KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, June 2, 2023

ELIMU YA MLIPAKODI KWA WAFANYABIASHARA MADABA

 https://www.youtube.com/live/aDXyrrpF3zo?feature=share

ELIMU YA MLIPA KODI MADABA - RUVUMA

02/06/2023

 

Wafanya biashara wa Mkoa wa Ruvuma wameipongeza Mamlaka ya Mapato TRA kwa kutoa Elimu ya Mlipakodi mlango hadi Mlango na kusogeza huduma karibu za kodi hususani katika Halmashauri za Madaba na Wilaya ya Nyasa.

 

Wafanya biashara hao wameyasema hayo wakati Timu ya Maofisa wa TRA ilipotembelea Halmashauri ya Madaba kutoa elimu ya mlipakodi.

 

Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi kutoka Makao makuu ya Mamlaka ya Mapato TRA Lydia Shio amesema huduma ya mapato imesogezwa karibu na wafanya biashara ili kuwasaidia kupata huduma karibu na kupata uelewa jinsi ya kulipa kodi na jinsi wanavyokadiriwa mapato.

 

  Lydia Shio – Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi.

 

Wafanya biashara hao wa halmashauri ya Madaba Songea Vijijini wameipongeza Mamlaka ya TRA kwa kuwasogezea huduma za kikodi kwamba sasa watapata Maelekezo kamili ya jinsi ya kuweza kulipa kodi pamoja na jinsi ambavyo wao wataweza kujiendesha kibiashara.

 

                 1. Petro Ndiba – Mfanya Biashara Madaba

                 2. Salimu Seif – Mfanyabiashara wa halmashauri ya madaba

                 3. Ezekiel Mkombo – Mfanya Biashara

 

Mamlaka ya Mapato TRA imekua ikifanya juhudi za kuwasogeza wafanyabiashara ili waweze kupata manufaa kuhusiana na kodi wanazolipa na kuwaelimisha jinsi wanavyoweza kufanya biashara zao bila kuipunja Serikali wala kujipunja wao.

 


No comments:

Post a Comment