KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, January 18, 2013

UCHAWI NIMOJA YA FANI KWA JAMII FULANI .TUFANYEJE ILI KUWARUDISHA KWETUNdugu zangu wasomaji wa Blog ya Songea Habari napenda kuwapongeza kwa mwaka 2012 kwa kutoa ushirikiano wa kuweza kuchangia katika Masuala yanayohusu jamii hasa jamii inayoishi pembezoni mwa Nchi na kuonyesha changamoto zinazowakabili.

Kwa habari za kina nilikuwa nikiifahamisha Jamii kwa kitu kinachoitwa uchawi ambacho ndicho changamoto kwa watu wanaoishi pembezoni.

Watu walio wengi huingiwa na hofu kufanya Maendeleo kwa kile kinachoitwa woga wa kuuwawa au kulogwa. Kwani sumu ya kitu uchawi ni kuona maendeleo ya mtu mmoja mmoja.

                 Mganga wa jadi bint Frola Ndembo
Nikiwa katika kambi ya Mganga mashuhuri wa Nyanda za juu Kusini Mama Binti Flora Ndembo nimeweza kupata siri kubwa kuhusu uchawi. Wachawi wenyewe wamesema wamejiingiza katika uchawi baada ya kuona Jamii ikiwatenga, wale ambao ambao hawana uchumi wa kutosha ndio wanaunda umoja wa kuwatesa wenzao.
Add caption


Mkuu wa Wachawi kutoka Mwambao wa Ziwa Nyasa akiwa amesimama akieleza Jinsi alivyojiingiza katika Uchawi. Mguu unao uona wa kulia uliovimba kama Rungu, huo Mguu ni gia ya kupaa angani akigonga na Mguu wa kushoto ndipo huanza kuruka akielekea eneo alilo panga.

Tu kiachana na Mchawi mkuu wa Mwambao wa Ziwa Nyasa sasa tuangalie mchawi  wa Matimila Songea Vijijini ambaye alimua mtoto wake ambaye alikuwa Padiri akitangaza kujitoa katika Uchawi  amesema ameamua kujitoa baada ya wachawi wenzie kumuua mtoto wake ambaye alifikia ngazi ya kuwa Askofu; hapo ndipo alipoona kuwa uchawi hauna maana.

Nikiwa mchambuzi wa habari za ushirikina  niliamua kumuulizaa mzee kuwa mtoto wake ambaye alikuwa mtu wa Mungu aliwezaje kuuwawa wakati yeye ndiye aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wachawi. Alijibu hakuna mtu anayeweza kuuwa katika ukoo kama ndugu hajaidhinisha na sheria hiyo hufuatwa kwa makini ukikiuka taratibu unauwawa mwenyewe “ndivyo ilivyonikuta kwa mototo wangu

 
Nikiwa katika Kambi hiyo ya Binti Ndembo nilikutana na Mwenyekiti wa wachawi katika maeneo ya Mwambao wa ziwa nyasa. Yeye anasema alijitenga na Jamii na alikuwa akiishi mashambani ambako ndiko kulikuwa Makao Makuu ya Mikutano ya wachawi wote.
Yeye anasema alijiunga na uchawi baada ya kaka yake kuweka rehani mwili wake baada
wa kuuwawa au kulogwa. Kwani sumu ya kitu uchawi ni kuona maendeleo ya mtu mmoja mmoja.
Nikiwa bado katika Kambi hiyo ya Binti Ndembo, nilitiwa na fadhaha baada ya kumuona Binti mwenye umri wa miaka 10 aliyepewa uchawi na Mama yake na kuweza kupewa mboga ya akiba ambacho ni kidonda kilicho ubavuni ambacho yeye alikiri kuwa akikosa mboga hutumia kwa kuchovya kwenye kidonda. Maskini Binti huyo katika maisha yake hadi kufikia miaka hiyo 10 alikuwa akichukia shule kama nini lakini baada ya kufika kwa Binti Ndembo ameacha uchawi na kuomba akaendelee na Masomo

Kamanda wa POLICE aliye hamia Iringa Maiko Kamhanda kushotona Kamanda Mpya Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Kaizilege Nsimeki
 Ndugu yangu nikiwa katika kambi hiyo na Binti Ndembo nimeona mambo mengi cha kufurahisha mganga huyo hana uchochezi. Yeye amekuwa akipatanisha ndugu hao na kuwa Jamii moja. Nikiwa Kambini hapo nimeshuhudia Viongozi wa ngazi za juu akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma akitoa elimu Shirikishi kwa kutaka Jamii iachane na Mambo ya Ushirikina.

Mganga huyo mashuhuri mbali ya kutibu watu wenye asili ya Ushirikina lakini hata hivyo ameshaweza kukamata Majambazi Sugu, na wao kusalimisha silaha zao na kuachana na Ujambazi.

Jambo la kuingilia Masuala ya Ujambazi, Mganga huyo mashuhuri amepata misukosuko kwa kuwahi kupigwa risasi mbili na kukimbizwa Hospitali ambako alitolewa.

Amewahi kufungwa Kamba na kutupwa msituni na kuambiwa aachane na masuala ya kufuata Majambazi lakini uganga wake uliweza kumwokoa.

Pia kwa Mara ya Kwanza Mganga huyo aliweza kubainisha ndoa iliyofungwa kati ya Mama na Mtoto wake wa kuzaa mwenyewe. Hatimaye aliweza kuibainisha Ndoa hiyo hadharani.

   Ndugu zangu wasomaji, Shabaha yangu ni kutaka kuendelea kupata mawazo kutoka kwenu, kitu kikubwa ambacho kinasababisha Maendeleo kuto chukua Kasi ni Kushiriki katika Mambo ya Ushirikina.   Sasa hapa tumeona watu walio wengi wakiacha Uchawi na kutangaza Hadharani.

  Hii ni Ruvuma Jee Mikoa mingine Ukombozi utatoka wapi?
 Wasomi na watu wenye Vipaji watume Elimu yao kuutokomeza Ushirikina na wale wenye Ushirikina wajitoe Hadharani kuachana na USHIRIKINA.   
No comments:

Post a Comment