KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, December 3, 2017

CHUO CHA KILIMO NA MIFUGO MAHINYA NA UTENDAJI WA KAZI RUVUMA

Wanafunzi wa Chuo cha Kilimo na Mifugo Mahinya wakiw katika Eneo la Chuo hicho kilichopo Kijiji cha Nambehe Kata ya Msindo wilayani namtumbo Mkoa wa Ruvuma.
Chuo cha Kilimo na Mifugo Mahinya kinamilikiwa na Jimbo Katoliki la Songea kwa kushirikiana na Ufadhili wa Ubalozi wa Italia, Kinatoa Mafunzo ya Kilimo na Mifugo kwa Kozi ndefu za Miaka mitatu na kozi fupi kwa wanakijiji wanaozunguka eneo la Chuo.
Wanafunzi wa Kike waliopo Chuo cha Kilimo Mahinya wameshukuru kwa Elimu inayotolewa chuoni hapo wameomba wazazi kutochagua fani za kuwasomesha watoto wa Kike wanawza kuwapeleka chuoni hapo wakapata Elimu ya Kilimo na Mifugo.
Chuo Kilimo na Mifugo Mahinya Kina Madhari nzuri na Vifaa bora kwa Mafunzo ikiwemo Maabara ya kisasa ya kuchunguza Magonjwa mbalimbali ya Mifugo.
Wanafunzi wa Chuo cha Kilimo na Mifugo Mahinya wakiwa katika Mafunzo kwa Vitendo katika Shamba la Migomba katika Eneo la Chuo hicho.
Mwanafunzi wa Fani ya Kilimo Makrina Komba akiwa katika Bustani amesema kabla ya kufika chuoni hapo kupata Mafunzo alikuwa hajafaham mambo mengi kitaalamu lakini kwa sasa ana uwezo wa kuendesha Kilimo cha zao lolote na kupata tija.
Wanachuo wakiwa Shuleni wanapata Mafunzo ya Nadharia na Vitendo kama wanavyoonekana pichani wakimwagilia pilipili iliyolimwa kwa ajili ya kujifunza zaidi kwa vitendo
Unapofika Chuo cha Kilimo na Mifugo Mahinya unakutana na Ufugaji wa aina mbalimbali ikiwemo Ng`ombe, Sungura, Kuku na Samaki ili kuwafanya wanachuo wanapomaliza Mafunzo ya darasani wanarudi katika Vitendo na kuona maendeleo na tofauti ya ufugaji wa kitaalam na ufugaji wa kienyeji.
Pichani ni Ng`ombe wa Maziwa ambao wanapatikana katika Chuo cha Kilimo Mahinya wenye uwezo wa kutoa Maziwa kwa wingi, Ng`ombe hawa hutumiwa na wanafunzi kama sehemu ya darasa katika kukamilisha Mafunzo yao.
Chuo cha Kilimo na Mifugo Mahinya hakiishii kutoa Mafunzo ya Kilimo na Mifugo pekee bali hata Mafunzo ya Kompyuta yanatolewa chuoni hapo ili kuendana na utandawazi wa Teknolojia na Mawasiliano kama wanavyoonekana pichani ni wanafunzi wa Chuo cha Kilimo Mahinya wakipata Mafunzo ya Kompyuta kwa vitendo.

Mafunzo yanayotolewa Chuo cha Kilimo na Mifugo Mahinya ni Mafunzo endelevu ambayo humwezesha kijana anapomaliza kuweza kujiajiri au kuajiriwa mahali popote.
Baadhi ya Wanachuo wa Chuo cha Kilimo na Mifugo Mahinya wakiwa katika Darasa la Kompyuta.
Wanafunzi wa Chuo cha Kilimo na Mifugo Mahinya wilayani Namtumbo Mkoa wa Ruvuma.
Mwanafunzi Makrina Komba wa mwaka wa pili katika Fani ya Kilimo akieleze jinsi ya kupandikiza miche ya matunda na kuifanya ikue vzr na kutoa Matunda yenye tija baada ya muda mfupi.
Baadhi ya Mazao ambayo yanalimwa katika Shamba darasa Chuoni hapo ni pamoja na Matunda ya Matango kama linavyoonekana pichani, Mazao hayo licha ya kutumika kwa elimu pia hutumiwa kama chakula kwa wanachuo wanaoishi Hosteli chuoni hapo.
Jengo la Utawala la Ofisi za Uongozi wa Chuo cha Kilimo na Mifugo Mahinya.
Mwanafunzi wa Chuo cha Kilimo na Mifugo Mahinya akiwa katika Maabara ya Mifugo akifanya Mafunzo kwa vitendo.
Mwanachuo anayechukua Mafunzo ya Mifugo akiwa katika Maabara ya Mifugo
Mwalimu akiwa na Wanafunzi wa Fani ya Mifugo akiendelea na Mafunzo ya Vitendo katika Maabara ya Mifugo chuoni Mahinya.
Wanachuo wakiwa maabara wakichanganya madawa ili kuchunguza bakteria katika damu ya mnyama, vinavyoonekana pichani ni baadhi ya vifaa ambavyo hutumika wakiwa maabara kuhifadhi sampuli mbalimbali za wanyama.
Mwanachuo aliyebobea kwa fani ya Mifugo akielezea namna wanavyomchunguza mnyama kubaini tatizo linalomkabili.
Mwanachuo akichunguza sampuli katika darubini ya kupimia damu ili kuchunguza matatizo ya wanyama.
M wandishi wa Blog ya Songea Habari Judith Lugoye akiwa na wanachuo wa Chuo cha Kilimo na mifugo Mahinya alipotembelea kujionea utendaji na uendeshaji wa Mafunzo chuoni hapo alifarijika na namna mabinti walivyoiva na kubobea na mafunzo wanayoyapata chuoni Mahinya.
Wanachuo wa Chuo cha Mahinya wakiwa nje ya Jengo la Maabara ya Mifugo.

