KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, June 11, 2014

MATUNDA NDILO SULUHISHO LA KURUDISHA NGUVU ZA KIUME -MKONGWE WA HABARI SONGEA

Ndugu zangu mara nyingi unapo zungumuza maswala ya Tendo la Ndoa watu wengi huona umekosa maadili, watu walio zaliwa miaka ya 1938 hadi 1961 wanajua maana ya Unyago au Jando, Katika eneo la Jando au Unyago kulikuwa na Mafundisho jinsi ya kuishi ndani ya Nyumba,
Nimeamua kupasua jupu hili ili wale ambao hawaja wahi kuingia Jando au Unyago wajue chanzo cha kuvunjika ndoa pia wajue kipi kina sababisha mwanaume kukosa nguvu za kiume, Nibora niweke wazi ili kwenye kujifundisha tuelewe tufanye nini, Mimi nime cchokoza lakini wewe kama unajua zaidi wasaidie wanaume wenzie pia saidia wanawake pia ,sasa hebu soma kwa makini,by Adamu Mzuza Nindi

MATUNDA UNAYO YAONA HAPO JUU YANA WEZA KUKUSAIDIA KURUDISHA UWEZO WA  NGUVU ZAKO ZA KIUME KUFANYA KAZI VIZURI

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume na kuacha idadi ya wanawake wanaokabiliwa na tatizo hilo kwa mujibu wa uchunguzi kubaki na asilimia 13. 
Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili. 
Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina kumi ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa.Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo:-
1. PILIPILI [CHOBOLA]
Pilipili zilizocheshwa zimetajwa kuwa na uwezo wa kusaidia msukumo wa usambazaji damu mwilini, ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo unaoweza kumfanya mtu akawa na hisia kali za kimapenzi. Kwa msingi huo, ni vema kwa wale wanaokabiliwa tatizo la uwezo wa kufanya mapenzi wakatumia pilipili si kwa wingi bali kwa kiwango stahili, ili waamshe hisia zao.
2. PARACHICHI
Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia kuongezamajimaji yenye utelezisehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana. 
3. NDIZI MBIVU
Wakati unafikiria uwezo wa kufanya vema tendo la ndoa unatakiwa kuwaza juu ya uimara wa misuli ya mwili ambayo inatajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye muhimu katika kujamiiana. Kwa msingi huo ulaji wa ndizi mbivu unatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini na kumfanya mtu aweze kuwa hodari katika tendo la ndoa. 
4. CHOKOLETI [KEKI ZENYE ASILI YA SUKARI ]
Ulaji wa Chokoleti huongeza uchangamfu mwilini na, hivyo kumuwezesha mtu anayeshiriki tendo la ndoa kuwa na mguso sahihi kwenye fikra zake, jambo litakalomuwezesha kupokea hisia za mapenzi kwa urahisi zaidi ya mtu ambaye anakwenda kwenye uwanja wa sita kwa sita akiwa mchovu wa mawazo. 
5. CHAZA NA PWEZA [SAMAKI WA BAHARINI ]
Aina hizi za samaki zinazovuliwa baharini huwa na madini ya zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia uzalisha wa vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa. 
6. POMEGRANATE [MATUNDA DAMU ]
Ni aina fulani ya matundamekundu yanayofananana na apple. Haya yatajwa kusaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumuongezea mtu uwezo kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa kubwa. 
7. MVINYO MWEKUNDU [NB;ZABIBU ]
Mvivyo mwenyekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na kuongeza msukumo wa damu, kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na baada ya tendo la ndoa, hivyo ni muhimu kunywewa hasa na wale ambao wanasumbuliwa na tatizo la kushindwa kurudia tendo. 
8. MBEGU ZA MATUNDA
Mchangayiko wa mbegu mbalimbali za matunda, mfano tikiti, maboga husaidia kuondoa ACID mwilini na kumfanya mtu ajione ni mwenye afya njema.
9. VANILLA
Vanila husaidia kuamasha hamasa mwili.Mwisho wa aina hizi za vyakula ni
10. TIKITI MAJI
ambalo linatajwa kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuusaidia mwili kuwa na nguvu za kutosha kufanya tendo la ndoa

