KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, June 28, 2016

MAFANIKIO YA MKOA WA RUVUMA NA SAID THABIT MWAMBUNGU AKIWA MKUU WA MKOA


Mabadiliko ya Ukuu wa Mkoa na Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya Luckness Adrian Amlima, Cosmas Nyano Nshenye, Isabera Octava Chilumba, Juma Homera na Polet Kamando Mgema umepokelewaje Mkoani Ruvuma.
Mkoa wa Ruvuma katika Miaka ambayo ametawala Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu umekuwaje,  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu katika utawala wake Mkoani Ruvuma ameweza kuunganisha Uhusiano mwema na Nchi jirani ya Msumbiji  na Tanzania na Nchi ya Malawi na Tanzania upande wa Wilaya ya Nyasa na wilaya ya Songea na Tunduru katika Mipaka ya Mkenda Muhukuru na Tunduru Tunduru Mpakani mwa Msumbiji.

 Mkuu wa mkoa Said Thabit Mwambungu alisimamia kikamilifu swala la marndeleo hata ulipo fika mwenge uliweza kufungua miradi kadha ya maendeleo

Katika Sekta ya Elimu ameweza kuinua kiwango cha Elimu kwa upande wa Shule za Msingi na Sekondari  kupunguza upatikanaji wa mimba kwa wanafunzi kutoka asilimia 60% hadi  asilimia 15%
Kuongezeka kwa uandikishaji wa watoto wenye umri wa kwenda shule  kuanzia awali hadi elimu ya msingi kutoka asilimia 40% hadi kufikia asilimia 90% na kufanya ongezeko la watoto wanaoandikishwa kuanza shule kuwa kubwa.

 Katika swala la usafi alisimamia kikamilifu hadi mkoa kila uendako kuna pendeza siyo kwa Songea pekee yake bali ni wilaya zote za mkoa wa Ruvuma. Tuta kukumbuka Mkuu kwa kazi ulizo fanya kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma tuna kutakia kazi mpya katika ofisi ya Waziri Mkuu

Katika Sekta ya Elimu ameweza kuinua kiwango cha Elimu kwa upande wa Shule za Msingi na Sekondari  kupunguza upatikanaji wa mimba kwa wanafunzi kutoka asilimia 60% hadi  asilimia 15%
Kuongezeka kwa uandikishaji wa watoto wenye umri wa kwenda shule  kuanzia awali hadi elimu ya msingi kutoka asilimia 40% hadi kufikia asilimia 90% na kufanya ongezeko la watoto wanaoandikishwa kuanza shule kuwa kubwa.


Sasa kazi ilikuwa katika kusimamia suala la Usafi, Utengenezaji wa Madawati, Kuimarisha Vyama vya ushirika kupitia Saccos  kwa Wananchi ili kuinua Uchumi wa kati lakini kutakana na Uhamisho wake tunategemea Mkuu wa Mkoa Mpya Mh Mahenge kuendeleza maendeleo katika Mkoa wa Ruvuma.


Kwa upande wa Afya Mwambungu ameweza kusimamia upatikanaji wa huduma nzuri za afya na kupunguza vifo  vya mama na motto kutoka watoto  .


Mkuu wa Mkoa kuna mambo mengi ambayo sijayaainisha lakini hayo machache ndiyo yaliyo jicho la wananchi katika Mkoa wa Ruvuma ikiwa utafanikiwa kuangalia hayo utaweza kusonga mbele. Pia jambo la muhimu ni kuwa na umoja na ufungamano na vyombo vya habari katika kuutangaza Mkoa wa Ruvuma.


Kwa Upande wa Uchumi Mkuu wa Mkoa Mwambungu Aliweza kuinua Sekta ya Kilimo kwa kuongeza uzalishaji wa mazao kutoka Tani 400,000 kwa Mwaka 2010 hadi kufikia Tani 1,480,000  ikiwa na maana ya kila Mwananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuwa na ziada ya Tani moja ya chakula.


