KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, June 5, 2017

KUIMARISHA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA MWAMBAO WA ZIWA NYASA KUTACHOCHEA MAENDELEO KWA KUONGEZA IDADI YA WATALII WATAKAOTEMBELEA NA KUONGEZA PATO LA WILAYA NA TAIFA



Wananchi wanao ishi katika mwambao wa ziwa Nyasa wametakiwa kuacha mtindo wa kuchafua mazingira kwa kuoshea Magari,Pikipiki,pamoja na kufua nguo huko ni kuhatarisha maisha ya viumbe wa kiwemo sa maki kwa kula sumu na sumu hiyo inaweza kuwa dhuru watu baada ya kula samaki wenye sumu

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Binilithi Satano Mahenge ameyasema hayo wakati wa kufanya usafi mwambao wa zaiwa nyasa   wilayani Nyasa mkoa wa Ruvuma kiatika kuadhimisha siku ya mazingira Duniani
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilithi Satano Mahenge amesema kufanya usafi mwambao wa ziwa nyasa ni kujiwekea utajili  mara wakifika watalii  kutembelea ufukwe  huo wa ziwa nyasa
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Mahenge amesema wananchi wakiimarisha usafi katika Ufukwe wa Ziwa Nyasa wata weza kuwafanya watalii watakao kuja kuweza  kuwa shawishi  watalii wengine  kuja  Mwambao wa ziwa  jambo ambalo lita kuza uchumi katika Wilaya Nyasa Mkoani Ruvuma  Tanzania pia litawezesha kuingiza fedha za kigeni.


Mkuu wa kituo cha  Police Wilaya ya Nyasa ambaye alishiriki katika usafi amesema jeshi la police kazi yake ni kusimamia sheria itahakikisha ufukwe wa ziwa Nyasa unakuwa safi yeyote atakaye vunja kanuni za usafi sheria itachukua mkondo wake.
 Zoezi la Usafi wa Mazingira likiendelea  likiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma katika fukwe za Ziwa Nyasa.
 Mkuu wa wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba amesema amefarijika sana kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kushiriki pamoja na wananchi wa wilaya ya Nyasa katika shughuli za usafi wa Mazingira ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi kujenga tabia ya kuhifadhi mazingira na kuyaweka safi daima.
 Mkuu wa kituo cha  Polisi wilaya ya Nyasa akiendelea na zoezi la usafi wa Mazingira katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira ambayo wakaazi wa Wilaya ya Nyasa waliadhimisha kwa kufanya usafi kwenye fukwe zinazozunguka Ziwa Nyasa.

Nao wanafunzi walio hojiana na RFA wameahidi kufanya usafi wa Mazingira na kuboresha club ya Mazingira wanachohitaji ni ufadhili wa vitendea kazi kutoka kwa wadau na viongozi mbalimbali pichani Nemia James akifanya usafi mwambao wa Ziwa nyasa.

 Mwansshi wa Star TV na mkurugenzi wa Blog ya Songea Habari Bw. Adam Nindi akiwa katika hoteli ya Masisita Mbamba Bay katika kufuatilia hali ya Uhifadhi na usafi wa Mazingira yanayozunguka mwambao wa Ziwa Nyasa.
 Mkuu wa wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba akiwa katika Hosteli ya Masista iliyoko Mbamba Bay mara baada ya shughuli za Usafi wa Mazingira, kulia ni mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Mahenge na kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Nyasa Mr Mbambe
 Wananchi walioshiriki katika kufanya usafi maeneo ya fukwe za Ziwa Nyasa wameahidi kuwa walinzi katika fukwe hizo ili kuhakikisha zinavutia wageni kuja kutalii.
 Katika kuazimisha siku ya Mazingira wilaya ya Nyasa iliadhimisha kwa kufanya usafi kwenye fukwe za Ziwa Nyasa chini ya Mkuu wa wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba akishirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Mahenge na wadau wengine wa Mazingira.

Mkuu wa mkoa  wa Ruvuma Mhandisi Binilithi Satano Mahenge  akiwa wilaya ya Nyasa amevunja kamati ya usimamizi wa usafi Mbambabay baada ya wajumbe wake   kuto hudhuria  katika usafi pamoja na kushindwa kuwa baini wanao vua samaki kwa kutumia Gonga au njia ya Baruti

No comments:

Post a Comment