Binti aliyebobea katika Ufugaji baada ya kupata mafunzo ya Mifugo chuo cha Kilimo Mahinya ameanzisha ufugaji wa Sungura ambao alianza na Sungura wa tatu na sasa ana sungura zaidi ya 15 ambao anawafuga kama sehemu ya Mafunzo kwa vitendo anasema sungura wakifugwa kitaalamu wanaongeza pato kiuchumi ambapo kila sungura mmoja huuzwa kwa wastani wa sh. 15,000 .
Baadhi ya wananchi wanaonufaika na uwepo wa Chuo cha Kilimo na Mifugo Mahinya wakiwa Darasani wakiendelea na Mafunzo ya muda mfupi ili kuwajengea uwezo wa kufuga kisasa kwa tija.
Darasa la watu wazima wanaopata mafunzo kwa Vitendo chuoni Mahinya ambao wanatoka katika Vijiji jirani vinavyozunguka Chuo hicho wamesema elimu wanayoipata imewawezesha kupata mapato mazuri na kumudu kujikimu mahitaji ya msingi na kusomesha kutokana na kuongeza mapato katika ufugaji baada ya kupewa mafunzo ya ufugaji wa kisasa.
Akina Mama nao hawako nyuma katika kuhudhuria mafunzo hayo ambao ndio walengwa zaidi wa Mafunzo hayo katika kuinua uchumi wa wananchi wa kipato cha chini.
Wanachuo wa Kozi fupi wakiwa darasani katika Chuo cha Kilimo na Mifugo Mahinya.
Wanafunzi Raia wanaopata mafunzo ya Kisasa ya Kilimo na Mifugo kutoka Chuo cha Kilimo na Mifugo Mahinya.
                                                             Wanachuo wakiwa darasani.
Mkurugenzi wa Shirika la COPE Antonela ambalo linafadhili Undshaji wa Chuo cha Mafunzo ya Kilimo na Mifugo Mahinya chini ya Ubalozi wa Italia akiwa na mmoja wa wanafunzi wa fani ya Kilimo chuoni hapo akimsikiliza anavyotoa Elimu ya Kilimo cha Matunda na Faida zinazopatikana.

  Mandhari ya Chuo cha Kilimo Mahinya kilichopo Namtumbo Mkoa wa ruvuma
Mmoja wa walimu waliobobea katika ufundishaji wa Mafunzo ya Mifugo na Kilimo chuoni Mahinya
Chuo cha Kilimo Mahinya kina Hosteli nzuri zenye usalama kama inavyoonekana moja ya chumba cha hosteli hicho hapo.

Tazama jinasi wanafunzi wanavyofurahia mafunzo wanayoyapata chuoni hapo wakiwa na nyuso za tabasamu, kwa kweli inapendeza zaidi kumpeleka kijana akapate Mafunzo endelevu ya kumwezesha kuishi kuendana na uchumi wa Viwanda.
                                             Mwanafunzi akiwa Maabara
Baadhi ya Vitalu vya miche ya miti ya kivuli na matunda vinavyoandaliwa chuoni hapo na kutumiwa kwa mafunzo pia kuwagawia wananchi wanaohitaji kufanya shughuli za Kilimo cha kisasa.
Vijana wakiwa katika Bustani na mwalimu akikagua maeendeleo ya wanafunzi kwa vitendo, kulia ni mkurugenzi wa shirika la COPE akiangalia kazi zinazofanywa na wanachuo hao.

No comments:

Post a Comment