KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, March 19, 2018

NAIBU KATIBU MKUU UWT TAIFA BI EVA KIWELE AMEKEMEA SUALA LA MMOMONYOKO WA MAADILI KWA WATOTO PIA AMEPONGEZA HATUA ZINAZOENDELEA ZA UJENZI WA KITUO CHA AFYA NAMTUMBO KATIKA KUOKOA MAISHA YA MAMA NA MTOTO

Katika Ziara yake wilaya ya Namtumbo Iliyolenga kukagua shughuli za utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi na kuangalia Uhai wa Jumuia ya Wanawake wa CCM (UWT) Naibu Katibu Mkuu pia aliweza kupokea wanachama wapya na kuongea na viongozi wanachama wa Vyama vya Upinzani wapenda maendeleo kama anavyoonekana pichani akiongea na Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Eva Kiwele ameyasema hayo wakati alipotembelea Zahanati ya Libango na kuwafariji wagonjwa , Naibu katibu Mkuu amesema Ujenzi wa zahanati na Kituo cha Afya hii inaonyesha UWT inavyo  jaliwa  na serekari kwa kuwa huduma zitakazo tolewa  maternity na theata ni miongoni mwa mikakati ya kuokoa maisha ya Mama na Mtoto.

Mhandisi wa Ujenzi anayesimamia ujenzi wa Kituo cha Afya Namtumbo     ameeleza gharama zinazotarajia kutumika mpaka ujenzi huo  kukamilika, Katibu wa UWT wilaya ya Namtumbo Ana  Ndumbaro  amesema kufika kwa Naibu Katibu Mkuu kutasaidia kusukuma miradi  iliyopo

Mganga Mfawidhi wa Wilaya ya Namtumbo Aloyce  Mushi ameiomba Serikali kuweka msukumo wa Upatikanaji wa wataalamu wa Afya katika idara ya upasuaji pindi ujenzi wa Kituo cha Afya  cha Rwinga Namtumbo utakapokamilika. Jambo ambalo Naibu katibu mkuu amehaidi kulifikisha kwa Waziri wa Afya watumishi wapatikane haraka iwezekavyo ili huduma zianze kutolewa.
Wanachama wa Jumuiya ya Umoja wa akina Mama UWT Namtumbo wakifurahi na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo nje ya Ofisi za chama cha Mapinduzi wilaya ya Namtumbo.
Naibu katibu mkuu wa UWT Bi Eva kiwele amewaomba viongozi wa UWT kuhakikisha wanachama wao wanalipa Ada na kuwa wanachama hai kwa kuwa uhai wa Jumuia unatokana na wanachama kulipia kadi zao.
Katibu wa UWT wilaya ya Namtumbo Ana Ndumbaro akipokea maelekezo kutika kwa Naibu Katibu Mkuu ameahidi kutekeleza yale yote yaliyoelekezwa na kuhakikisha Jumuiya inakuwa Imara.
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa alihitimisha ziara yake kwa kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Piachani ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Bi Eva Kiwele akiwa na wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Mkoa wa Ruvuma na Katibu wa UWT wilaya ya Namtumbo Ana Ndumbaro
Katibu wa UWT wilaya ya Namtumbo akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Mkoa wa Ruvuma wakiwa nje ya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Namtumbo.
Huu ni Msimamo wa Utendaji kati wa wilaya ya Namtumbo.
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Bi Lackness Amlima akiwa na ugeni ulioambatana na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Bi Eva Kiwele walipotembelea Ofisini kwake.
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT mkoa wa Ruvuma kutoka kulia ni Katibu wa UWT wilaya ya Namtumbo Ana Ndumbaro, anayefuata ni Mjumbe kamati ya Utekelezaji kutoka wilaya ya Tunduru Bi Yunus, Anayefuata ni Mjumbe kutoka wilaya ya Songea Bi Yusta Mwarabu na wa mwisho kushoto ni Pendo Ngonyani mwakilishi kutoka Namtumbo.
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo akisagana na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Mama Eva Kiwele
Wajumbe wa UWT wakiwa katika picha ya Pamoja, kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Namtumbo Matha Nikata na kulia wa mwisho ni Katibu wa UWT wilaya ya Namtumbo Ana Ndumbaro, katikati ni wajumbe wa kamati ya utekelezaji mkoa waliokuwa wameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa UWT katika ziara yake ya siku tatu wilayani namtumbo.

Huu ndio msimamo wa Utendaji kazi wilaya ya Namtumbo
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Namtumbo Matha Maiko Nikata amemweleza Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya UWT Taifa mikakati ya wanawake wa UWT wilaya ya Namtumbo kuwa ni pamoja na kujenga Jengo la kitega uchumi la Ukumbi ambao amesema ukumbi huo watautunuku jina la Naibu Katibu Mkuu EVA Kiwele.
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Eva Kiwele amesema amesikitishwa baada ya kuona baadhi ya wanafunzi wakiwa wamevaa nguo zinazo ashiria ngono uzembe na wengine wakionyesha dalili za kuwa wajawazito na kuahidi hali hiyo ataifikisha kwa mheshiwa Rais amewaomba wazazi  washirikiane na serekari kukemea vitendo hivyo ili wanafunzi waepukane na mimba za utotoni

