KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, November 3, 2017

BOMOA BOMOA YASITISHWA MKOANI RUVUMA

Wakurugenzi wa Halimashari sita za mkoa wa Ruvuma wakiwa katika ikulu ndogo mkoani Ruvuma kushuhudia makazibdhiiano kati ya mkuu wa mkoa anaye hamia Dodoma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge na Mkuu mpya wa Ruvuma  Mh,CistineMdeme
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma, Katibu wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma wakuu wa wilaya ya Songea na Tunduru na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa Mikoa wanaokabidhiana majukumu Dr Binilith Mahenge na Christine Mdeme nje ya Jengo la Ikulu ndogo Songea

Mkuu wa Mkoa mpya Christine Mdeme akipokea makabidhiano, mikakati miongozo na mipango ya utekelezaji kutoka kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma amesema kuna methali isemayo Mzigo mzito mpe mnyamwezi hivyo yeye yuko tayari  kwa mema na tabu amekuja kuwatumikia wana Ruvuma ili kuhakikisha malengo ya kuwaletea maendeleo wananchi yanafanikiwa.

Katika makabidhiano hayo Mkuu wa Mkoa Dr Mahenge alitumia wasaa huo kumjulisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kuwa Nyumba zilizo kando kando ya Barabara ya Songea Mbamba Bay zilizowekewa alama ya {X} kutaka kubomolewa na Wakala wa Barabara TANROADS zoezi hilo  la kubomoa limesitishwa na Serikali ya Mkoa wa Ruvuma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge ameyasema hayo wakati alipokuwa akimkabidhi Mkuu wa Mkoa mpya wa Ruvuma Christine Mdeme Mafanikio na changamoto ikiwemo ya bomoa bomoa kwa nyumba zilizo kando kando ya Barabara ya Songea Songea Mbamba Bay ikiwemo Ofisi za Hazina ndogo na Benki ya NMB.


Mkuu wa Mkoa anayehamia Mkoa wa Dodoma akieleza mafanikio yaliyopo ni pamoja na kiwanda cha Maziwa, kiwanda cha kusindika mahindi, shamba la kahawa, kiwanda cha uundaji wa Maboti ya kisasa ya uvuvi katika Ziwa Nyasa.




Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akimkabidhi vitendea kazi mkuu mpya wa mkoa wa Ruvuma ikiweme sheria za serekari ya mitaa na miongozo mbalimbali itakayo msaadia katika utendaji wake wa kazi

 Mkurugenzi wa Blog ya Songea Habari Adam Nindi akimpongeza kwa uteuzi mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na kumkaribisha mkoani Ruvuma huku akimsisitiza kuhakikisha anatekeleza majukumu yake kwa kusaidia wanyonge katika kutatua kero zao.
 Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma wameahidi kumpa Ushirikiano mkuu wa Mkoa wa Ruvuma katika kuhakikisha Ruvuma inavuma na inasonga mbele wamesema wanachoomba ni ushirikiano kutoka katika Ofisi yake katika shuguli mbalimbali za maendeleo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge akikabidhi Mkoa wa Ruvuma kwa Mkuu wa Mkoa Christine Mdeme amesema anawashukuru wana Ruvuma na Viongozi mbalimbali kwa ushirikiano mkubwa alioupata katika kipindi alichokuwa mkoani Ruvuma amewaomba Viongozi kumpa ushirikiano wa hali na mali kwa Mkuu wa Mkoa wa sasa.
 Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma wamemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa ushiririkiano mkubwa aliutoa kwao akiwa mkoani Ruvuma uliowafanya kutekeleza kwa uraisi majukumu yao wameahidi kushirikiana na Mkuu wa Mkoa mpya kama walivyofanya kwa Dr Mahenge.
 Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali wakiwa katika ukumbi wa Ikulu ndogo Songea katika hafla ya makabidhiano ya wakuu wa mikoa wa Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Songea wakifuatilia makabidhino ya wakuu wa mikoa Dr Binilith Satano Mahenge na Mkuu wa Mkoa Christine Mdeme.
Katikati ni mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Binilith Mahenge aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akiwa na Mrithi wake Mh Christine Mdeme , Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akiagana na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Ruvuma amesema atawakumbuka sana wana Ruvuma kwa ushirikiano pia amemuomba Mkuu wa Mkoa mpya kuendeleza mipango ambayo aliinza kuitekeleza katika kuinua uchumi wa wana Ruvuma  na kutatua kero mbalimbali katika sekta ya Kilimo na viwanda.

No comments:

Post a Comment