KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, March 9, 2018

MAZOEZI YA VIUNGO ZIWANI NYASA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nyasa Dr Osca Mbyuzi amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kujitokeza kwa wingi kila juma mosi kufanya mazoezi ya ufukweni  mwa mwambao wa ziwa nyasa kwa kufanya michezo ya kuogelea, mpira wa miguu kukimbia ufukweni na michezo mingine

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya nyasa Dr  Osca Mbyuzi ameyasema hayo wakati watumishi mbalimbali wa wilaya ya Nyasa walipo shiriki michezo katika fukwe za Ziwa Nyasa  ikiwa ni sehemu ya kuboreesha Afya zao pamoja na kutii amri ya viongozi wa juu ya kutakiwa kufanya mazoezi kila  mwezi

Watumishi walio hudhuria katika mazoezi hayo ya michezo ya ufukweni wamesema licha ya kuboresha afya zao lakini michezo hiyo pia itaongeza uhusiano mzuri baina ya watumishi na wananchi
Nao  Walimu wamsema michezo ya ufukweni itaongeza ari kwa wanafunzi kuja shuleni wakivutiwa na mpira wamiguu  hasa baada ya kuona ushindani wao wanapo cheza mshindi  hupewa mbuzi ambaye huchinjwa hapo hapo na wanafunzi kufanya kitoewo baada ya ratiba za michezo.


Waalimu kutoka Shule ya Uburcant wanasema wanatumia michezo kama motisha ya kuwafanya wanafunzi wanaopenda michezo wapende shule na kutokana na kuandaa mashindano ya mbuzi cup ambayo mshindi hupata kitoweo hivyo hakuna mwana funzi anaye kosa michezoni

 watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Nyasa wakiwa na Wananchi katika Mazoezi ya Viungo kando kando mwa Ziwa Nyasa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nyasa Dr Mbyuzi amesema siku zijazo Halmashauri itaandaa zawadi za aina mbalimbali kwa washindi watakaoshinda michezo ya ufukweni, Aidha amewaomba wawekezaji mbalimbali kuwekeza katika michezo ya ufukweni kupitia fukwe nzuri za Mwambao wa Ziwa Nyasa.
 Mazoezi ni sehamu ya kuimarisha Afya na Akili ya Binadamu lakini yasipozingatiwa ipasavyo inakuwa ni ugonjwa, Pichani watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Nyasa wakinyoosha viungo.


Michezo ya ufukweni iliyo fanyika katika ziwa nyasa ili ambatana na michezo wa Mpira wa miguu wa ufukweni ,kufanya jogging,kukimbia mbio ndefu za ufukweni, kuogelea na zoezi la kukimbiza mtumbwi

 Miongoni mwa Michezo iliyofurahisha katika fukwe za ziwa Nyasa ni pamoja na mpira wa ufukweni ambao ulivutia watazamaji wengi.
Watumishi wa Halmashauri ya Nyasa wakisakata Boli la Ufukweni mubashara.

No comments:

Post a Comment