KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, September 10, 2013

WAZIRI WA ELIMU AELEZA NIA YA SEREKARI KULETA MABADILIKO KWA WATANZANIA

 Waziri wa Elimu Shukuru Kawambwa akikagua Maabara ya St Joseph Tanzania Songea
 Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti akiwa katika Maandamano kwa wahitimi wa Sitashahada na Shahada wa Chuo kikuu cha St Joseph Tanzania katika Tawi la Songea
 Wanawake walio hudhulia Maafali ya kuhitimu wanafunzi wa chuo kikuu cha st, Joseph
Rais wa wananzi wa Chuo kikuu cha St. Joseph akipokea zawadi baada ya kufanya vizuri katika uongozi na Masomo

Rais wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph chenye Makao yake Makuu Nchini India, Arul Raj ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwaunga mkono katika suala la Elimu pia ametoa shukrani kwa Serikali kuonesha nia ya kutoa Aridhi kwa ajili ya mafunzo ya kilimo. Ameomba serekari kuunga mkono swala la kilimo katika chuo cha st joseph tanzania


Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo la Mbinga John Chrisostom Ndimbo amesema Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Tanzania kinapokea Wanafunzi wa Dini zote ili kukuza umoja na Mshikano wa Tanzania.


 W
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Songea wakipokea wageni waalikwa waliokuja kushuhudia Mahafali ya Nne ya Wanafunzi waliohitimu Elimu ya Juu ya Sayansi
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru Jumanne Kawambwa akionyeshwa Mahabara ya Chuo Kikuu cha St Joseph ilivyokamilika kwa vifaa
Wanafunzi wa Sekondari ya Ruhuwiko wakiwa katika Mahafali ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph
Wazazi wakiwa katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph kuwashuhudia watoto wao wakitunukiwa Shahada na Stashahada ya Elimu ya Juu ya Sayansi

Wanafunzi waliohitimu Mafunzo ya Sayansi wamewaomba wenzao kutoogopa Masomo ya Sayansi pia wameomba Mikopo inayotolewa kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu itolewe mapema.


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania toka Mwaka 1961 ilikuwa na Wanafunzi wa Chuo Kikuu 13 tu lakini hadi hivi sasa ina Wanafunzi wa Chuo Kikuu 170,000 na katika mwaka 2005 ilitoa Mikopo kiasi cha Shilingi bilioni 56.1 na mwaka 2012 imetoa mikopo shilingi bilioni 326 hata hivyo mikopo hiyo ni kwa wanafunzi wa shahada tu nayo haijawafikia wote.

Hapo ni Fundi Mitambo akihakikisha Matangazo yanakwenda barabara katika Sherehe za Mahafali ya Wahitimu wa Elimu ya Juu ya Sayansi yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Ruhuwiko Songea

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr.  Shukuru Jumanne Kawambwa amesema ili kupata Maendeleo Serikali imeazimia kufundisha Wataalamu mbalimbali  wa ngazi ya Uhandisi wapatao 414,000 ifikapo Mwaka 2015.

Waziri wa ELimu na Mfunzo ya Ufundi Dr Shukuru Jumanne Kawambwa ameyasema hayo wakati akiwatunuku Shahada na Stashahada Wanafunzi Wahitimu 97 katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Josefu Tanzania Tawi la Songea


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr.Jumanne  Shukuru Kawambwa amesema lengo kuu la Serikali ni kuhakikisha kuwa inawasomesha Wataalamu mbalimbali ili kuongeza ujuzi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuinua uchumi nchini mwetu

Wageni waalikwa kutoka Maeneo mbalimbali wakifuatilia Hotuba ya Mgeni Rasmi katika Mahafali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Tanzania tawi la Songea.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakihakikisha wanapata kwa usahihi yaliyojiri katika Mahafali ya Wahitimu wa Chuo kikuu cha Mtakatifu Joseph tayari kwa kuwafikishia Jamii.
Hapo Waandishi wa Habari kutoka TBC na Star Tv Songea wakichukua Habari katika Mahafali ya kuhitimu Elimu ya Juu (Chuo Kikuu) ya Sayansi

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr.Jumanne  Shukuru Kawambwa amesema lengo kuu la Serikali ni kuhakikisha kuwa inawasomesha Wataalamu mbalimbali ili kuongeza ujuzi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuinua uchumi nchini mwetu

Wanafunzi wahitimu wa Elimu ya Juu ya Sayansi waliotukiwa shahada na stashahada kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Josefu Ruhuwiko Songea

No comments:

Post a Comment