KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, June 7, 2023

WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI BRELA WATUA RUVUMA

Wakala wa Usajili wa biashara na Leseni (BRELA) wametoa elimu ya Biashara kwa njia ya mtandao kwa wananchi wapatao 700 wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Jimbo la Peramiho Mkoani Ruvuma ili kuwafanya wakulima  wanapofanya biashara za mazao yao waweze kuzirasimisha na kuuza katika mifumo yenye kuleta tija pasipo usumbufu wa kutafuta masoko.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mh Jenista Mhagama akiongea katika semina elekezi iliyotolewa na Brela amesema kila anapokaa amekua akifikiria jinsi ya kuwawezesha wananchi kiuchumi ili wapate maendeleo yenye tija pamoja na kuwaongezea nyenzo ambazo zitaweza kuwasaidi katika shughuli zao 

Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa BRELA Koyani Abubakari amesema ni wajibu wa BRELA kuwafundisha wananchi jinsi ya kusajili na kurasimisha biashara zao ili waweze kuendesha biashara zao kitaalamu kwa maendeleo yao.


Baadhi ya washiriki waliohudhuria katika semina iliyoendeshwa na BRELA katika ukumbi wa NJUNDE peramiho Songea Vijijini

Baadhi ya Mastafu wa BRELA walioendesha semina ya usajili wa biashara na Leseni
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Songea Simon Kapinga amesema elimu iliyotolewa kwa wananchi imesaidia kufahamu umuhimu wa kumiliki NEMBO katika biashara.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Menas Komba amewataka wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Songea kuzingatia mafunzo wanayoyapata ili yawasaidie kubadilisha hali ya uchumi kwa familia na kuongeza pato la serikali.

Wananchi waliohudhuria Mafunzo ya BRELA wamesema wamefurahi kuona BRELA  imetoa Elimu ya kuwawezesha kufanya usajili katika biashara zao pamoja na kuwafanya wapate leseni zitakazotumika katika biashara za Mazao ya kilimo pamoja na mambo mengine.

Semina iliyoendeshwa na wakala wa Usajili BRELA katika eneo la Peramiho Songea Vijijini imweza kuwanufaisha wananchi 700 kutoka kata zote za Halmashauri ya Songea Vijijini na kusema kutokana na mwanga walioupata utaweza kuwasaidia kuinua biashara zao na kuwa na kampuni zao.


 

No comments:

Post a Comment