Wanawake wa wa Kata ya Luegu wamelalamikia ukosefu wa Maji safi ambayo imekua chanzo kikuu cha maradhi ingawa mabomba yalishasambazwa lakini maji hayapatikani na kupelekea magonjwa ya mlipuko kusambaa naKUSABABISHA  watoto wakike kubakwa wakati waKI tafuta maji .
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Eva Kiwele katika ziara yake wilayani Namtumbo alitembelea Zahanati ya Libango na kuwafariji wagonjwa , na kupongeza jitihada za Serikali za kusogeza huduma za afya karibu na wananchi amesema jwepo wa zahanati na Ujenzi wa  Kituo cha Afya Namtumbo ni faraja kwa akina mama hii inaonyesha dhahiri UWT ina jaliwa  na Seiekali kwa kuwa huduma zitakazotolewa  za Maternity na theater ni miongoni mwa utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi katika mikakati ya kuokoa maisha ya Mama na Mtoto.
Naibu katibu Mkuu wa UWT Taifa aliweza kutembelea eneo la mradi wa Uwanja wa UWT wilaya ya Namtumbo ambako wanatarajia kuwekeza katika Ujenzi wa Ukumbi wa mikutano katika kuinua uchumi wa Jumuiya.
Pamoja na kutembelea shughuli mbalimbali za maendeleo pia alisikiliza kero za wananchi katika kata ya Luegu na kufanikisha kutatua kero moja ya maji kwa kuendesha harambeed ya kuchangia fedha za kumalizia ujenzi wa mradi huo ili maji yapatikane.

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Namtumbo Matha Nikata ameunga mkono suala la watoto wa kike kupata ujauzito ni suala ambalo UWT wilaya ya Namtumbo itasimamia kutoa Elimu ili kumlinda motto wa kike na mimba za utotoni.

Mhandisi wa Ujenzi anayesimamia ujenzi wa Kituo cha Afya Namtumbo     ameeleza gharama zinazotarajia kutumika mpaka ujenzi huo  kukamilika, Katibu wa UWT wilaya ya Namtumbo Ana  Ndumbaro  amesema kufika kwa Naibu Katibu Mkuu kutasaidia kusukuma miradi  iliyopo
Aidha Naibu katibu Mkuu Eva Kiwele akiweza kuwaingiza wanachama wapya wa UWT wanafunzi wa Sekondari katika Kata ya Luegu
Wanafunzi waliojiunga na Jumuiya ya UWT Songea na kukabidhiwa kadi ya Jumuiya za uanachama wa UWT. Katika ziara hiyo pia Naibu katibu Mkuu hakuacha kuwaasa wanafunzi kuzingatia masomo na kujiepusha na kupenda vizawadi vidogo vidogo wakiwa shuleni kufanya hivyo ni kukaribisha kuvurugiwa mfumo wa maisha yao ya baadaye.

Wilaya za Namtumbo na Tunduru zimekuwa ni wilaya ambazo zinaoongoza kwa watoto wa kike kuolewa mapema kabla ya umri wao ambapo mikakati iliyowekwa na mkoa wa Ruvuma ni kuzingatia taratibu za kuvaa magauni manne kwa kila gauni na wakati wake  na kupiga marufuku kumuita motto wa kike Baby au mrembo mtiririko sahihi wa magauni ni Sare ya Shule ya Msingi, Sekondari na joho la chuo kikuu na kumalizia shela ya harusi.
Wilaya ya Namtumbo imekuwa na changamoto ya watoto walio chini ya miaka 15 kuwa na watoto wenzao kuwepo kwa zahanati na vituo vya Afya kutasaidia kuokoa Maisha ya Mama na Mtoto.  Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa amehitimisha Ziara yake kwa kukagua miradi ya UWT ikiwemo kiwanja cha kujenga ukumbi, Ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya na kupokea kero za wananchi.
Naibu katibu Mkuu akiwa ameshika kadi ya Mwanachama wa CUF aliyeamua kurudisha kadi na kujiunga na CCM. Ambapo akiwa kata ya Luegu aliweza kuingiza mwanachama mmoja na mwenyekiti wa Kitongoji kupitia chama cha CUF.
Katika kuwapokea wanachama hao Naibu katibu Mkuu alihamasisha ukarimu kwa wageni na kufanya harambee ya kuwapokea ambapo zilipatikana fedha kiasi ambazo walikabidhiwa wageni wakapate kitoeo ikiwa ni pongezi kwa kurudi nyumbani.
Naibu katibu Mkuu wa UWT Taifa amewapongeza waawake wa UWT wilaya ya Namtumbo amesema amefurahi sana kwa mapokezi yao mazuri na kuahidi kushirikiana nao katika maendeleo na kuwaasa kutumia zaidi mawasiliano katika kjazi taarifa ni muhimu ili kuondoa migongano na muingiliano katika utekelezaji wa majukumu yao.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu UVCCM wilaya ya Namtumbo Twaha akiongoza msafara wa Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa.
Hizi ni nyumba ambazo alifikia Naibu Katibu Mkuu katika Hoteli ya ZIRO Namtumbo zenye mandhari nzuri wa kuvutia
Nyumba bora za kulala zinazopatikana Hoteli ya ZIRO wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma
Nyumba ya kulala wageni inayovutia ambayo ni Self Contained.

Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa amewataka wanawake kuwa watekelezaji wa kusimamia Maadili badala ya kusimamia badala ya kugeuza Maadili kama wimbo huku Vijana wakiendelea kupata madhara yanayotokana na mmomonyoko wa maadili kama  vile kupata Mimba zisizotarajiwa.
Wanachama wa UWT wilaya ya Namtumbo wakimuonyesha Naibu katibu Mkuu Eneo litakalojengwa Ukumbi.

No comments:

Post a Comment