KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, November 6, 2012 BENK YA POSTA MKOANI RUVUMA WAISAIDIA TIMU YA MAJIMAJI
Adam  Nindi, Songea.

Meneja wa Tawi la Benki ya Posta Mkoani Ruvuma Joseph Priscus Shirima ameweza kuichangia Timu ya Majimaji ya Mkoa wa Ruvuma ambayo iko katika ligi ya daraja kwanza ngazi ya Tifa kwa  kuipa Shilingi Laki Tano (500,000)

Meneja wa Posta Mkoa wa Ruvuma amesema Shirika la Posta linathamini sana michezo, Wateja wa Benki ya Posta walio wengi wanapenda michezo kama Benki haitawaunga mkono maswala ya michezo haita kuwa ina watendea vizuri wateja wake ambazo ni wanamichezo
.
 Meneja wa  Tawi la Benki ya Posta Mkoa wa Ruvuma Joseph Pricus Shirima  amesema mchango wa Shilingi 500,000 ni moja ya kuhamasisha Timu ya Majimaji iweze kufunya vizuri katika Ligi ya daraja la kwanza  Tanzania.
.
 Mwenyekiti wa FARU Mkoa wa Ruvuma Golden Sanga amewaomba wana Ruvuma kuziunga mkono Timu za Majimaji na JKT Mlale ili ziweze kufanya vizuri katika Ligi Daraja la Kwanza Tanzania. Pia ameshukuru msaada wa Shilingi 500,000 uliotolewa na Benki ya Posta Mkoa wa Ruvuma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Saisdia Majimaji Ruvuma Dadiely Chanachayo amesema Timu ya Majimaji ambayo iko Iringa kwa sasa imekwama kutokana na ukwasi, msaada wa Shilingi 500,000 uliotolewa na Benki ya Posta utasaidia Maimaji kuendelea na michuano ya Ligi Daraja la Kwanza na kuisaidia timu hiyo kwenda morogoro

Mwenyekiti wa Mchezo wa Mpira wa Miguu mkoani Ruvuma Golden Sanga kwa mara ya Kwanza toka achaguliwe baada ya kumwangusha mpinzani wake mkubwa Joseph Mapunda  ambaye alikuwa mwamuzi wa kimataifa  wa mpira wa miguu pia kuwa mjumbe wa TFF aliweza kumwangusha kwa kura mbili. Hivi sasa Mwenyekiti Godeni Sanga ana enda nyumba hadi nyumba kuomba mchango wa kuweza kuinua michezo mkoa wa Ruvuma

Wakati huohuo aliye kuwa mwenyekiti wa michezo mkoa wa ruvuma Joseph Mapunda amesma anaupongeza uongozi wa mpira wa miguu chiniya mwenyekiti Golden Sangawani na ameahidi kushirikiana na uongozi huo

No comments:

Post a Comment