KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, October 21, 2013



Adam Nindi, Songea.



Dereva wa Shirika la Umeme TANESCO Tawi la Songea, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kusababisha ajali katika Msafara wa Waziri wa Maendeleo Mifugo na  Uvuvi Dr David Mathayo.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsmeki aliyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Ajali ilyotokea kutoka Mbambabay – Songea na kusababisha watu 5 kujeruhiwa ambao walilazwa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma.



Akimtaja Dereva anayeshikiliwa na Polisi amemtaja ni Ahamadi Hamisi 33 ambaye alikuwa akiendesha Gari lenye lenye No. za Usajili SU 37788  TOYOTAHilax iliyo  igonga gari no stk 9906 mali ya RAS Mkoa wa Ruvuma Akiwataja waandishi wa habari walio pata ajali na kulazwa ni   Joseph Mwambije, Lauf Mohamed, Lauf Mohamed, Cresensia Kapinga na Joicy Joliga na mwingine ni Abiria mmoja aliyekuwa kwenye Gari la TANESCO.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsmeki ameelezea  Madereva wa Shirika la TANESCO  Mkoani Ruvuma pamoja na kupewa onyo wamekuwa wakiendelea kwanda kwa  mwendo kasi.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsmeki amesema Madereva wa Shirika la TANESCO ambao huendesha kwa kasi gari zao, mara nyingi wapitapo mitaani wamekuwa wakizomewa na Wananchi ikiwa ni ishara ya kupinga mwendo mkali



 lakini hata hivyo wao huishia kuongeza mwendo .  Dereva Ahamad Hamis anayeshikiliwa na Polisi anahojiwa na upelelezi utakapokamilika atapelekwa Mahakamani.  



Waziri wa Maendeleo, uvuvi na Mifugo Dr. David Mathayo alikuwa Ziarani Mkoani Ruvuma kwa kutoa Majibu ya Utafiti juu Samaki waliokuwa wanakufa Ovyo katika Ziwa Nyasa Wilayani Nyasa na kugundua ilitokana na Uchafuzi wa Hali ya Hewa na siyo Sumu.

No comments:

Post a Comment