KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, July 7, 2015

MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID THABIT MWAMBUNGU KUSHIRIKI FUTURU NA VIONGOZI WA DINI IKULU NDOGO SONGEASerikali Mkoani Ruvuma imetoa tahadhari kwa wale wote waliojiandaa  kufanya vurugu wakati tukielekea katika uchaguzi  kuvuruga Amani tuliyonayo, Serikali itachukua hatua kali za kisheria   za kupambana na watu hao
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu ameyasema hayo katika futuru ya Mwezi wa Ramadhani iliyoandaliwa Ikulu ndogo ya Songea na kujumuisha Waumini wa Dini ya Kiislamu na Wakristu wakiwemo  ma Askofu na Masheikh

Wanawake wakiwa katika futuru iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga wamewaomba wanawake wenzao kusimamia maadili ya vijana na watoto wao majumbani wanaokengeuka kwa kutamani kuchochea vurugu na kupoteza amani iliyopo. Wamesema wamama kama walezi wa familia wana wajibu wa kuelimisha watoto wao na kuzuia kujiunga na masuala yanayoashiria uvunjifu wa amani.

Miongoni mwa Viongozi waliohudhuria Futuru ya Mwezi wa Ramadhani iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga, Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Bakari Nalicho, Viongozi wa kisiasa na viongozi wa dini ya kikristo ngazi ya mapadre na Maaskofu
Waumini waliohudhuria katika Futari ya mwezi wa Ramadhani 2015 Ikulu ndogo Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wameomba Viongozi wa Dini kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha Amani ya Tanzania inaendelea kudumishwa kwa kuhubiri amani upendo na Mshikamano katika Misikiti na Makanisa na hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Oktoba 2015.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amesema dalili ya mvua ni Mawingu lakini Serikali imejidhatiti kukabiliana na Vurugu zozote zitakazojitokeza , Serikali  haitamvumilia Kiongozi yoyote wa dini au wa Kisiasa   kufanya uchochezi kwa waumini wake ili kuhatarisha amani serekari ita kuwa macho muda wote.Sheikh wa Mkoa wa madhehebu la  Suni Shaban Chitete aliweza kuiombea Nchi ya Tanzania ili iendelee kuwa na Amani pamoja na kuwalinda viongozi waliopo .

No comments:

Post a Comment