KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, April 25, 2015

BENKI TA POSTA TAWI LA SONGEA YATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI WALIOPATA UFAULU WA DARAJA LA I NA LA II KWA KUWAZAWADIAMeneja wa Benki ya posta Tawi la Songea Josph Shirima amesema Shabaha ya Benki ya Posta ni kuungana na Wazazi kutoa Motisha ili Wanafunzi waweze kujisomea kwa Bidii.
 Benki ya posta tawi la songea  iliahidi  kwa wanafunzi wa secondary ya zimanimoto Manspaa ya songea kuwa Mwanafunzi atakayepata Daraja la kwanza atapata 500,000 na Mwanafunzi atakayepata Daraja la pili atapata Shilingi 300,000 . Katika Ahadi hiyo Wanafunzi wawili waliweza kufaulu kwa kupata daraja la Pili. Joseph Kapinga Hafidhi AllyBenki ya Posta Tawi la Songea imewaomba Wazazi kuzingatia Elimu pamoja na kutoa Motisha kwa Wanafunzi pale wanapofanya Vizuri.
 Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Songea Joseph Shirima ameyasema hayo wakati akitoa Shilingi Laki Sita  kwa Wanafunzi wawili wa shule ya secondary ya zimanimoto iliyko Manspaa ya Songea  waliofanya vizuri katika Mitihani ya Kidato cha nne mwaka 2014

Waalimu wa Shule ya Sekondari Zimanimoto Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wakiwa katika Picha ya Pamoja na

 Vijana waliofanya vizuri katika ufaulu na wale walioonyesha vipaji vyao na kuvitumia vizuri wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Benki ya posta tawi la Songea Joseph Shirima, Shuleni Zimanimoto Manispaa ya Songea.
 Hapo Mchezaji Bora wa Soka kutoka Sekondari ya Zimanimoto akijinyakulia Kitita cha Sh 20,000 kutokana na kutoa heshima
 Mkuu wa Shule ya Sekondari Zimanimoto akimpongeza mchezaji Bora wa Mpira wa Miguu kwa kuiletea sifa Shule yake.
 Mchezaji Bora wa Mpira kutoka Sekondari ya Zimanimoto akipokea zawadi mara baada ya kufanya vizuri katika michezo kwenye mashindano mbalimbali yakiwemo ya kitaifa ya Copa Cocacola

 Waandishi wa Habari wakichukua Picha katika Ghafula ya Kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofaulu Shule ya Sekondari ya Zimanimoto Manispaa ya Songea.

Mwalimu Fulola Haule akitoa Shukrani kwa Meneja wa Benki ya Posta kwa kuthamini Elimu na kuunga Mkono katika kutoa Hamasa ya Vijana kupenda Masomo.

Hapo Joseph Shirima Mhitimu wa Kidato cha Nne Mwaka 2014 akipokea zawadi ya Shilingi laki Tano kutoka kwa Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Songea Joseph Shirima baada ya kufaulu daraja la Pili ikiwa ni Utekelezaji wa Ahadi aliyoitoa kwenye Mahafali yao ya kuwa Mwanafunzi atakayefaulu daraja la kwanza atazawadiwa kitita cha Sh. Laki Tano na atakayepata Daraja la pili atavuna Sh. Laki Tatu.
 Shule ya Sekondari Zimanimoto iliyopo Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma ni Shule ya Kata yenye Wanafunzi 215 kati yao wasichana 119 na wavulana 96 inafanya vizuri katika masomo lakini inakabiliwa na ukosefu wa hosteli na kusababisha wanafunzi kupata mimba kutokana na kutembea umbali mrefu
 Mkuu wa Shule ya Sekondari akimshukuru Meneja wa benki ya Posta kwa Mchango wake katika kuleta hamasa ya Elimu Shuleni Hapo.
 Waalimu wa Sekondari ya Zimanimoto wakitafakari jinsi ya kuboresha ufundishaji ili kuendelea kutoa Matunda Mazuri kwa vijana wao kupata ufaulu wa juu hadi Daraja la Kwanza.
 Vijana wa Sekondari ya Zimanimoto c tu wanafanya vizuri katika Masomo Pia wana vipaji vya Sanaa Kama ya muziki na Mpira wa Miguu. Hapo wakifutilia Burudani ya Muziki ambayo vijana wenzao walikuwa wakitumbuiza Shuleni hapo wakati wa Ghafla ya kukabidhi zawadi kwa vijana waliofaulu.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari Zimanimoto Manispaa ya Songea Kandindus Kowero amesema pamoja na Shule yake kukabiliwa na changamoto mbalimbali lakini imefanya vizuri katika Mtihani wa kuhitimu kidato cha nne 2014 vijana 9 wamechaguliwa kwenda kidato cha tano kati yao 7 wakiwa wamepata daraja la tatu na 2 daraja la Pili.


