KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, August 26, 2012

MTOTO AFUNGA NDOA NA MAMA YAKE MZAZI - SONGEA

Umati wa watu uliofurika kwa Mganga wa Jadi Flora Ndembo Namabengo wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma watu wapatao 400 wameomba Serikali ichukue Mkondo wa Sheria pia Mtoto wa Pili wa Mama Kondrada Ngonyani ameomba Serikali ichukue hatua za kisheria dhidi ya condorada ngonyani na joseph Mapunda.
Joseph Mapunda mwenye umuri wa miaka 40 amesema ameweza kuishi kindoa na Mama yake Mzazi Condorada Ngonyani 70 baada ya yeye kukubaliana wenyewe yeye na mama yake mzazi kuishi kindoa kama mume na mke alipo ulizwa Mama alikiri kuwa kweli wameishi kindoa kwa miaka 10 na anampenda Mtoto wake Joseph Mapunda.Mama Condorada Ngonyani mwenye umuri wa miaka 70 ambaye ana ishi kinyumba na mtoto wake watatu wa kumzaa mwenyewe kama Mke na Mume hapo anaonekana akisononeka kwa nini jamii iingilie ndoa yake

Kwa mkoa wa Ruvuma hii ni mara ya kwanza mtoto wa kiume Joseph Mapunda pichani hapo juu kutembea na mama yake mzazi. Wana Ruvuma wanauliza tume jikwaa wapi watanzani hadi kupoteza mila desturi na maadili ya mtanzania pia kukiuka sheria za dini
Joseph Mapunda ana sema upendo ni upendo amempenda mama na anaishi kindoa wamependana nyie watu mnataka nini kwetu ?
Mama Condorada Ngonyani anasema mara baada ya kufariki mume wake Mzee Mapunda alimchagua mtoto wake amrithi baba yake Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maendelo ya Jamii, Jinsia na wtoto kuangalia kati sheria inayomruhusu Mtoto na Mama Mzazi kuweza kuishi kindoa

2 comments:

  1. Hakika huko tuendako sasa ni kubaya...hii inabidi ichukuliwe hatua.Mila na desturi zimeenda wapi jamani? mtoto na mama kuwa mke na mume lazima kutakuwa na shetani amewaingia...

    ReplyDelete
  2. Nimejaribu kufikiri ni kwanini cpati jibu,huu sasa hivi ni ushenzi mtupu,hii ni laana tupu

    ReplyDelete