KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, September 4, 2017

MKUU WA MKOA WA RUVUMA AITAKA AVIV KUJENGA KIWANDA CHA KAHAWA RUVUMA

 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Dr Binilith Satano Mahenge, akipokea tarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Shamba la Aviv

Mkurugenzi wa AVIV Meda Medppa amesema anaishukuru kuona wananchi wanao zunguka kampuni wanalima kahawa na kwa mwaka huvuna tani 20,000 nakulipwa kwa kilo shilingi 3500


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Satano  Mahenge amesema ili kuongeza ajira katika Mkoa wa Ruvuma pamoja na  Kampuni ya AVIVI   kuajiri wafanyakazi 1800 swala hilo halitoshi . jambo la msingi ni kuhakikisha kampuni ya Avivi ina jenga kiwanda cha kusindika kahawa mkoani Ruvuma ili kutangaza jina la Tanzania pale itakapo onekana lebo ya kahawa  ya mkoa waruvuma


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Mahenge ameitaka Kampuni ya AVIVI  inayofanya shughuli za Kilimo cha Kahawa wakiwa wana  miliki shamba lenye ukubwa wa hekita 1900  ambapo kwa mwaka huvuna tani 1200 wanauwezo wa kujenga kiwanda cha kusindika kahawa jambo litakalo weza kuifahamisha Ruvuma Ijulikane  kwa kuweka lebo ya  usindikaji kahawa kutoka  Mkoa wa Ruvuma


Shamba la Kahawa la Kampuni ya AVIVI linahudumia vijiji 19 vinavyozunguka shamba hilo ambapo mwaka jana wana kijiji waliweza kuuza Tani 20 za Kahawa na Wananchi 120 kupata Ajira kwenye Mtambo wa kukoboa Kahawa.

 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Mahenge akikagua utendaji wa kiwanda cha kukoboa kahawa kikiwa na uwezo wa kukoboa tani mbili kwa siku

Afisa Uhusiano wa Kampuni ya AVIVI Frola Hauko  amewaomba wananchi wanaozunguka Shamba la AVIVI kuchangamkia fursa za kuweza kulima Kahawa kwa kuwa Soko lipo. Naye Bwana shamba wa Shamba la Kahawa Hamuza Kasimu  amesema Shammba la Kahawa la Kampuni ya AVIVI mwaka huu lina tarajia kuvuna tani 1200

 Mkurugenzi wa Aviv akimtembeza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Satano Mahenge katika kiwanda cha kukoboa Kahawa Eneo la Lipokela
                Mmoja wa Viongozi katika shamba la kahawa la Aviv katika eneo la Lipokela
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akionyehswa kahawa inayo zalishwa na Kampuni ya Aviv
 Eneo la kusafisha kahawa katika kiwanda cha kukoboa kahawa
W3atalamu wa ufungaji umeme wakitoa Tarifa ya kutekeleza kauri ya Waziri Mkuu ya kutoa Umeme katika Kampuni ya Aviv

No comments:

Post a Comment