KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, December 28, 2016

VYOMBO VYA HABARI VYA SAIDIA KUWAKOMBOA WANANCHI KATIKA KUWADHULUMU WAJANE NA WAGANE KATIKA KUPATA HAKI ZAOMkuu wa Wilaya ya Makete Mkoani Njombe Veronica Kessi  amewaomba Wananchi ili kuepukana na dhuluma inayofanywa na Jamii kwa kupora Mali za wajane na wagane suluhu yake ni kushirikiana vitendo vinavyotoa Msaada wa Kisheria kwa Wananachi ambao hawana Elimu hiyo, Pamoja na kutoa habari zao za kudhulumiwa kwenye vyombo vya habari.

Mkuu wa Wilaya ya Makete ameyasema hayo baada ya Wagane na Wajane 80 kupata msaada wa kisheria na kuweza kurudishiwa mali walizoporwa.
Mkuu wa Wilaya ya Makete Veronica Kessi amesema wilaya ya Makete ina Kata 23 na katika Kata hizo kata 22 zina wasaidizi wa kisheria ambao wamekuwa msaada kwa wasiojua sheria wakishirikiana na vyombo vya habari  za kitaifa pamoja na vyombo vya wilaya ikiwemo  Green FM na Kituro FM

Mkuu wa wilaya ya Makete Veronica Kessi amesema anashukuru vyombo vya habari kwa kuwa wameweza kusaidiana na wananchi katika kupunguza migogoro mbalimbali inayowakabili wananchi kwa kutangaza  hatua zinazochukuliwa na Serikali baada ya kuona wajane na Wagane wakitaka kudhulumiwa mali zao.
Mkuu wa wilaya ya Makete amesema kuwa na wasaidizi wa kisheria kwa Kata 22 za wilaya ya Makete kumeleta mwanga kwa wasiojua sheria  kusaidiwa na kupata haki zao ikiwemo kurudishiwa mali zao.

Mkuu wa wilaya ya Makete Veronica Kessi amelipongeza Shirika lisilokuwa la kiserikali la PADI  likishirikiana na shirika la Msaada wa Kisheria SOPSE  kutoa Elimu kwa wasaidizi wa kisheria  na kuweza kufuzu vizuri katika utetezi huo, amesema wilaya itaendelea kusaidia Asasi zinazounga mkono shughuli za Maendeleo ikiwemo PADI

Mkurugenzi wa Shirika la PADI Iskaka Msigwa amesema wafadhili baada ya kuona PADI ilivyofanya vizuri katika mwaka mmoja uliopita wameongezewa ufadhili kwa miaka mi nne na kuongeza wigo wa utoaji huduma kutoka wilaya moja ya Makete hadi kufikia wilaya tano za Mkoa wa Njombe.

Mkurugenzi wa Shirika la PADI Iskaka Msigwa amesema vitendo vya kudhulumu wajane na wagane katika wilaya ya Makete vilikuwa vingi mno kiasi cha kuwaacha watoto waliofiwa na wazazi wote wawili kuishi kwa matatizo jambo lililosababisha ongezeko la watoto wanaoishi katika Mazingira hatarishi.
Shirika la PADI limeweza kufikisha Elimu kupitia vitengo vya kisheria na kuweza kusaidia watu 80 waliopatwa na majanga ya Mirathi, ndoa na masuala ya kumiliki Ardhi.

Mkurugenzi wa PADI ameomba pamoja na washauri wa kisheria wameweza kufanikiwa katika kazi hiyo lakini msaada wa vyombo vya habari kama inavyofanya Radio Free Africa , Green FM na Kitulo Fkujitolea kutangaza matukio yanayowapata Wagane na wajane kwa kutangaza bure, na vyombo vingine viige tabia hiyo.


Mkurugenzi  Mtendaji Halimashauri ya Makete Gregory Emanuel amesema katika kupata kituo hicho sasa suala la Maendeleo liko mbele kwani migogoro ya Ardhi sasa imepungua , kwa kiasi kikubwa sasa  wananchi wanashiriki kazi za Maendeleo. Migogoro inashughulikiwa na wasaidizi wa kisheria kwa njia ya upatanishi.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya ya Makete Felex Mbwiro  amesema kazi ya Afisa Maendeleo ni kuhakikisha hakuna Mwananchi anayekosa Maendeleo kwa ajili ya kunyanyaswa kwa kudhulumiwa mali zake, akiungwa mkono na Afisa Idara ya maji jinsi vitengo vya kisheria vinavyosaidia wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Makete Veronica Kessi amewaomba wananchi na Viongozi wa Serikali kutofumbia macho vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa wananchi kwa kudhulumiwa mali zao na familia za wajane na wagane baada ya mme au mke wa marehemu kufariki. Na kuwataka waache kudhulumu mali za familia ya marehemu aliyefariki badala yake wawe wasimamizi kuhakikisha hakuna anayeingia na kudhulumu mali hizo.


No comments:

Post a Comment