 Vijana wa Shule ya Sekondari Zimanimoto wakiwa katika Nyuso za Furaha kwa Kitendo kilichofanywa na Benki ya Posta kwa kuthamini shule za kata na Kuzipa kipaumbele cha kutoa Motisha kwa wanafunzi wanaofanya Vizuri katika Masomo. Wameomba Mashirika na taasisi Zingine kuiga Mfano wa Benki ya posta Tawi la Songea.
 Hapo wanafunzi wakifuatilia kwa makini Nasaha za Mgeni Rasmi Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Songea Joseph Shirima.
 Wanafunzi wa Sekondari Zimanimoto Manispaa ya Songea wakishuhudia Wenzao wanavyopokea zawadi kutokana na kujituma.
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Zimanimoto wakitafakari kuipigania Zawadi ya laki Tatu na Laki Tano baada ya Kufaulu.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari Zimanimoto Kandindus Kowero akifurahia Matunda ya Vijana wake waliotunukiwa kitita cha Sh Laki tatu kila mmoja kutokana na Kufaulu ufaulu wa Daraja la Pili, ameishukuru Benki ya Posta kwa kuunga Mkoano jitihada za Walimu na Wazazi katika kuhamasisha Ufaulu kwa Vijana. Amesema Shule ina changamoto ya Kukosa Hosteli ambayo iko umbali wa Km 15 ambapo wanafunzi hutembea umbali mrefu kufika Shuleni.
 Vijana Hafidhi Omary Kushoto na Joseph K,apinga waliofaulu ufaulu wa Daraja la II katika Shule ya Sekondari Zimanimoto na kuudhirishia Umma kuwa Shule za kata nazo ni sehemu ya kusoma na sio kupoteza muda, wao wamejituma na wameweza Matokeo yao yamekuwa mazuri.
 Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Songea Joseph Shirima Akifurahi kutekeleza Ahadi kwa Vijana Hafidhiomary n na Joseph  Kapinga waliopata Ufaulu wa Division Two. Amesema Shule za Kata si za Kuzibeza kinachotakiwa ni vijana kuwa na Bidii na kujituma katika Masomo Ufaulu utapatikana Popote.
 Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Songea Joseph Shirima akifurahia kuona faida wanayoipata katika Benki yake inarudi kuwasaidia Vijana katika kutoa hamasa ya kupenda Elimu. Hapo akiwa katika Shule ya Sekondari Zimanimoto iliyopo Manispaa ya Songea muda Mfupi kabla ya Kukabidhi zawadi ya Sh. Laki Sita kwa Vijana wawili ikiwa ni utekelezaji wa Ahadi aliyoitoa wakati wa Mahafali 2014 Shuleni hapo.
 Kijana Joseph Kapinga aliyehitimu 2014 katika Shule ya Sekondari Zimanimoto akitafakari kwa nini Benki ya Posta imeona ni muhimu kuwachangia pesa ya kuanzia kupata Mahitaji ya kwenda Kidato cha Tano. Amesema Lakitatu aliyopewa ba Benki ya Posta kwa ke si ndogo kwani yeye anaishi na mzazi mmoja hivyo pesa hivyo itamwezesha kupata mahitaji ya Shule amewaasa wanafunzi kujisomea kwa bidii hakuna linaloshindikana ufaulu hauji kwa miujiza.
 Meneja wa Benki ya posta Tawi la Songea Joseph Shirima akitoa Nasaha kwa Vijana wanaoendelea na Masomo kutia juhudi katika Masomo yao kwa kujali kilichowaleta Shuleni na kuwa yeye ataendelea kuwa sambamba na wale wenye moyo wa kujituma. Nyuma ni Waalimu wa Shule ya Sekondari Zimanimoto.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Zimanimoto Mwalimu Kowero akiratibu namna ya kuendesha Ghafla fupi ya Kuwakabidhi zawadi vijana wake Hafidhi Omary na Joseph Kapinga waliohitimu kidato cha Nne 2014 Shuleni hapo.
 Meneja wa Benki ya posta Tawi la Songea Joseph Shirima akiwa na Afisa Mahusiano wa Benki hiyo wakiwa Ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Zimanimoto mara Baada ya kuwasili Shuleni hapo tayari kwa kutekeleza Ahadi yake aliyoitoa katika Mahafali  ya 2014 ya kuwazawadia wanafunzi watakaofaulu daraja la kwanza na la pili.

 Waandishi wa Habari wakijadili jitihada zinazofanywa na Benki ya Posta Tawi la Songea katika kuchangia Maendeleo kwa Wananchi.
 Afisa Mahusiano wa Benki ya posta Tawi la Songea akitafakari jinsi ya kufikisha huduma hii ya kutoa Hamasa ya Elimu kwa Vijana wanaosoma katika Mkoa wa Ruvuma ili Elimu iweze kuwa na tija kwa wanafunzi kupenda kujituma katika Masomo.
 Waalimu wa Shule ya Sekondari Zimanimoto wakiwa katika ghafla fupi ya kukabidhiwa zawadi kwa vijana wao waliopata ufaulu wa Daraja la Pili kutoka Shuleni hapo.
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Zimanimoto wakiwa na Shauku ya kupata zawadi kama wanavyoshudia kwa wenzao wawili waliojipatia shilingi laki laki tatu kila mmoja kutokana na juhudi zao katika masomo.
 Baadhi ya Wanafunzi wa Sekondari ya Zimanimoto wakiwa katika Viwanja vya Shule hiyo iliyopo Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Zimanimoto Manispaa ya Songea wakipokea Nasaha za meneja wa Benki ya Posta alipotembelea Shuleni hapo kwa ajili ya Kutekeleza Ahadi ya kuwatunuku Vijana waliofaulu Mtihani wa Kidato cha Nne 2014.

No comments:

Post a Comment