KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, December 19, 2016

CHAMA CHA AKIBA SACOS YA WALIMU MANISPAA YA SONGEA YAPATA FAIDA YA SH MILION 14 KTK KIPINDI CHA JAN HAD OKTOBER 2016



Wanachama wa Sacoss ya Walimu Manispaa ya Songea yenye Wanachama 320 imeweza kuwakopesha wanachama kiasi cha Shilingi Bilioni 3,931,780,000/


Mwenyekiti wa Sacoss ya Walimu Manispaa ya Songea Antony Mahundi amesema Saccos ya Walimu imeweza kupata faida kutokana na Wanachama wake kukopa na kurudisha mikopo kwa wakati. Jumla ya Shilingi Milioni 14 na laki 6 imepatikana na kuweza kuendesha Mkutano Mkuu bila kukopa mahali


Mgeni rasmi Godrey Majuto akimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea katika mkutano huo wa chama cha kuweka na kukopa cha manispaa ya songea amewataka viongozi kutoa elimu kwa wanachama wapya ili kuongeza Idadi ya wanachama na huduma za kiuchumi ambazo zitawawezesha kujikwamua katika masuala mbalimbali ya maendeleo.



Mwenyekiti wa Chama cha Akiba na Mikopo Sacos ya Walimu wa Manispaa ya Songea Antony Mahundi amesema katik kutafuta washindi waliongoza kurejesha mikopo kwa wakati jumla ya wanachama 7 waliweza kurejesha mikopo kwa wakati ambao walishindanishwa na kupatikana washindi watatu walifanya vizuri zaidi.



Katibu wa Chama cha kuweka na kukopa cha walimu wa Manispaa ya Songea Gebhard Nyoni akielezea hali ya mapato na matumizi yaliyopatikana katika chama hicho kwa mwaka 2016  amesema katika kipindi  cha January hadi Oktoba Chama kimeweza kukusanya kiasi cha Tsh. 60,886,811.38 na kutumia kiasi cha shilingi 46,642,959.10



Amesema Makusanyo hayo yamepatikana kutokana na faida ya mikopo shilingi 46,684,692.64, viingilio vya Wanachama 100,000.00,makusanyo toka uwekezaji Tsh, 13,816,800.00 na Mapato mengine ikiwa ni Tsh 285,318.00.



Wanachama waliokopeshwa na kuweza kurudisha kwa wakati ambao walioshindanishwa na kushinda 3 wamesema mikopo imeweza kuwasaidia kusomesha watoto hadi chuo kikuu . Sacoss ya Walimu wa Manispaa ya Songea pia imeweza kutoa rambirambi kwa wafiwa kiasi cha shilingi Milioni 6,300,000 kati ya shilingi  24,678,328.50 zilizotengwa.

No comments:

Post a Comment