KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, March 1, 2018

GENERAL MABEYO KUMBUKIZI VITA VYA MAJIMAJI


Mkuu wa Majeshi Nchini Tanzania amewataka Watanzania kuwa na kitu cha kujivunia baada ya Maisha haya ya Dunia.
Mkuu wa Majeshi Nchini Tanzania  General Venance Mabeyo ameyasema hayo katika kumbukizi ya Mashujaa wa vita vya Majimaji iliyofanyika katika uwanja wa Mashujaa Mahenge, Mkuu wa Majeshi amesema tunapowakumbuka Mashujaa ni lazima tujue sisi tumefanya nini kwa Taifa letu lazima tujitoe kulinda Taifa letu.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amewaomba Wananchi na Jeshi la Wananchi Tanzania kuendelea kulinda Raia na kuendeleza Amani iliyopo Tanzania

Chifu wa wangoni chifu Emanuel  Zulu akishirikiana na Mzee wa Baraza la Machifu Yasini Mbano am muomba Mkuu wa Majeshi ili kuongeza Amani katika Mioyo wana Ruvuma wameomba  Rais Magufuli atembelee Mkoa wa Ruvuma.

 Mzee wa Baraza la Wazee kutoka Matimila Yasini Mbano akiwa akifuatiwa na Chifu Emanuel Zuru anaye fuatia Mkuu waMajeshi Nchini Jenelali Venance Mabeyo na wa Mwisho Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Cristine Mndeme
 Mzee Yasini Mbano akitoka kuweka Rungu kwenye Mnara wa kumbukumbu wa Vita vya Nduli Iddi Amini Dada wa Uganda


Pamoja na Tumbuizi za ngoma ya Asili pia kulikuwepo na sanaa za Vijana wa JKT Mlale ambao waliwakumbusha wananchi umuhimu wa kudumisha Amani tuliyonayo na kuwatii viongozi wetu  tuliowachagua.

 Kiongozi wa Dini ya Kristo akitoa Dua kwa kuwaombea Mashujaa walio kufa miaka 112 iliyo pita katika vita vya Majimaji
 Mkuu wa Majshi Nchini Tanzania akiweka shahada la Maua kwa Mashujaa 66 walio zikwa kwenye kaburi moja katika viwanja vya mahenge Manspaa ya Songea

Mkuu wa Majeshi Nchini Tanzania Jenerali Mabeyo  amehaidi kujenga Ukumbi wa Mikutano katika viwanja vya Makumbusho ya Majimaji vilivyopo Mahenge manispaa ya Songea. Insert

 Kutoka kulia Mzee wa Baraza la Wazee Yasini Mbano wapili kutoka kulia Chifu Emanuel Zulu na anaye fuatia ni Mkuu wa Majeshi Nchini Jenelali Venance Mabeyo

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Tanzania amesema Maombi ya kujenga Ukumbi wa Makumbusho ya Majimaji Jeshi litajenga pia kila Mwaka Jeshi litafanya Paredi ya kuwaenzi Mashujaa hao.

 Emanuel Zuru Chifu wa Kingoni katikati Mkuu wa Majeshi Venance Mabeyo na Mwisho Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Cristine Mndeme
Wageni waalikwa kutoka Malawi na Nchi jirani zinazopakana na Mkoa wa Ruvuma wameshukuru uhusiano wa kitamaduni kualikwa katika sherehe hii kubwa ya kukumbuka Mashujaa 66 walionyongwa wilayani Songea.

Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Nchini Tanzani Jeneral Venance Mabeyo amewataka watanzania kuenzi Mila na Utamaduni wa Mtanzania  ambao unaonyesha ni njia moja wapo  ya kuweza kuongeza Ajira kwa Vijana wa Taifa  Tanzania.
Mkuu wa Majeshi Nchini Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akikagua ngoma za asili katika sherehe za kumbukizi ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji vilivyopiganwa miaka 112 iliyopita amesema pamoja na kuenzi utamaduni huo lakini kupitia Ngoma za asili na michezo vitaweza kuongeza Ajira kwa Vijana.

No comments:

Post a Comment