KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, October 3, 2010

Huyu ndiye bwana Adam Nindi

Ndugu Msomaji wa Mtandao huu YALIYO JIRI MKOANI RUVUMA kwa Jina na itwa Adamu Mzuza Nindi , kazi yangu ni Mwandishi wa Habari napenda sana Kusoma vitabu mbalimbali kama vya dini,siasa, mambo ya Uchumi pamoja na kuelimisha wanchi kwa njia ya TV, RADIO na Magazeti ukitaka kuwasiliana nami unaweza kutumia E-mail adam_nindi@yahoo.com au tumia simu nomba 0755 731 234, 0658 731 231

MAISHA YA ADAMU MZUZA NINDI

Ndugu zangu ni vizuri kwanza kujua nani una zungumza naye pili ana pendelea nini.
Kwa jina naitwa Adamu Mzuza Nindi, nilizaliwa 7/7/1954 katika kijiji cha Chiulu wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma, Elimu ya shule ya msingi nilianza nikiwa na miaka 7 katika shule ya msingi Gatoma nchini Zimbabwe ambako wazazi wangu waliamu kwenda kufanya kazi katika machimbo ya Gatoma Mine zimbwabwe,

Nikiwa Zimbwabwe nilisoma hadi darasa la nne wazazi walipo amua kurudi Tanzania ,baada ya kusitahafu .baada ya kufika Tanganyika 1960 kutokana na kuto jua kiswahili nili rudia darasa la kwanza katika shule ya msingi chiulu liyoko Tarafa ya Mbambababay Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma, Nilianza maisha mapya katika kijiji cha Zoole kata ya Chiulu Tarafa mbambabay wilaya ya mbinga mkoa wa Ruvuma.

Nilisoma katika shule ya msingi chiulu baadaye nilihamia shule ya msingi Nyoni Mbinga baada ya kufaulu darasa la nne na kuchukuliwa na dada yangu Alice Nindi ambaye wakati huo alikuwa mwalimu wa shule ya msingi nyoni mbinga kilometa 40 kutoka kijiji cha chiulu .

Nikiwa darasa la tano nilihama tena kwenda kusoma wilaya ya Njombe Mkoa wa Iringa na kujiunga na shule ya msingi Mdete nikiwa dada yangu Alice Nindi ambaye wakati huo aliolewa na na Oddo Matembo ambaye alikuwa ana fanyia idara ya kazi Wilaya ya Njombe Mkoa wa Iringa.

Nikiwa darsa la sita nilihama tena na kwenda kusoma shule ya msingi Wangingombe katika wilaya iringa nilisoma kwa mdu wa miezi sita hatimaye kurudi tena shule ya msingi mdete hadi nilipo maliza shule ya msingi mwaka 1967.

Wakati nikingoja majibu ya mtihani wamatokeo ya darasa la nane dada yangu Alice Nindi aliamua kunipeleka shule ya kulipia mkoani Dodoma ijulikanayo kwa jina la Y.P.Insitute Ovada ambayo ili kuwa iki milikiwa na Father super .

Nilijiunga na Secondary ya Ovada 1968 na kumaliza masomo yangu mwaka 1972 nilijihusisha na maswala ya biasha kwa kufanya biashara kati ya Tanzania ,Malawi.Zambia,Zimbabwe, Msumbiji, Mpaka Africa kusini. Katika biashara zangu kwa asilimia kubwa likuwa na Tembea kwa mguu pale ilipo bidi biashara za Mkononi hatimaye nafaka mbalimbali.

Mwaka 1974 ili jiunga kuandikia gazeti la Watu ambalo lilikuwa likichapishwa Dar –es –Salaam nilifanya kwa mwka mmoja na kujiunga na Gazeti la Sani nako sikudumu nikajiunga na Gazeti la Mwenge la dini linalo chapishwa Peramiho Songea kipindi chote hicho lilikuwa nikijiendeleza na masomo ya uandishi wa habari,

Mwaka 1980 nilichukua masomo ya dini ya kiislamu na kuweza kufaulu vizuri nilianza kufanya mahubiri katika nchi za Malawi, Msumbiji, Zimbabwe na Zambia, na kuweza kufungua misikiti zaidi ya 5

Mwaka 1985 nililijiunga na Televisheni CNN ambayo makao yake yalikuwa Dar –es – Salaam nime fanyia Tv hiyo kwa muda wa miaka 4 na mwaka 1989 lianza kutuma habari Radio Free Africa na badaye kuanzishwa tv ambako niko mpaka sasa. napenda kuwa fahamisha elimu niliyo pitia na vyeti nilivyo pata na ambatisha hapa chini.

No comments:

Post a Comment