KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, July 1, 2016

HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA I MEKAMILISHA ZOEZI LA UTENGENEZAJI WA MADAWATI KWA ASILIMIA 99 KUTOKA UPUNGUFU WA MADAWATI 13,013 HADI KUFIKIA 301 AMBAYO YATAKAMILIKA MWEZI JULAY MWAKA HUU.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Rajabu Mtiula amesema kwa kiasi kikubwa wadau mbalimbali wameweza kuchangia kukabiliana na upungufu wa madawati kati ya watu waliochangia ni pamoja na Mbunge wa jimbo la peramiho Jenista Mhagama pamoja na Madiwani ambao wamechangia Madawati 60.


Halmashauri nya Wilaya ya Songea yenye wanafunzi 28,045 kwa Shule za msingi na wanafunzi 3706  wa Shule za Sekondari imeweza kukabiliana na upungufu wa Madawati Madawati 13,013 yanayohitajika hadi kubakiwa na upungufu wa Madawati 301.


Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Weniselia Swai,  amewashukuru wadau wote waliowezesha kufanikisha zoezi la Madawati katika Halmashauri  Songea vijijini.


Afisa Elimu Shule za Msingi Tanu Kameka ameelezea jinsi ya upungufu wa Madawati ulivyo na kuweka  Mikakati ya kukamilisha upungufu huo hadi kufikia mwezi wa 7 mwaka huu.kuta kuwa hakuna upungufu tena


Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini ambayo imebakiwa na upungufu wa Madawati 301 katika Bajeti yake ya 2016/2017 imetenga shilingi milioni35 ili kumaliza tatizo la upungufu wa Madawati.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Juma Ally amesema juhudi za Serikali pamoja na wananchi zime weza kufanikisha kutatua tatizo la Madawati. Kazi kubwa kwa wanafunzi ni kuhakikisha wanasoma kwa bidii ili waje walete maendeleo katika Jamii.

No comments:

Post a Comment