KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, November 27, 2011

MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO JENISTA MHAGAMA AMWAGA MTOTO WAKE BAADA YA KUPATA JIKO

Wabunge kutoka Nzanzibabar ,Tanzania Bara walikuja kumunga mkono mwenzao katika kumwaga mtoto wake kipenzi Ledina Mhama hapo wanaonyesha wakicheza kwa furaha zote.

Jambo la pekee linalo furahisha familia ni pale unapo ona umeweza kumsomesha mtoto wako na mtoto akapata mchumba na wewe mzazi upo. Picha ya juu ni Mama Pinda ambaye alikuja kushuhudi mtoto wa Mwenyekiti la Bunge la Tanzania Mh.Jenista Mhagama alipo kuwa akimwaga mtoto wake baada ya kupata mchumba

Mila na Desituri zina faa kuzingatiwa kwa mila za kingoni huwezi kuchukua zawadi kwenye vyombo vya kichina hapo mh. Jenista Mhagama anaonyesha jinsi anavyo heshimu mila na desturi kwa kuchukua zawadi na kuweka kwenye Jamanda akimzawadia mtoto wake Ledina Mhagama

Binti ledina Mhagama akiwa katika nyuso ya Huzuni kuona ana achana na familia aliyo izoea na kwenda kuanza maisha mapya na mchumba wake baada ya Ndoa


Kwenye sherehe huongozwa na chereko hoi hoi na vigelegele hapo Mama Pinda mke wa wawaziri mkuu Mh.Mizendo pinda akipiga makofi baada ya mshenezi kutoa mistari yenye kusisimua

Sherehe haikosi chereko Vijana wanao onekana ni kikundi cha mganda kikitumbuiza kumwaga Ledina Mhagama huku mama yake mzazi Jenista Mhagama naye akicheza ngoma hiyo kwa furaha zote


Mwanamziki wa zamani Makasi kutoka zaire aliimba furaha ipo aina mbili kucheka na kulia hapo juu ni Mke wa Mheshiwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Mh. Tomasi Sabaya akiwa analia haijulikani ni uchungu au furaha

Viongozi walijitoa kwenda kumfariji Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama huyo anaye toa nasaha ni Mke wa Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Said Thabiti Mwambungu akimwasa mtoto akaishi vizuri na mchumba wake baada ya kufunga pingu za maisha

Mama Mwambungu akitoa zawadi kwa Ledina Mhagama aliye kuwa kulia ,zawadi ya Sufuria ili akaweze kumpikia mumewe na kama atabahatika akapikie uji kwa mtoto atakaye zaa

Ndugu za Ledina Mhagama wakiwa wame zunguka meza wakiendelea kumpa nasaha za maisha mema

3 comments: