KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, September 17, 2016

KAMPUNI YA FREEDOM INAYO SAMBAZA VIFAA NYA NYUMBANI YA TOA MSAADA KWA SHULE YA MSINGI LITISHA VIFAA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 2.5

 Shule ya Msingi Litisha iliyoko Songea Vijijini ilianzishwa Mwaka Mmoja baada ya kupata Uhuru wa Nchi ya Tanzania mwaka 1962 Mpaka sasa imefanikiwa kufanya maafali ya darasa la saba kwa kutoa wanafunzi 2160 kwa maafali  ya 48
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Freedom Martias Zacharia amewaomba wadau wengine wa Elimu kuwekeza katika Elimu kwa kutoa misaada itakayo weza kumjengea maisha mazuri Mwanafunzi wa Elimu ya Msingi ili elimu anayotoka nayo imsaidie katika maisha 
 Katika maafali ya 48, kijiji cha Litisha Mkurugenzi wa Freedom Martias Zacharia akiwa na Mwalimu mkuu wa Shule ya Litisha Andrew Mapunda kulia kwa mgeni rasmi.
Mkurugenzi wa Freedom alisisitiza wanafunzi kwenda shule akitoa mfano amesema yeye Mwenyewe ametokea katika shule hiyo hadi akawa na maendeleo hivyo anajua changamoto za shule hiyo wale wote walionufaika na shule hiyo inawapasa kurudisha fadhila kwa kuwasaidia wanafunzi waliopo, hapo Martias Zacharia alisoma shule ya msingi Litisha  miaka ya 1984 - 1986 na baadaye alihama shule.
 Kibao ni nembo muhimu ya kutambulisha taasisi jambo ambalo wengi huona kama ni mali ya wanafunzi au walimu.Kuimarisha Vielelezo ni njia moja wapo ya kufahamisha historia ya maendeleo ya kitu au jambo kwa jamii.
 Shule ina Manjonjo yake, Kwanza ukiwa msafi inakupa hamu ya kupenda kusoma hebu ona wanafunzi hawa walivyopendeza huwezi kujua kama wako vijijini. Mkamilishe mtoto wako kwa kumpa mahitaji ya msingi katika kujifunza ili kumpa hamasa ya kusoma kwa bidii na kupenda kujifunza kuanzia viatu,sare za shule daftari peni na vitabu pia bila kusahau chakula cha shule.
 Wahitimu 56 wa Darasa la saba shule ya Msingi Litisha Songea vijijini wakifurahia kufikia darasa la saba na kuomba wazazi wawaandalie mahitaji ya Elimu ya Sekondari.
 Wahitimu wa darasa la saba wakisoma risala kwa mgeni rasmi wa maafali ya 48 ya Shule ya Msingi Litisha wameiomba Serikali kuwasaidia upatikanaji wa maji shuleni hapo ili waepukane na adha ya kutafuta maji umbali mrefu.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Biashara ya FREEDOM SHOPING CENTER Songea Martias Zacharia ameomba wafanya biashara wengine wakubwa kushirikiana na Serikali katika kuwekeza kwenye Elimu, Amesema yeye anatambua umuhimu wa Elimu ya Msingi aliyoipata kwa ufasaha na kumwezesha kufanya Biashara kwa ufasaha na kuchangia pato la taifa kupitia kodi.
 Kulia ni Mkurugenzi wa FREEDOM Martias Zacharia akiwa na Mwenyeji wake Andrew Mapunda Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Litisha katika Maafali ya Darasa la saba.
 Waalimu wa Shule ya Msingi Litisha wakiwa katika maafali hayo wamemshukuru mgeni rasmi kwa kuweza kutambua changamoto zinazozikabili shule za msingi katika ufundishaji kwa kutoa vitendea kazi ambavyo vitarahisisha utendaji kazi.
 Wananchi waliohudhuria katika Maafali ya 48 Shuleni hapo wamesema hii ni maafali ya kihistoria kwao kwa kitendo kilichofanywa na Mkurugenzi wa FREEDOM mfanyabiashara mkubwa kuwekeza katika shule za Vijijini.
