KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, February 24, 2018

WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU JENISTA MHAGAMA ATEMBELEA MACHIMBO YA MAKAA YA MAWE KATIKA KIJIJI CHA MANIAMBA KATA YA MUHUKURU SONGEA VIJIJINI


Mwenyekiti wa Kampuni ya Kambas Group of Companies Yahaya Yusuph Kambaulaya amesema lengo la Kampuni yake kuchimba Madini ya Makaa ya Mawe ni pamoja na kuongeza Ajira kwa Vijana na kuleta Maendeleo kwenye kijiji cha Maniamba kwa kutoa ushuru unaopaswa kutolewa kwa Halmashauri asilimia 0.03%  na Serikali kuu asilimia 4%


Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera Bunge Ajira Vijana na watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama ameitaka Kampuni ya Kambas LTD inayochimba Makaa ya Mawe kufuata Sheria zilizowekwa na Serikali katika kuchimba Madini hasa Mrabaa unaotolewa baada ya kuchimba Madini.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati alipotembelea Machimbo ya Makaa ya Mawe yaliyopo Kijiji cha Maniamba Kata ya Muhukuru Songea Vijijini, Makaa yanayotarajiwa kuchimbwa kwa miaka 40, Waziri amesistiza Mapato yatakayopatikana kutokana na ushuru wa mgodi yafunguliwe Akaunt maalumu ili yawezeshe kufanya shughuli za Maendeleo ikiwemo ukarabati wa barabara.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Kambas Group of Companies Bi Safina Nasoro amesema Kampuni ya Kambas imeshapata Soko la kuuzia Makaa ya Mawe pamoja na bidhaa zingine zitakazotokana na Makaa ya Mawe.

Mgodi wa Kambas una Eneo la Hekarari 200 lakini ambazo zimeshapimwa na kubainika uwepo wa Makaa ya Mawe ni Ekari 45.  Mpaka sasa Sampuli ya Mkaa huo imepelekwa kwa wataalamu kuupima na kubainika kuwa una ubora wa hali ya juu.

No comments:

Post a Comment