka Wananchi wa Mwambao wa Ziwa Nyasa kutumia fursa zilizopo kwa ajili ya kuimarisha uchumi kupitia michezo na utalii. (Pichani ni Samaki wa Mapambo wenye rangi tofauti tofauti)
 Watalii waliokuja kushiriki katika Tamasha la Uzinduzi wa Utalii Mwambao wa Ziwa Nyasa wakisubiri usafiri wa boti tayari kuelekea katika visiwa mbalimbali kuona maajabu na mazuri yanayopatikana katika visiwa vya ziwa Nyasa.

Naibu Waziri wa Elimu amesema Ziwa Nyasa ni kitega uchumi kikubwa , hasa kwa kuanzisha Mashindano ya Mitumbwi katika kutembelea visiwa vilivyopo Ziwa Nyasa.

Mashindano ya michezo mbalimbali Ligi ya Uzinduzi wa Tamasha la Utalii wilaya ya nyasa yamemalizika kwa kupata mshindi wa mpira wa miguu kutoka timu ya yatima Fc baada ya mchuano wa timu 6 za mpira wa miguu zilizoshiriki ligi hiyo.
Tamasha hilo liliudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na wa Kimila Pichani kulia ni mhifadhi Mkuu wa Makumbusho ya Majimaji Bartazar na kushoto ni Dr Lucy Mwalimu wa chuo cha Utalii waliokuwepo kuona fursa za utamaduni na utalii.
 Katika Tamasha hilo lililofanyika kwa kushirikisha Nyanja mbalimbali za michezo kwa Timu za Mpira, Ngoma za Utamaduni, kuogolea, kukimbia,  mashindano ya kupalaza mitumbwi, washindi walipata zawadi mbalimbali
 Safari ya kuelekea katika kisiwa cha lundo. Watalii wakifurahia hali ya Ziwa lenye maji fresh.
 Baadhi ya Samaki wanaopatikana katika Ziwa Nyasa hapo Mvuvi akitoka kuvua samaki aina ya Hangu.
 Ngoma ya kihoda ni maarufu kwa wamama wa Mwambao wa Ziwa Nyasa kama unavyoona pichani ikichezwa kwa manjonjo ya aina yake katika kusherehesha sherehe ya uzinduzi wa utalii wialaya ya Nyasa
 Vifaa vya asili vya kuhifadhia nafaka au vinaweza kutumika kama mapambo ndani ya nyumba ambavyo husukwa na wakaazi wa mwambao wa ziwa nyasa vinapatikana kwa bei nzuri pamoja na uzuri wake wa kuvutia kama inavyoonyesha pichani.
 Vifaa vya asili, visugulio, ungo na makapo vyote vinapatikana katika Wilaya ya Nyasa.
Katika Tamasha hilo kulitanguliwa na michezo mabalimbali ikiwemo na mpira wa miguu ambao Yatima FC  iliibuka kidedea kufuatia fainali iliyochezwa baina ya timu za Yatima FC na Kings FC  za Mbamba Bay wilayani Nyasa ambapo mshindi wa kwanza alijipatia zawadi ya Kombe na jezi na mshindi wa pili akapata kombe na mpita wa miguu.

upande wa Mpira wa miguu Yatima FC walipata zawadi ya Kombe na Jezi seti moja na Mshindi wa Pili Kings FC walijipatia zawadi ya Kikombe na Mpira na washindi wa michezo mingine walizawadiwa pesa taslimu.

 Mkuu wa wilaya ya Nyasa Isabela Octava chilumba amewataka wakaazi wa wilaya ya Nyasa kuzitumia vizuri fursa zinazopatikana ziwa nyasa kwa kujipatia ajira pia kuzilinda. ameomba kushirikiana na wadau wenye nia ya kuwekeza katika mwambao wa ziwa Nyasa ili kuinua pato la wilaya mkoa na taifa kwa ujumla aidha ametahadharisha kutouza fukwe kiholela kwa kuwa ni kinyume cha taratibu.
 Wadau wakiwa katika mdahalo wa kujadili fursa za utalii zizilopo wilaya ya Nyasa namna zinavyomnufaisha mwananchi husasani mkaazi wa Mwambao wa Ziwa Nyasa. Katikati mama Helen Mahenge.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge amewaomba wawekezaji kuja kuwekeza Nyasa kupitia fursa za usafirishaji, amesema Nyasa kunahitaji usafiri wa majini na Hoteli kwa kuwa ni wilaya ya kitalii ambayo ina vivutio vingi vya kitalii.
 Mkuu wa Mkoa wa ruvuma Dr mahenge amesema wasomi wazawa wa wilaya ya Nyasa ni vizuri sasa wakaja kuwekeza nyumbani kwa kuweka viwanda na uwekezeji mwingine kulingana na fursa zinazopatikana katika wilaya hiyo kwa kuwa sasa barabara ya mtwara - mbinga imefunguka kwa kiwango cha lami tunategemea kupata wageni wengi watakaohitaji kuwekeza mwambao wa ziwa Nyasa.
 Kisiwa cha Lundo ambacho wavuvi hutumia kujistiri pindi wanapozidiwa na dhoruba wakiwa ziwani pia ni kisiwa ambacho kilikuwa makaazi ya wagonjwa wa ukoma wakati wa ukoloni ambao walitengwa kutokana na ugonjwa.
 Katika Tamasha hilo pamoja na maonyesho mbalimbali pia kulikuwa na kitoweo cha samaki wanaopatikana katika Ziwa Nyasa kama wanavyoonekana piachani ni samaki aina ya Hangu wakiwa wamechomwa kwa ufasaha katika kisiwa cha Lundo
 Afisa Utamaduni wa wilaya ya Nyasa Charles haule amesema wilaya ya Nyasa ina hazina kubwa ya kiutamaduni ambayo ikitumika vizuri kwa kushirikiana na halmashauri itachangia pato la wilaya kukuwa.
 Watalii wa ndani waliopata fursa ya kuzunguka katika visiwa mbalimbali vilivyopo ziwa nyasa wakiingia katika kisiwa cha Lundo kwa Boti.
 Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na teknolojia Mhandisi Stella Martin Manyanya akiongoza msafara wa kutembelea vivutio vilivyopo Kisiwa cha pomonda liuli wilaya ya nyasa mbele ni mhifadhi wa eneo hilo bw. Josefu Ndomondo
 Camp ya Liuli pomonda ambayo imewekwa kiasili ni sehemu nzuri ya utalii kama unavyoona kitanda chenye mithili ya mwavuli ambacho hutumiwa na watalii wanaokuja kutembelea katika kisiwa cha pomonda chenye jiwe lenye pango ambalo lilitumiwa wakati wa vita vya dunia kujificha wasiuwawe ambalo lina uwezo wa kuhifadhi zaidi ya watu 100
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Mahenge akizundua rasmi Tamasha la utalii wilaya ya Nyasa 30 dec 2016 kuashiria kuzifungua fursa za uwekezaji wa utalii katika wilaya hiyo. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba na kulia kwa mkuu wa mkoa ni Mhandisi Stella Manyanya (Mb) Naibu waziri wa Elimu anayefuatia kushoto ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nyasa Alto komba
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Mahenge  katika Uzinduzi wa tamasha la Utalii wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.

1 comment:

  1. HAKIKA NAJIVUNIA KUWA MNYASA.KARIBU TUDUMISHE UTALII WA KWETU

    ReplyDelete