 Mratibu Elimu Kata ya Litisha Erick Kifaru amewataka Wazazi kujua kuwa watoto wanaomaliza bado ni wanafunzi wanahitaji kuandaliwa mahitaji ya kuendelea na Elimu ya msingi, haitarajiwi kusikia mzazi amepokea mahari au kuidhinisha mtoto wa darasa la saba kuoa au kuelewa hilo ni kosa kisheria na yeyote atakayewaza hilo sheria itachukua mkondo wake.
 Mkurugenzi wa FREEDOM Martia Zacharia akifurahia kutimiza azima yake ya kutoa sehemu ya mapato yake katika kuchangia Elimu kwa watoto wa Tanzania.
 Mkurugenzi wa FREEDOM Martias Zacharia amewaomba waalimu na wazazi wa shule ya Msingi Litisha Peramiho Songea Vijijini kutobadilisha matumizi ya vitu alivyovitoa, amesema vifaa vimetolewa kwa ajili ya wanafunzi vitumike kwa wanafunzi na vihifadhiwe shuleni isitokee Jezi alitoa kwa ajili ya wanafunzi zikaenda kutumika kwa watu wazima timu za  wakubwa, vivo hivyo kwa makabati, laptop na mipira.
 Wananchi wamesema kwa hali aliyoionyesha Mdau wa Elimu Mkurugenzi wa FREEDOM SHOP watashirikiana katika kuhakikisha watoto wao wanaendelea na masomo ili nao waje wafuate mfano wa Mkurugenzi wa FREEDOM hata kama watashindwa kupata Ajira ya Serikalini.
 Wageni waalikwa wa maafali ya 48 ya kuhitimu darasa la saba shule ya Msingi Litisha, kutoka kulia ni Afisa Mtendaji wa kata ya Litisha, Mratibu Elimu Kata ya Litisha, Shekhe wa Kijiji na kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Litisha.
 Pamoja na nasaha za mgeni rasmi na utoaji wa zawadi shuleni hapo pia aliweza kutoa Vyeti vya kuhitimu Elimu ya Msingi kwa wanafunzi 56 waliohitimu darasa la Saba 2016.
 Wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi shule ya Litisha walianza darasa la kwanza mwaka 2010 wakiwa wanafunzi 65 na leo wamehitimu wakiwa 56.
 Wanafunzi 9 kati ya 65 walioanza darasa la kwanza 2010 walipungua kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro, kuhama shule na ugonjwa.
 Kijana wa Darasa la saba akipokea cheti kwa mgeni rasmi Mkurugenzi wa FREEDOM ikiwa ni uthibitisho kwake kuwa amehitimu Elimu ya Darasa la Saba.
 Wahitimu wakiendelea na zoezi la kupokea vyeti kutoka kwa mgeni rasmi wa maafali ya 48 shule ya Msingi Litisha Bw. Martias Zacharia mkurugenzi wa FREEDOM SHOPING CENTER iliyopo Mjini Songea Mkoani Ruvuma.
 Kukabidhiwa mkono wa hongera kwa kuhitimu salama.
 Mkurugenzi wa FREEDOM SHOPING CENTER Martias Zacharia aliweza kupiga picha na wahitimu na wazazi mbalimbali ikiwa ni ishara ya kuboresha mahusiano na umoja katika uendelezaji wa masuala ya Elimu.
 Katika Maafali hayo Mkurugenzi wa FREEDOM Martias Zacharia ambaye ni mfanya biashara wa Fenicha za ndani na neti na mablanket aliweza kukabidhi zawadi za chaki , mipira, rim za karatas, peni, spika ya Amplifayer, Filimbi na Jezi za michezo kwa mpira wa mikono na mpira wa miguu.
 Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa FREEDOM akikabidhi Spika kwa mwalimu mkuu na kuonyesha namna inavyofanya kazi amesema spika itawasaidia kutangaza matangazo mbalimbali kwa wanafunzi ili kuleta usikivu.
 Hapo akionyesha aina ya Jezi za Mpira wa miguu kwa wanafunzi wa kiume amesema michezo inahitaji kuwa nadhifu kwa kuvaa sare ili kuleta hamasa kwa wachezaji kucheza kwa malengo ya kuona mchezo ni sehemu ya ajira.
 Wageni waalikwa katika maafali ya mwaka 2016 shule ya Msingi litisha Tarafa ya Peramiho Songea Vijijini.
Maandamano ya pam,oja kuelekea eneo la sherehe ya maafali wahitimu waalimu na mgeni rasmi wa maafali hayo Mkurugenzi wa FREEDOM SHOPING CENTER.

No comments:

Post a Comment