KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, December 23, 2012

WANAUME WA MWAMBAO WA ZIWA NYASA WATOA LAWAMA YA KUNYANYASWA KWA KUNYIMWA UNYUMBA

 Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Prisca Haule akifafanua mambo yanayoashiria kutozingatia usawa wa kijinsia na kukwamishaMaendeleo huku akiwataka wananchi wa Wilaya ya Nyasa kuzingatia usawa wa Kijinsia.
 Washiriki wa Mdahalo juu ya Masuala ya Usawa wa Kijinsia katika Ukumbi wa Kapt Komba Lituhi Nyasa
 Washiriki wa Mdahalo wakifuatilia Mdahalo huku wakipata vinywaji baridi katika ukumbi wa Kept Komba Lituhi Wilayani Nyasa Mkoa wa Ruvuma
 Picha ya pamoja washiriki wa mdahalo na uongozi wa Mtandao wa RUNECISO ambao ndio waandaaji wa Mdahalo kwa Ufadhili wa FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY na wawakilishi wa Serikali
 Baadhi ya washiriki wa Mdahalo wakibadilishana mawazo nje ya Ukumbi mara baada ya kutoka katika Ukumbini.
 Wengi wamezoe kuona mifugo ya aina mbalimbali ikizagaa kama Mbuzi, Ng`ombe, kuku na Kondoo lakini kwa Mji mdogo wa Lituhi ni tofauti pichani ni Nguruwe ambao wanafugwa kama kitega uchumi kwa wananchi wa Lituhi wilaya ya Nyasa.
 Pichani kulia Mwenye shati la kijivu ni Mwasibu wa Mtandao wa Asasi za Kiraia mkoa wa Ruvuma RUBECISO Francins Mlimila akiwa safarini kutoka Songea mjini kuelekea kwenye Mdahalo Lituhi wilayani Nyasa  km 176 kutoka Songea Mjini.
Dereva wa Basi la Mapenzi ya Mungu Hassan Hassan linalosafirisha abiria kutoka Songea - Liuli akiwa safarini na Viongozi wa Mtandao wa RUNECISO wakielekea kwenye Mdahalo juu ya Usawa wa Kijinsia Lituhi

Picha ya Chini ni Basi la Mapenzi ya Mungu likifanya safari kutoka Songea kuelekea Lituhi ambalo walokuwemo viongozi wa Mtandao wa RUNECISO wakielekea kwenye mdahalo wa Usawa wa kijinsia
Afisa Mtendaji wa Kata ya Lituhi Bw. Chawala akichangia mada katika Mdahalo wa wazi juu ya Masuala ya Kijinsia uliofanyika Ukumbi wa Kept Komba Lituhi ambao umeendeshwa na Mtandao wa mkoa wa Ruvuma RUNECISO kwa ufadhili wa FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY.
 Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi za Kiraia Mkoa wa Ruvuma Michael Mahecha akitoa ufafanuzi kwa washiriki wa Mdahalo wa wazi juu ya Masuala ya Kijinsia katika ukumbi wa Kept Komba Lituhi Wilayani Nyasa, kulia kwake aliyekaa ni Mratibu wa RUNECISO Bw Juma Nyumayo.
 Washiriki wa Mdahalo juu ya Masuala ya Kijinsia wakifuatilia kwa makini mada ya usawa wa kijinsia wakati mwezeshaji akiielezea.
Picha ya Chini ni Katibu wa Matandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Ruvuma A/InspFadhila Chacha akitoa mada juu ya Masuala ya Usawa wa Kijinsia katika Kijiji cha Lituhi Wilaya ya Nyasa Mkoani  Ruvuma ambaye aliombwa na wanaoishi katika Mwambao wa Ziwa Nyasa kutafuta suluhu kuhusu unyanyasaji wa wanaume kunyimwa unyumba na wake zao.
Baadhi ya washiriki wa mdahalo wakisikiliza kwa makini masuala yanayohusu jinsia na maendeleo katika Mdahalo wa wazi juu ya Usawa wa Jinsia kwa Maendeleo uliofanyika katika Ukumbi wa Kept Komba Lituhi Wilayani Nyasa.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Lituhi wakisikiliza jinsi ukatili wa kijinsia unavyoweza kukwamisha maendeleo ya watoto kielimu na kuwaathiri katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha.
 Washiriki wa Mdahalo juu ya Masuala ya Usawa wa Kijinsia wakionyesha kuguswa na mada kwa kulinganisha na mazingira yao, hapo wakifuatilia kwa makini ili waelewe namna ya kuzingatia usawa wa kijinsia kwa maendeleo yao
 Washiriki wa Mdahalo wa Masuala ya Usawa wa Kijinsia wakichangia mada katika Mdahalo uliofanyika Lituhi Wilayani Nyasa.
Washiriki wa Mdahalo wa usawa wa Kijinsia hapo juu ni mzee akiandika mawazo yake ili achangie juu ya masuala ya usawa wa kijinsia yanavyorudisha nyuma maendeleo

No comments:

Post a Comment