KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, April 28, 2012

MTOTO WA AJABU AZALIWA SONGEA SEHEMU ZA SIRI ZIKIWA KICHWANIAdam nindi Songea

Mtoto wa ajabu amezaliwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma akiwa na sehemu nne za siri za kike na za kiume mbili zikiwa kichwani na mbili zikiwa katika hali ya kawaida.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Mathayo Chanangula amesema Mzazi wa Mama huyo ajulikanaye kwa Jina la Situmai Hausi na Mume wake Said Abdalah wameweza kubahatika kuzaa mara tatu na huyu ni mtoto wa nne .

Mganga Msaidizi Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Mathew Chanangula amesema kuzaliwa kwa Mtoto huyo kuwa katika maumbile hayo yanaweza kutokana na kutumia Madawa Makali wakati akiwa Mjamzito.

Mathew Chanangula amesema waja wazito wengi huharibu mimba kwa kutumia madawa makali wakati mwingine watoto huzaliwa wakiwa na mdomo wa sungura hiyo yote hutokana na kutumia madawa yasiyo ruhusiwa na dakitari.

Mzazi wa mtoto aliyezaliwa katika Maumbile ya ajabu Said Abdalah amewaomba Wataalamu kuweza kumfanyia upasuaji ili mtoto sura yake iwe ya kawaida ,ameomba kuwa hali ya upasuaji silazima ifanyike hapa watalamu wowote wanao ona wana weza kumusaidia mtoto wake wamsaidie ..

Mama Mzazi wa Mtoto wa Kike amesema kinachotakiwa ni kupokea Mapenzi ya Mungu, Nao wuuguzi wa Wodi ya watoto wamesema kutokana na Maajabu ya Mtoto huyo wameamua kumuweka katika Wodi Maalumu ili kupunguza Wimbi la watu kumshangaa Mtoto huyo wauguzi hao wameomba jamii kutoa ushirikiano kwa mzazi wa mtoto huyo kuona hicho ni kitu cha kawaida.

Watu mbalimbali waliofika katika Hospitali ya Mkoa wameomba jamii kujitolea kwa hali na mali ili kumwezesha mtoto huyo kurudi katika hali ya kawaida aidha wame shirikiana na wazazi wa mtoto kuiomba serekari kurudisha hali ya mtoto kuwa ya kawaida .

2 comments:

  1. ni kumrudishia mungu sifa na utukufu maana tunaamini huyo mtoto ameumbwa na Mungu

    ReplyDelete