KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, December 24, 2016

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AKIWA ZIARA WILAYANI NYASA MKOA WA RUVUMA



Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Medard Kalemani amesema nyumba nyingi zinazoungua kwa ajili ya Umeme ni makosa yanayotumika kwa kutumia  Mafundi Vishoka, kutandaza nyaya za umeme pasipo na ujuzi.

Mkurugenzi wa TANESCO Kanda ya Kusini Joyce Ngahyoma akiwa katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Ruvuma


Naibu Waziri amewaomba Wananchi kuacha kutumia Mafundi umeme wasio na sifa, wakandarasi wote wanaohusika na ufungaji  umeme majina yao yabandikwe katika mbao za matangazo ili mwananchi aweze kujua fundi kamili ni nani.



Naibu Waziri wa Nishati na Madini akiwa ziara wilayani Nyasa amewaambia wananchi wa wilaya ya Nysa kuwa  REA awamu ya tatu inaanza kwa kasi ambapo vijiji vyote ambavyo havina umeme vinatakiwa kufungiwa umeme ikiwemo na vijiji vya wilaya ya Nyasa.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Medard Kalemani  amesema ili kuharakisha zoezi la kufunga umeme linafanyika kwa wakati Viongozi wa TANESCO wanatakiwa kuweka vituo katika Kata  na vijiji ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kurahisisha kupokea malipo kwa wateja wanaounganishwa badala ya  wananchi kufuata huduma Mbamba Bay.



Wananchi wa mwambao wa ziwa nyasa wameishukuru Serikali kuleta umeme wa Rea wamesema itasaidia kupata mwanga vijijini pia katika biashara ya samaki na dagaa wanavuliwa Ziwa Nyasa wataweza kuhifadhi  katka majokofu na kusafirisha salama pindi wanapokwenda kuuza nje ya wilaya pamoja na  kukuza uchumi kwa kufanya shughuli zinazohitaji umeme.

Meneja wa TANESCO wilaya ya Nyasa akifuatilia kwa makini maelekezo ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini katika kutekeleza Mradi wa REA awamu ya tatu wilayani humo.


Afisa tawala wa wilaya ya nyasa Richard Mbambe akimweleza naibu waziri wa Nishati na Mdini amesema kati ya vijiji 94 vya wilaya ya nyasa ni vijiji 7 tu ndivyo vilivyo na umeme wa Rea hivyo juhudi zina takiwa kuvifikia vijiji vilivyo baki


Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr. Medard Kaleman amesema katika Mkoa wa Ruvuma watu ambao hawajafungiwa Umeme wa REA  wanafikia zaidi ya 3000 na ifikapo 2018 kila Kijiji kitakuwa umeme. Naibu waziri wa Nishati ametoa angalizo kwa kiongozi yeyote wa Shirika la TANESCO atakayeshindwa kumfuata Mwananchi basi atakuwa amejiondoa mwenyewe kazini

No comments:

Post a Comment