NINI SABABU YA KUPUNGUA NGUVU ZA KIUME SOMA KWA MAKINI UELEWE


.Miongoni mwa mambo ambayo mwanaume hataki kuyasikia yakitoka kwenye kinywa cha mwanamke ni kuambiwa HAWEZI TENDO LA NDOA. Mwanamke akimwambia mwanaume wakati au baada ya tendo kuwa hawezi, atakuwa amemsababishia tatizo kubwa la kisaikolojia ambalo litampelekea kupotea nguvu za kiume taratibu.
Msaada unaohitajika kwa mwanamke anayekutana na mwanaume dhaifu kwenye tendo si kumwambia hawezi, bali ni kumtia moyo na kumsaidia kuweza. Wanawake wamewasababishia waume zao upungufu wa nguvu za kiume kwa kuwaambia maneno kama haya: “Yaani siku hizi sijui umekuwaje, yaani huwezi kazi kabisa!

MWANAMKE KUGEUKA YEYE NDIYE MUME
Wanawake wengi hasa waliopo kwenye ndoa, wanapuuza ujuzi kwenye tendo la ndoa. Hawajishughulishi kumsaidia mwanaume ‘kuwika’, si wabunifu na watundu, jambo hili humfanya mwanaume kushiriki tendo kwa kutegemea kupanda kwa hisia zake mwenyewe, hivyo anapokuwa amechoka au ana mawazo, hawezi kusisimka kwa vile hapati ushirikiano toka kwa mwenzake.
Pamoja na wengi kutokuwa wajuzi, lakini wapo wengine ambao ni watundu mno kwenye sita kwa sita kiasi cha kumfanya mwanaume ajione kama mgeni wa mchezo huo.
Kimtazamo, wanaume hupenda sana ushindi wakati wa ‘kazi’, lakini pale wanapogeuzwa ‘chekechea’ hupunguza uwezo wa kujiamini na kuruhusu hofu kuongezeka mawazoni mwao, hivyo kuwasababishia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Inashauriwa kwamba, mwanamke anapokuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya mapenzi hasa wakati wa tendo, asioneshe kiwango kikubwa kwa haraka bali amchukulie mwenzake kama mwanafunzi, asiwe na maneno kama: “Leo nakuja kukupa vitu adimu kuliko vya juzi, hakuna kulala kasi mtindo mmoja.” Kauli hizi huwaogopesha wanaume na kuwafanya wapungukiwe na nguvu.
MWANMKE KUJIPENDA KIUSAFI NA KITABIA
Mwanamke anapokuwa si msafi, huweza kumsababishia mwanaume matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume. Sote tunafahamu umuhimu wa usafi wa mwili na kero za uchafu wakati wa tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu atamfanya mwanaume apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa. Unadhifu wa mavazi na mwili ni muhimu sana katika mapenzi.
        MANENO YA KASHIFA
Jambo lingine linaloweza kumsababishia mwanaume upungufu wa nguvu za kiume ni gubu au karaha za maneno ya uchokozi yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Uchokonozi wa mambo, ugomvi, usaliti na hali ya kutokuwa na staha ni mambo yanayosababisha tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Mwanamke anapokuwa mwingi wa maneno ya kashfa, dharau na matusi huweza kumfanya mume amchukie na kutopenda kushiriki naye tendo. Uchunguzi unaonesha kwamba wanawake walioolewa wenye tabia hii, huwafanya waume zao wawe na msisimko wa kimapenzi kwa wanawake wa nje kuliko wake zao hao.
          MWANAMKE KUTOKA NJE YA NDOA YAKE
Tabia ya usaliti kwa mwanamke ni chanzo kingine cha mwanaume kupata tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Mwanaume anapoona, kuhisi au kubaini kuwa anasalitiwa, huumia sana moyoni, maumivu ambayo hatimaye humfanya muhusika kuwa na mawazo mengi ambayo humuondolea hamu ya tendo.
Mada hii imezungumzia zaidi wanawake, lakini vipengele vilivyomo kwenye somo hili vinatumika pia kwa upande wa wanaume kuwasababishia wanawake matatizo ya kupoteza msisimko wakati wa tendo.

8 comments:

 1. Greetings admin
  I like your topic, after reading your article very helpful at all and can be a source of reference
  I will wait for your next article updates
  Thank you, for sharing

  Penirum

  Penirum Asli

  Obat Pembesar Penis

  Titan Gel

  Vimax

  Hammer Of Thor

  Extenze

  Extenze Asli

  Viagra

  ReplyDelete