Tukiingia wilaya ya Namtumbo kuna Madini ya Urenium, Mbuga za Seluu,  Kilimo cha Tumbaku pamoja na Kilimo cha Mahindi.


Tukiwa wilaya ya Tunduru tuna madini ya Vito ambayo yanapatikana  Muwesi na maeneo mengine  pamoja na Kilimo cha Korosho na Mpunga.


Aidha Wakuu wa Wilaya zote 5  za Mkoa wa Ruvuma  wamefanya kazi kubwa bila kumsahau Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya , Ukifika wilaya ya Songea zao kuu la biashara kwa wananchi katika kukuza uchumi ni Mahindi, Mazao mengine ni Kahawa, Maharage , Mpunga pamoja na mazao ya misitu ambayo ni mbao katika Milima ya Matogoro.


Mh Mkuu wa mkoa Mpya wa Ruvuma Binilith Saatano Mahenge kazi kubwa kwako ni kuinua uchumi wa mwana Ruvuma, Mkoa wa Ruvuma una Vipaumbele vya Uchumi vifuatavyo;


Wilaya ya Nyasa yako maeneo ya Utalii kama Milima ya Living Stone, Ziwa Nyasa Ufukwe wa Ziwa nyasa, Visiwa vya Pomonda na Samaki wa Mapambo wanaopatikana Ziwa Nyasa. Katika kilimo kunahitaji kuendeleza Zao la Korosho Mawese pamoja na minazi , Kilimo cha umwagiliaji na kuboresha Bandari ya mbamba Bay na uzalishaji wa Samaki na Dagaa.

hiki ni kisiwa cha pomonda ambacho kipo liuli katika wilaya ya nyasa ni kisiwa ambacho kilikuwa kikitumika kwa ajili ya watu kujificha vita ya kwanza ya dunia kilikuwa na uwezo wa kuhifadhi watu 250 wakiwa ndani ya pango, ugunduzi wa kisiwa hiki ni matokeo ya utawala wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu. Miti inayo onekana ina zaidi ya karine moja kiwa na maana ya miaka mia moja na miti hiyo iko juu ya mawe

Pia kuna Masuala ya Utalii katika Bonde la Agati pia mbuga za Seluu Mitomoni mpakani mwa msumbiji, pamoja na kuinua zao la Kahawa ambalo ni kiungo kikubwa cha uchumi katika wilaya ya Mbinga.  


Tukiingia Wilaya ya Mbinga tuna vyanzo vingi vya Mapato, kwa upande wa Madini kuna makaa ya Mawe yanayopatikana Rwanda, pia kuna Madini ya Vito na Zeebaki yanayopatikana eneo la Dar Pori.

 Aliye kuwa mkuu wa wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga akifungua mtambo wa mawasiliano eneo la Mhukuru karibu na mpaka wa msumbiji tuta wakumbuka kwa utendaji mzuri wa kazi
 katika utawala wa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu alijitahidi kuhakikisha shule zote zilizopo mkoa wa Ruvuma kuanzia Shule za awali mpa Sekondari watoto wana kaa ka
tika Madawati, Mkuu wa wilaya ya Songea akiwa msitari wa mbele katika kutengeneza Madawati hapo ana pakua mbao zilizo tolewa na wafanya biashara  Mkuu wa wilaya Beson Mpesya ni huyo aliye vaa sweta ya njano

Mkuu wa Mkoa kuna mambo mengi ambayo sijayaainisha lakini hayo machache ndiyo yaliyo jicho la wananchi katika Mkoa wa Ruvuma ikiwa utafanikiwa kuangalia hayo utaweza kusonga mbele. Pia jambo la muhimu ni kuwa na umoja na ufungamano na vyombo vya habari katika kuutangaza Mkoa wa Ruvuma.

No comments:

Post a Comment